Siku ya tarehe 17.7.2021 nilitoa pesa kimakosa kwa kukosea namba ya wakala.
Nikapiga simu wakasema wanashughulikia irudi. Nisubri masaa 72. Baada ya masaa hayo message ikaingia kwamba pesa imerudishwa kwa wakala.
Sasa baada ya hapo nimeendelea kupiga simu majibu yanayotoka ni
1. Kusubiri masaa 72 kutokea tarehe hiyo tarehe 17 imagine masaa 72 yamepita mangapi mpaka leo August 3
2. Nimekwenda kwenye ofisi zao kufuatilia wakaniambia ndani ya masaa mawili hiyo hela itakuwa imerudi. Nikapewa namba ili isipokuwa imerudi nipige. Ila hiyo namba haikupokelewa mpaka leo
3. Customer care namba 100 mpaka sasa hawapokei simu yangu.
Nachotaka kujua kwamba halotel pesa yangu mmenitapeli au wiki zaidi ya mbili mnanisumbua na simu yangu mmeacha kupokea.
Kama halotel wamo humu naomba mtu anisaidie kuwatag.
Huduma za pesa ni bora uwe unatumia m- pesa,
Halotel ukitaka kutuma pesa mda mwngine jina la mtu unaetaka kumtumia halifik kuna jamaa alikosea kutuma elf 50 akapiga huduma kwa wateja hakupew majib yanayoeleweka