Vox Populi Vox Dei
Member
- Jun 30, 2013
- 21
- 14
Halmashauri mpya ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara haijapata fedha za uendeshaji kutoka serikalini kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Novemba 2013 hadi sasa.Kufuatia hali hiyo,shughuli mbali mbali katika halmashauri hii zimekwama ikiwa ni pamoja na malipo mbalimbali ya watumishi kama uhamisho,posho na fedha za malipo ya nauli za likizo hususan walimu.
Walimu wote walioomba na kukubaliwa kwenda likizo hawajalipwa fedha zao hadi sasa likizo imekwisha.
Pia madiwani katika halmashauri hii wameshindwa kukaa vikao vya kawaida vya baraza kutokana na ukata unaoikumba halmashauri hii.
Sambamba na hilo,magari mengi katika halmashauri hii hayafanyi kazi kutokana na halmashauri kukosa fedha za mafuta.
Itakumbukwa kuwa halmashauri ya Rorya ni miongoni mwa halmashauri zinazoongoza kwa kupata hati chafu kutokana na matumizi mabaya ya fedha za Umma.Kupatikana mara kwa mara kwa hati chafu katika halmashauri hii kunatokana na watendaji wake wengi kugeuza halmashauri kuwa kijiwe cha kugawana posho.