Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,863
- 5,694
Wapo wanaoshangaa kwanini polisi wanatumia nguvu kuzuia mahafali ya wanachama wa CHADEMA vyuoni wakizani kuwa ni jambo dogo. Kuna sababu ya MSINGI ya kufanya hivyo kwa CCM yenyewe.
CCM inaonekana ipo ndembe ndembe na hoi katika kumiliki na kupata ushawishi ktk siasa za vyuo vikuu. Wamezidiwa kila idara, mikakati, mbinu na hata maarifa tuu madogo.
Kitendo cha polisi kuzuia mahafali ya CHADEMA huku wakiyaacha yale ya CCM kuendelea ni fedheha kubwa sana kwa ccm na serikali yake. Inadhirisha uimara wa upinzani vyuoni na kuonesha udhaifu mkubwa wa CCM.
Kwa wasiojua siasa za vyuo vikuu, vyama vyote vya siasa vikubwa vinafanya siasa na vina viongozi wao wanaowakilisha vyuoni.
Ukweli mchungu ni kuwa CCM haipendwi vyuoni na inachukiwa sana kutoka na matendo yake ambayo huathiri maisha ya wanachuo wenyewe au watanzania wengine. Huo ni ukweli nilio shuhudia mwenyewe pale UDOM mpaka nilipo hitimu shahada yangu mwaka 2011.
Kwa mfano pale UDOM kadi za uanachama za CCM zilikuwa zinatolewa bure kwa anayetaka kujiunga lakini zilikuwa zinakosa wateja na kuwadodea. Lakini kadi za vyama vya upinzani zilikuwa zikiuzwa na watu walikuwa wanazitafuta kila kona na hata kuzimaliza.
Ilikuwa ukionekana umevaa sare ya CCM pale UDOM ni jambo la kustaajabu na hata CCM wenyewe walikuwa wakivalia sare zao ktk magari pindi wanapoenda ktk mikutano yao nje ya chuo ili wasionekane ni wanachama.
Ili ushinde uchaguzi ktk serikali ya wanachuo kigezo kikuu kwa wanachuo kilikuwa ni mgombea kutokuwa mwanachama wa CCM au kufungamana na CCM au kufadhiliwa nacho.
Nakumbuka uchaguzi wa serikali ya wanachuo 2009 mgombea mmoja alikuwa anaelekea kushinda katika kampeni kwa kuwa na sera nzuri kabisa. Lakini upepo ulibadilika siku moja kabla baada ya picha zake kubandikwa zikionesha amevaa sare ya CCM.
Pamoja na mgombea yule kukanusha kuwa sio mwana CCM, aisee aliisoma namba. Alibwagwa vibaya na mtu ambaye hata hakuzaniwa kuwa angeshinda.
Watu walikuwa wakibeba picha za yule mgombea mwenye sare ya CCM na kuzunguka nazo mabwenini madarasani huku wakilia. Walikuwa hawasemi chochote walikuwa wakilia tuu huku wakionesha picha ya mgombea aliyevaa sare ya CCM.
Uchaguzi ulibadilika kutoka kuwa wa serikali ya wanachuo kuwa wa kuikataa CCM na vibaraka wake waliotumwa.
Tangu wakati ule hakuna mgombea aliyekuwa tayari kuonesha mafungamano na CCM, kila mgombea alijinasibu kuwa sio mwana CCM ili aweze kupigiwa kura.
Kimsingi sishangai CCM kutumia nguvu kuzuia mahafali ya chaso maana wameteswa na kuumizwa sana kwa muda mrefu. Wameona aheri watumie bunduki maana njia zote za diplomasia zimefeli vibaya Sanaa.
Hawa wanachuo ni wakaidi na viburi sana. Badala ya kujiunga kwa wingi CCM wanajiunga vyama vya upinzani. Na wanatumia hata mabumu yao kusaidia ujenzi wa vyama vya upinzani, aaaa waache wapigwe tuu bwana hakuna namna pumzi inakata hivyo.
Hiyo ndio hali halisi ya vyama vya siasa vyuo vikuu na sababu za upinzani kuzuiwa kufanya mahafali vyuoni.
Asanteni karibu kwa mjadala wenye hoja za kujenga.