Halmashauri: Moja ya chanzo cha umasikini kwa taifa

Huo ndiyo ubunifu tunaouhitaji. Ma injinia wengi wa manispaa/majiji/halmashauri sidhani kama wanalijua hilo zaidi ya kusubiri tenda na kulamba 10%
 
Miaka 10????Utakuwa umeendekeza "chini"!Nilitaka kukuelewa lakini hapo siwezi kukuelewa!Mtu mwenye muda huo kazini anatakiwa awe na maendeleo zaidi ya hayo. Akiwa na ufahamu mkubwa anaweza kuwa na maduka ya jumla hata matano!Wengine kwa miaka hiyo atakuwa anamiliki combine harvester achana na kuvuna guni 1000!nini gari 2 au nyumba 2 bhana, tutafute wezi wa hela na kuacha wivu wa kipuuzi!Usipojua mwenzako kawekeza wapi haikupi tiketi ya kudhani hana mradi!
 
Huo ndiyo ubunifu tunaouhitaji. Ma injinia wengi wa manispaa/majiji/halmashauri sidhani kama wanalijua hilo zaidi ya kusubiri tenda na kulamba 10%
Hapo bado pana shida hasa kwa zama hizi za UKUTA. Mhandisi anaweza hata kusanifu size na idadi ya mabomba na viungo vyake vyote, na akapendekeza na shortest route!Lakini hawezi kununua mabomba kwa mshahara wake!Ukisema wananchi wachangie, kina TL wanasema ni wajibu wa serikali!Lazima siasa zikome kwanza wakati wa kazi badala ya kulaumu wahandisi ama wataalamu wengine
 


Kuwataifisha na kuwanyonga ni bora zaidi ili iwe fundisho kwa wengine watakaokusudia kufanya haya. Uncle Magu fanya kweli, uwavajilie njuga hawa wazezeta na kuwanyonga.
 
MTENDAHAKI ni ukweli usiopingika awamu za serikali zilizopita zilichangia sana kudumaza ubunifu wa watendaji serikalini. Siyo ma injinia tu bali hata watu wa mipango miji, ma bwana afya (mfano masoko mengi ni machafu sana, niliwahi tembelea moro kipindi fulani nilijiuliza bwana afya ana kazi gani, yaani sokoni utadhani ni jalala, linanuka mavi), sehemu kubwa hawana ubunifu. Nadhani mjadala huu ingependeza kama ungepewa muda wa hewani kwenye TV wadau wajadili njia muafaka ya kuongeza ufanisi wa hawa watu, la sivyo Dkt Magufuli anaweza maliza 5 years wakati mambo bado magumu
 
Exactly
 
Kwenye nchi za wanaotumia juhudi na maarifa, Serikali za Mitaa na Vyama vya Ushirika ndizo zinazoajiri watumishi wengi tena kwa mishahara mikubwa kuliko ya Serikali Kuu! Serikali za Mitaa ndizo zinazosukuma maendeleo ya wananchi kwani Serikali inahangaika na mambo machache ya Kitaifa bila ajizi. Hapa kwetu Serikali za Mitaa zinatumika kama vyombo vya kisiasa na siyo maendeleo!
 
labda miaka ya nyuma kuanzia 2013 kurudi chini kwa ufupi kuanzia 2013 mwishoni halmashauri zote zinapumulia mashine na ni fedha za UNCEF ndio zinafanya kazi
 

Mkuu kuna tofauti kubwa sana kati ya muajiriwa na mfanya biashara, ukinisoma vizuri utaelewa nini nilikuwa namaanisha. Huwezi kumiliki hiyo mali tajwa huku hatuoni uhusiano wa input zako kwenye huo utajiri wako, mfanyakazi wa serikali anaelipwa mshahara wa 1.2 mil au 2mil kwa mwezi akiwa hana biashara yoyote wala mkopo wowote anamiliki mali ya zaidi ya 200mil halafu unaniambia wivu? Kama umeanza kazi na mshahara wa 2mil ukaweka akiba ya 1.5mil kwa miezi sita utakuwa na mil 9 ambayo inaweza kuwa mtaji, ukafanya biashara fulani kwa miaka fulani ukamiliki hiyo mali ya 200mil hatuwezi kuwa na shaka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…