hali ya uchumi wa tanzania part 1

hali ya uchumi wa tanzania part 1

MTENSA

Member
Joined
Mar 21, 2015
Posts
9
Reaction score
1
Hali ya uchumi wa nchi ni mbaya Sana katika kipindi hichi kuliko hata kipindi cha miongo miwili iliyopita. Uchumi wa nchi unaonekana unakua kwa 7%toka mwaka 2000 mpaka na leo na per capita income imeongezeka kwa 50%, lakini takwimu hizi zime neglect ongezeko la watu (population growth) kwan kuna ongezeko la watu million 1 kwenye kundi la watu million 11 waliokuwa below poverty line na hivyo kufikia million 12 kwa sasa. Hivyo hali ya umaskini imeongezeka badala ya kupungua, kwa mwaka wa fedha 2014/15 GDP ilikuwa $36.6 billion , GDP growth rate ilikuwa 7.4% na GDP per capita income ilikuwa $768. Kutumia GDP Kama kipimo cha kuangalia umaskini in individul bases Ina upungufu Mkubwa kutoa picha halisi ya kiwango cha mapato anayokusanya MTU kwa mwaka maana computation yake inakuwa,
C+I+P+NX
C=total house hold expenditure
I=government expenditure
P=private investment
NX=NET CAPITAL (IMPORT - EXPORT)
Hivyo per capita income ya $768 ambayo kwa exchange rate ya sasa ni 1,536,000/= kwa MTU kwa mwaka ni figure ambayo haiakisi hali halisi ya makusanyo ya mapato kwa mwaka kwa wa anzania wa kawaida ni kutokana na mchango wa hela hiyo kuwa umepatikana toka kwa watu wengine wenye uwezo Mkubwa rejea formula hapo juu.
Kilimo kinachangia 24.5% katika GDP, Viwanda 22.2% na shughuli nyingine 44.3%. Kilimo kinachangia kiasi kidogo ukilinganisha na jinsi sector husika ilivyoajiri watu wengi kwani 80% ya watanzania wanategemea shughuli za kilimo. Hivyo kuna tatizo katika kilimo miongoni mwa matatizo hayo ni bei za mazao, masoko, miundo mbinu, vifaa, mbegu bora n.k.
Usafirishaji wa bidhaa kwa mwaka 2014/15 usafirishaji wa bidhaa kwenda nje (export) ilikuwa na thamani ya $5.754 billion wakati usafirishaji kuingia ndani (import) ilikuwa $10.826 billion hivyo net export ilikuwa $-5.1billion hii inamaanisha tumenunua Sana kuliko kuuza na hivyo kupelekea kushuka kwa thaman ya shilling ya kitanzania dhidi ya dollar ya kimarekani.
 
Back
Top Bottom