Hali ya maisha yazidi kuwa tete tz,waandishi wahofia ya tunisia na misri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya maisha yazidi kuwa tete tz,waandishi wahofia ya tunisia na misri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by M TZ 1, Feb 13, 2011.

 1. M

  M TZ 1 Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Bajeti ya Serikali yapigWa panGA Sunday, 13 February 2011 09:21
  NI KWA AJILI YA KUFIDIA NAKSI YA BILIONI 640
  Mwandishi Wetu
  HALI mbaya ya uchumi imeilazimisha Serikali kufumua bajeti yake ya mwaka wa fedha 2010/11 kwa kupunguza matumizi ya Wizara ili kufidia upungufu wa Sh670.4 bilioni zilizotegemewa kupatikana kutokana na makusanyo ya kodi katika mwaka huu wa fedha.
  Uamuzi huu ambao umetokana na kupungua mapato ya ndani ya mwaka huu wa fedha, umesababisha Serikali kupiga panga fedha za miradi ya maendeleo na za matumizi ya wizara zote.
  Taarifa za kuaminika ambazo Mwananchi Jumapili imezipata, zinaeleza kuwa fedha hizo zinapunguzwa kutoka katika kila wizara kwa viwango tofauti kulingana na bajeti ya wizara husika, ili kufidia makusanyo ya kodi yaliyokusudiwa na kulipia mahitaji ya fedha za mishahara na kuwalipa makandarasi wa Barabara.
  Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustaffa Mkullo, alipoulizwa kuihusina na hali hiyo alisema taarifa ya hali ya uchumi wa nchi alishaitoa hivi karibuni kwenye chombo kimoja nchini, hivyo hahitaji kuitoa tena.
  "Nilitoa taarifa kwa wenzenu wa gazeti (sio Mwananchi) sasa siwezi tena kuirudia," alisema.
  Habari hii inakuja wakati Serikali imeelezwa kuwa imetuma barua kwa nchi wafadhili kuziomba ziweze kuchangia miradi ya maendeleo katika bajeti yake.
  Kwa mujibu wa taarifa hizo, Wizara ya Fedha na Uchumi (Hazina), imekuwa ikifanya vikao mbalimbali vya kujadili tathmini ya hali ya uchumi na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti tangu Desemba mwaka jana.
  Katika vikao hivyo vilivyofanyika Januari11 hadi 24 mwaka huu ilibainika kuwa kuwepo kwa upungufu wa mapato kwa mwaka huu wa fedha unafikia Sh670.4 bilioni.
  Kutokana na hali hiyo, Serikali imelazimika kupunguza fedha za matumizi kwa wizara zake, kiasi cha Sh480.51 bilioni ili kufidia upungufu huo.
  Vile vile, itapunguza fedha za matumizi, kiasi cha Sh153 bilioni ili kuziba pengo la gharama za mishahara.
  Taarifa zaidi zinasema kuwa, Serikali inahitaji kiasi cha Sh258 bilioni kulipa madai ya wakandarasi wa barabara na mkandarasi aliyekarabati Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, huku fedha hizo zikielezwa kuwa mikataba yake ilifanyika nje ya bajeti ya mwaka 2010/11.
  Kwa mujibu wa chanzochetu cha habari, katika mkutano wa makatibu wakuu wa wizara, uliofanyika hivi karibuni kuliibuka mjadala juu ya kwanini malipo ya kandarasi ya barabara yaonekane kuwa ni ya dharura wakati kuna wizara ambazo pia zinadaiwa na wakandarasi.
  Mvutano mwingine ulihusu kiwango cha fedha za matumizi ya wizara zilizopendekezwa kupunguzwa, kuwa ni kikubwa na kuwa hali hiyo itazifanya wizara kushindwa kuendesha shughuli zake kwa kipindi kilichobaki cha mwaka wa fedha.
  “Kulitolewa mapendekezo kuwa badala ya serikali kupunguza kiwango hicho cha fedha kutoka katika kila wizara, inatakiwa iibane Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuziba mianya inayosababisha kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato,” kilisema chanzo hicho.
  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Beno Ndulu akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni mwa mwezi huu alisema hali ya uchumi wa nchi ni nzuri na kwamba Serikali ina hazina ya kutosha ya fedha.
