Halotel mnanikera





[HALO SOKA] Wajuwe Mabingwa wa Ligi kuu ya Uingereza msimu huu.Pata taarifa LIVE za timu uzipendazo kama StokeCity vs ManCity, Burnley vs Liverpool,LeCity vs Arsenal tuma neno LIVE PL to 15602. Ahsante!
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji122] naona umeedit/ au umesaidiwa na Moderetor.

Nashukuru kwa kuelewa ulichokiandika ni upuuzi.
Mwanaume kamili ni aibu kusema neno My #$@/@.
Shame on You Never repeat again tht word kama kweli ww Ni Rejali.
Utakapoacha Kunzungumza kama muhuni ndipo jamii ya watu Intellectuls kama Halotel wanaweza kukjibu hoja zako ..
Otherwise unaweza kuonekana hata hizo sms unaziona msimu baada ya kua umeshapata Steam za Bangi.
MPE msaada, Mkuu uandishi wako tu, nami nimehis utakuwa in mfanyakazi Wa halotel. binafsi sijapendezwa na jamaa an anavoropokaropoka kwani hapa so mahal anapoweza pata msada kuliko angepiga no. 100
 
Asalaam ndugu zangu! Poleni ni harakati za kulainisha vyuma kwa grease! mungu ni mwema kwa wale wenye changamoto za kimaisha mungu yu pamoja nanyi!
Bila kupoteza muda naomba niende kwenye hoja yangu moja kwa moja...... Nimekuwa mteja mzuri sana wa haloteli tangu mwaka 2016, Baada ya kuvutiwa na huduma zao ila kwa sasa naona mimi pamoja na kundi langu kubwa nililolishawishi tumewachoka kwani huduma zenu zimeoza na zinanuka!
kwanza mmekuwa na kawaida ya kuiba MB mfano kuna siku nilijinga 1 GB na kuingia whatsupp tu ila baada ya muda nakuta MB 400 Hivi kuna whatsupp ya kutumia MB 600 bila kudownload wala kuandika kitu na whatsapp yangu autodownload ipo off! nikawapotezea!
Juzi nikaweka vocha lakini kwa sababu nilikuwa busy nikashindwa kujiunga kifurushi chochote! lakini baadae kutaka kujiunga nakuta wamepunguza Tsh 50/- Nikaona sio mbaya ngoja niwaulize huduma kwa wateja hii kitu imekaaje? Ebhanaaa eee nilikutana na dada mmoja sijui alikuwa kagombana na bwana yake ananijibu kwa ukali na wakati hata hanijui! ananiambia kuwa nimejiunga halowin nikabaki nashangaa kwa sababu mambo ya bahati nasibu huwa sishiriki kabisa! nikawa namwambia bhasi naomba unitoe na hiyo huduma maana mimi siijui! alichonijibu ni kuwa halowin huwa haijiungi yenyewe utakuwa umeunga wewe hivyo na kutoa utoe wewe! kisha akakata simu kiukweli nilijisikia vibaya sana na huduma ya yule customer care!
Sasa leo ndio maamuzi ya kuukimbia huu mtandao pamoja na jopo langu umefikia na ninaahidi kufanya kampeni ya kuichafua haloteli ni kuwa iko hivi....... jana jioni nilinunua vocha nikaweka kwenye wallet! sasa asubuhi kama unavyojua sisi wanaume wa mikoani nikawasha pikipiki yangu nikavaa mabuti yangu na kuanza safari ya shamba! Bahati mbaya wakati wa kurudi mvua kubwa ilianza kunyeesha nipo njiani hakuna hata kwa kukujikinga! vitu vyote nilivyokuwa navyo vikalowa isipokuwa simu sababu huwa sibebi simu shamba! vocha ikalowa chapa chapa pia nilivyofika home nikaikausha ikakauka lakini kila nikikwangua ili niweke namba ule ukungu wa juu ukawa unatoka na namba! ikabidi nipige huduma kwa wateja sabau serial namba zilikuwa zinaonekana vizuri! safari hii mtoa huduma kwa wateja alinijibu vizuri tu akasema kwa sasa hawana huduma hiyo hivyo nifike halotel shop wanibadilishie vocha! na kwakua duka hilo lipo mtaani kwangu sikupaa shida nilifika fasta ila nilichokikuta kilinitia hasira sana! nilimkuta kijana bishoo namueleza shida zangu ma yeye naona kama ananifokea hivi kuwa kwanini nimelowesha vocha? mimi vocha za kubadilisha sina! nimewasaidia wengi sana hahaha! sikumjibu kitu nilichofanya niliitupa ile vocha yangu kwenye dust bin na kuondoka heri nusu shari!
Hayo ndiyo yaliyonikuta katila mtando wa halotel yapo mengi ila hayo ni kwa uchache! mimi naahidi kulala na ninyi halotel mbele!
 
Mi niulizie hao watu wa halotel hii halowin yao huwa wanachezesha lini? Mi naona tatu mzuko na Biko tu wao kila nikiweka vocha basi ni mitext tu inaingia
 
Hawa jamaa nimewaacha juzi rasmi.

Baada ya kukatakata mb na pesa bila maelezo,napigia castomer care wote ni kama wajawazito hivi,kwanza wanaonekana hata hawajui nini kimewaweka hapo.

Imagine mtu unamuuliza swali sensitive anakujibu,hujui matumizi ya mb kweli *****.natumia internet kabla hamjaajiriwa na hiyo kampuni mbuzi yenu.
 
Mbona umelalamika na kuumia sana?kama customercare ni poor wateja watahamia kampuni nyingine,na namshauri kama haridhiki na huduma za halotel atafute kampuni nyingine ili apate anachokitaka.
.........alaaah mteja ni mfalme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…