Hali ya mapato ya serikali yashuka, serikali haina pesa wananchi tujifunge mikanda

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883
Habari wadau!

Nimepata fursa ya kuongea na kiongozi mmoja toka BOT nilikokuwa nafatilia mambo yangu ya kifedha.

Ni ukweli unafichwa kwa gharama kubwa sana kuwa hari ya kiuchumi wa nchi nimbaya sana.

Mapato ya kodi yameshuka kwa kasi sana na serikali inashindwa kujiendesha vizuri na kuna baadhi ya malipo yamesitishwa hasa kwa wazabuni.

Na njia walio itumia ya kuhamishia makato BOT badala ya hazina ni kuwa kuna baadhi ya taasisi hazitapata fedha kwa wakati hasa makusanyo mbalimbali kama makato ya mishahara na michango mbalimbali kama ile ya mifuko ya hifadhi za jamii, na makato ya hiyari ya taasisi mbalimbali kama vile mikopo nk.

Lengo ni kuzitumia wakati wakikusanya mapato.

Sababu kubwa ya kudorora kwa uchumi inadaiwa ni sera zilizoanzishwa na kupelekea biashara nyingi kufungwa na kuhamisha fedha yoka benki za biashara na kupeleka BOT.

Sasa huko BOT ni vimemo vya maagizo fedha ziende wapi lakni hawafati bajeti pangwa na kujikuta kuwekeza sehemu zisizo na return ya mda mfupi na kuzima mzunguko wa fedha.

Hivyo jamaa kashauri kila pesa unayoipata itunze maana ya kesho haijulikani itakuwaje
 
Hakuna hela BOT
Ndio vizuri sana..

Mi nataka huu utawala ufeli kabisa..

Na Mungu lazima awachape fimbo hawa awamu ya 5..

Mlianza na kuminya demokrasia, kukandamiza upinzani, kukandamiza vyombo vya habari, utekaji nk nk.

Mungu hawezi kuacha waja wake wakiteseka kwa haya yote..

Ndio anawapiga fimbo kwa upande mwingine..

Kila kitu kipo ovyo kabisa kwenye suala la uchumi wa Nchi.. Everything is Stagnant..!!

Malipo ni hapa hapa Duniani.
 
Back
Top Bottom