Halmashauri zitakazokuwa chini ya UKAWA

Halmashauri ya wilaya kilombero na Halmashauri ya mji ifakara zote zitakuwa chini ya CDM
 
Dah mkuu yaani bora kuachia ngazi unamaanisha kujiuzuru udiwani kuliko kutokuwa mwenyekiti wa halmashauri, iliwa madiwani wa chama chake ni wachache sioni atapataje huo wenyekiti, huko ni sawa na kusema leo kambi ya upinzani ipiganie ipate spika kutoka upande wao.
 
halmashauri ya wilaya kyerwa. chadema madiwani 10 ( ccm diwan 7 + diwani tatu wa pingamizi za kisenge = 10)
 
kumbuka chadema walishonda jimbo la kyerwa kumtumia benedicto mutungirehi na mkurugenzi katangaza kwa nguvu ccm
 
Halmashauri ya manispaa ya kinondoni jimbo la kawe,ubungo,kibamba,kinondoni zote ukawa.......
 
Jamani nawashauri sana halmashauri zote zitakazokuwa chini ya uongozi wa UKAWA kupiga kazi ya ukweli na kuleta maendeleo yanayoonekana kwa wananchi ili wananchi walichagua upande wa pili katiaka halmashauri zao waone waziwazi kuwa walikosea na uchaguzi ujao wafanye uamuzi sahihi.
PEOPLE'S........
 
Ndsio kitu hata mimi nilikuwa nakiwaza. Ukawa District Councils MUST
show the difference!
 
Ukitoa CHADEMA na NCCR, wale UKAWA wengine wamepata madiwani wangapi?
 
Dah! niliona sehemu wanasema zinafika 22 si haba.


hii hata mm nimeipenda....muhimu kuwa makini....ccm hawakosi strategy ingine hata km ukawa/vyama husika kuna mtu anaweza kuwa meya/mwenyekit wa halmashauri wakamundaa na kumpa pesa mpk ashinde alafu aje kuhumu wenzake.....km vile halmashuari fulan sijui ni mwanza au bukoba sikumbuki vizuri meya alijuzuru akajiunga na ccm......tuwe makini
 
Nafikiri baraza la madiwani linauwezo wa kumkataa mkurugenzi au kutoshirikiana naye.
 
Hakika ni kweli watuonyeshe mabadiliko
 
Na ndio kitu cha msingi saaana wajitahidi kupunguza ufisadi kwenye tenda za halmashauri .na
 
Umenena....kale ka tabia ka wakurugenzi kupleka hela SISIEM ka shughuli za chama kwa Halmashauri hiz katakoma
 
Pia Arusha Mjini, Arumeru Magharibi, Monduli, Babati Mjini, Simanjiro, Longido, Loliondo

Logindo sina uhakika, unaweza kututajia idadi ya Madiwani kwa kila chama? Mwenye taarifa pia ya Ngorongoro tafadhali aje nazo! Kwa mkoa wa Arusha ongeza Karatu ambayo iko chini ya cdm since 2000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…