Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Kwa dunia ya leo maendeleo ya nchi huja haraka kutokana na msuguno wa fikra za kisiasa,
Unapoona leo Rais Magufuli anahangaika huku na huko kulitumikia taifa, tambua kuwa ni matokeo ya siasa za upinzani kuwa imara, bila upinzani kuwa imara maendeleo hayatakuja kamwe.
Kulegalega kwa vyama vya siasa hasa mitafaruku ya ndani, kwa mtu yeyote anayependa demokrasia na siasa za maendeleo ni lazima kumsikitishe,
Chama cha Mapinduzi kimekumbwa na mtafaruku ambao mwamuzi atakuwa Juni...., Aina ya utawa wa Rais Magufuli umekifanya chama chake kukimbia kivuli chake, duru za kisiasa zinabashiri mpasuko kuongezeka pindi takwa la kikatiba litakapotimia na usukani wa Chama kushikwa na Rais, Magodfather wanahofia aina ya uongozi wa kada wao huyo hasa kile kinachoitwa kupambana na uhalifu (utumbuaji majipu) ambao kwakiwango kikubwa ulishikiliwa na kushirikiwa na chama hicho, hivyo haraka zote za mapambano ya uhalifu hasa ufisadi na mengineyo yanakibomoa chama hicho kwa kiasi kikubwa.
Pia Chama cha ACT Wazalendo kimekubwa na mtafaruku ambapo kiongozi wao mkuu anaonyesha kusuguana na waasisi wa chama hicho,
Huenda kiongozi mkuu anaipenda demokrasia zaidi ama haitaki kabisa, Waasisi wa ACT Wazalendo Nyakarungu na Mwigamba wamefukuzwa ijapokuwa kuondoka kwa Mwigamba kulitangazwa kwamba anakwenda masomoni, lakini hiyo ilikuwa njia tu yakupita kujinasua na misumari ya mkuu wa chama huku siku za aliyekuwa mgombea wa Urais Mama Anna Mgwira zinahesabika...
Migogoro mingi ndani ya vyama vya siasa inatokana na ukata ama ukwasi. Pia uroho wa madaraka ama wivu wa nyota za kisiasa kwa makada husika.
Vyama vya Muungano wa UKAWA vinaonyesha kuimarika kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miezi sita baada ya uchaguzi hali inayoleta taswira angavu kwa ukuaji wa fikra za kisiasa na demokrasia nchini. Uimarikaji wa vyama hivi unapimwa katika dhana ya uwepo migogoro na mitazamo ya kijamii katika imani yavyo.
Bila upinzani imara Tanzania isahau maendeleo, na CCM itambue kuwa inao wajibu wakuruhusu upinzani ukue ili kuruhusu maendeleo yaletwayo kwa msuguano wa fikra za kisiasa na ikitokea yenyewe ijibidiishe kuwatumikia Watanzania, na sio kufanya juhudi za kuua upinzani ili itawale milele ikiwa gizani.