Halmashauri Ya Jiji la Arusha

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAISI
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA JIJI ARUSHA


Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. CD/E.40/3/103 Tarehe: 01 Machi 2016

● Makatibu wa Wilaya
Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu
Halmasahuri ya Jiji
ARUSHA

TANGAZO LA UCHAGUZI NA UTARATIBU WA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WAMUCHAGUZI MDOGO WA SERIKALI ZA MITAA 2016.

Marejeo ni mada kaririwa hapo juu.

Napenda kuwajulisha kwamba nimekuambatanishia MAELEKEZO YA UCHAGUZI niliyoyatoa kwa umma na pia Ratiba ya Uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 17 April 2016 katika Mitaa 8 kwenye Kata 8 katika Halmasahuri ya Jiji la Arusha.

Nawajulisha pia kuwa zoezi la kuchukua fomu kwa Wananchama wenu wenye sifa na wanaotaka kugombea uongozi katika uchaguzi huu mdogo litaanza rasmi tarehe 09 Aprili 2016 kwenye Ofisi za Maafisa Watendaji wa Mitaa au Kata husika, na litaendelea kwa siku saba (7) hadi 16 Aprili 2016 ambayo pia itakuwa siku ya kufanya uteuzi utakaofanywa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi.

Hii inafuatia kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa nafasi hizi zilizo wazi kulikofanywa na Ofisi yangu kwa kushirikiana na Viongozi wa vyama vya Siasa wakiwa Wadau Wakuu wa Uchaguzi huu kadri ya barua yangu Kumb .Na CD/E.40/3/99

Kwa nakala ya barua hii, Maafisa Watendaji Kata (WEO) wanatakiwa kuwajulisha na kusimamia viongozi wa Mitaa husika kusimamia zoezi hili la kukabidhi barua hizo.

Nawatakia maandalizi mema


J.A.R Iddi
MKURUGENZI WA JIJI
ARUSHA

Nakala;
: Katibu Tawala (M)
S.L.P 3050 - Kwa taarifa

: Mkuu wa Wilaya
Arusha - Kwa taarifa
: Mkuu wa Polisi (W)
Arusha Mjini - Kwa taarifa

: Mkuu wa Usalama wa Taifa (W)
Arusha Mjini - Kwa taarifa

: Mkuu wa TAKUKURU (W),
Arusha Mjini - Kwa taarifa

: Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi (Kata/Mitaa husika tu
Halmashauri ya Wilaya Arusha - Kwa Taarifa
: Maafisa Tarafa
Arusha Mjini - Kwa Taarifa
 
Back
Top Bottom