Halima Mdee aishiwa nguvu, tangu afikishwe Polisi Oysterbay aligoma kula

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,498
54,923
_HMB0488.JPG

Heshima kwenu Wakuu,

Mbunge wa Kawe ambaye amefungwa Korokoroni Masaa 48 kwa matakwa ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, amegoma kula akishinikiza kufikishwa Mahakamani.

"Tumetoka Osterbay kumjulia hali Mh. Halima Mdee nasikitika kuwafahamisha kuwa hali yake sio nzuri maana tangu jana anakataa kula chakula mpaka pale watakapo mpeleka mahakamani". Amsema katibu wa BAVICHA Temeke.

Vijana walipewa Uongozi Serikalini wametuangusha sana. Naamin watatumia makosa yao kujisahihisha.. Mungu awasaidie. Yaani unamuweka ndani Mbunge wa Wananchi bila kosa kisa cheo chako cha kuteuliwa kimekupa madaraka!. Hii ni aibu kwetu sisi watoto wa Kiume.

Ningemuunga mkono mkuu wa Wilaya iwapo angempeleka Mahakamani akahukumiwa kuliko kujichukulia Sheria mkononi.
 
Heshima kwenu Wakuu,

Mbunge wa Kawe ambaye amefungwa Korokoroni kwa amri ya Mkuu wa Mkoa, amegoma kula akishinikiza kufikishwa Mahakamani. Tumetoka Osterbay kumjulia hali Mh. Halima Mdee nasikitika kuwafahamisha kuwa hali yake sio nzuri maana tangu jana anakataa kula chakula mpaka pale watakapo mpeleka mahakamani.
Daa lakini
 
Mwambie aache kugoma kula chakula atakufa!! Lakini kama ameishiwa nguvu anawezaje kutujulisha??
 
Kwani kukaa ndani saa 48 si ndo ilikuwa adhabu yake aliyopewa na Mkuu wa Wilaya? mahakamani watamshitaki kwa kosa gani?
Akitoka amshtaki Mkuu wa Wilaya kwa kumuweka ndani bila kosa.

Ukisoma sheria inayompa nguvu Mkuu wa Wilaya kumuweka ndani mtu kwa masaa 48,chini ya sheria hiyo kuna sheria ya kumuhukumu Mkuu wa Wilaya anayemuweka mtu ndani bila kosa.

Kwa hiyo kama hana kosa akiachiwa bila kufunguliwa mashitaka amshtaki huyo Mkuu wa Wilaya kwa kumfunga bila kosa.
 
Kosa lake lilielezwa wazi wakati ametakiwa kukamatwa...acha atulizwe kipago hapo stoo...akitoka atajifunza.

KAMA HAJIFUNZI AKIRUDIA ATADAKWA TENA MPAKA ATAKAPONYOOKA KAMA LEMA.
 
Back
Top Bottom