Mkosasura Ng'ong'a
Member
- Jan 25, 2016
- 32
- 64
Taarifa kutoka kikao cha Baraza la Madiwani, zimetonya kwamba kuna ubadhirifu wa kutisha Halmashauri ya Pangani. Miongoni mwa maeneo ambayo yametajwa ni pamoja na Mradi wa Maji uliofadhiliwa na Benki ya Duni ambapo Shilingi 800 milioni hazieleweki zimetumika-tumikaje mpaka sasa. Mwenyekiti wa kamati husika, Diwani wa Pangani Mashariki, ameshindwa kutoa taarifa mbele ya kikao. Mbali ya pesa hizo kutumika, tatizo la maji mjini Pangani bado sugu, na kwa miezi isiyopungua mine (4) baadhi ya maeneo hayana maji. Maeneo hayo ni pamoja na ofisi za ofisi ya mkuu wa Wilaya na nyumba za Halmashauri zilizopo Mkoma.
Baraza la Madiwani pia limeibua ni malipo hewa ya fidia kwa wananchi walionyang'anywa mashamba yao na Halmashauri kwa ajili ya upimaji viwanja. KUMB.NA.HWP./ A.20/ 1/ VOL.IV/ 101. Wafanyakazi wa idara ya ardhi, ambao ndiyo miongoni mwa vinara wa rushwa waliokubuhu Pangani, kwa kuuza maeneo yanayotwaaliwa kupimwa viwanja na Halmashauri. Wafanyakazi wa Idara hii wamekuwa mwiba wa haki za wananchi Pangani kwa muda mrefu. Hata baada ya taarifa kadhaa kutolewa kwa vyombo husika, bado wamejimilikisha maeneno kadhaa na wanaendelea kuwanyima wanachi haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kukataa kuwapimia maeneo bila kupewa malipo, na kukalia hati za viwanja vilivyopimwa kwa muda mrefu bila sababu na hivyo kuikosesha serikali mapato.
Taarifa ndani ya Baraza zimethibitishwa kushindwa kwao Mkurugenzi wa Halmashauri kuwasilisha nakala za mikataba iliyoingiwa na Halmashauri au ankara kuthibitishwa malipo kwa walionyang'anywa mashamba na "kufidiwa." Baraza la Madiwani, kupitia Kamati ya Uchumi, limeamuru aliyekuwa mwanasheria wa halmashauri na ambaye sasa amehamishiwa Mkoa mpya wa Songwe arejeshwe kuonyesha nakala za mikataba bandia aliyoingia kwa niaba ya halmashauri.