  Hata hivyo, pamoja na mjadala huo mkali, Mwananchi Jumapili imebaini kuwa Wizara ya Fedha imesema Serikali haina budi kulipa deni hilo la kandarasi ya barabara linalofikia Sh250 bilioni ili kuendelea na kazi ya ujenzi wa barabara kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua.
  Pia wizara hiyo imesema hali ya uchumi imeathiriwa na mgao wa umeme unaoendelea, na hivyo kuathiri mwelekeo wa kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.
  Wachambuzi wa uchumi, Serikali kulazimika kupunguza bajeti yake kunatokana na kuwepo kwa matumizi mabaya na utoaji holela wa misamaha ya kodi iliyosababisha kushuka kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato.
  Habari zilizopatikana kutoka mkutano wa wahisani na watendaji wa Serikali kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2010/2011, ulifanyika hivi karibuni zinaeleza kuwa Serikali ina upungufu wa Sh600 bilioni kutoka kwenye bajeti ya Sh11 trilioni, iliyopitishwa na Bunge mwaka jana.
  Kati ya Sh11trilioni, Sh6 trilioni zilitarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani vya mapato na kiasi kilichobaki kingetokana na fedha za wafadhili.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, John Haule, hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari akiwatoa hofu wananchi kwamba Serikali haina mpango wa kuwa na bajeti ndogo kukabiliana na hali hiyo.
  Alisema Serikali inatarajia kuwa na mkutano wa kutathmini utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambao utatoa picha ya hali halisi ya uchumi wa taifa nchini.
  Comments #14 jj 2011-02-13 12:08 Najaribu kuifikiria nchi, nachukia sana! yote haya ni kwasababu ya kuwa na VIONGOZI AMBAO HAWANA AKILI WALA UBUNIFU AU KAMA SIVYO NI WENYE FIKRA FUPI ZISIZO ZA KIZALENDO. Inakuwaje kila mwaka tuwategemee wafadhili katika bajeti zetu tena kwa kiwango kikubwa kila mwaka tena kwa asilimia ileile?
  Tanzania kuna rasili mali nyingi sana na nyingi ya hizi tukiwa matajiri kuliko nchi nyingine Africa ila tupo katika nchi maskini kabisa, hii ni kwasababu ya VIONGOZI WASIOKUWA NA AKILI WALA UBUNIFU. Akili za viongozi wetu ni kwenda KUJICHEKELESHA KWA VIONGOZI wa nje na kuwa omba omba wa misaada KILA MWAKA. AIBU AIBU!! nafikiri huyu atakuwa sio kiongozi, LABDA NIMWITE KIRANJA. Kiongozi utasijikiaje moyoni kwenda kujichekelesha kwa kiongozi mwingine ili upate chochote? utajisikiaje kama baba wa familia ukatoka kwenda kuombaomba ilikuilisha familia badala ya kufanya kazi? Naamini hutajisikia tena mwanaume! hakika! IPO SIKU HAO WAFADHILI( MABWANA ZETU) WATATUPANGIA MASHARTI NAMNA YA KULALA KWENYE VITANDA VYETU! THIS IS SHAME!!! Viongozi acheni UVIVU WA KUFIKIRI!! Hata baada ya kuombomba huko, msaada tunaopewa haufikii hata kidogo thamani ya rasili mali zetu zinaibwa! HAKIKA SIKU RASILI MALI ZIKIISHA, HATUTAPATA HUO MISAADA MAANA HAKUNA WATAKACHOFAIDI! Watanzania lazima tuone mbali, lets make a change now! tuwakatae viongozi wenye matumbo makubwa zaidi ya ubongo! lets act now! wanatuua kifo cha amani!
  Quote
  +1 #13 Amina Juma 2011-02-13 11:49 kweli mwandishi nashukuru kwakutuletea taarifa ilanaomba mambomengine hata mtufiche tusijue tutapata presha wenzenu hatujamaliza la dowans, ambalo litasababisha vituvipande bei zaid ikaja umeme hakuna tunashindwa hatakufanya biashara ili tupate kipato chakutosha tuweze kukabiliana namfumuko wa bei limekuja tena na hili! jamani nchimbona inakwisha! kilasiku unayoamka afadhali ya jana!
  Quote
  0 #12 Karemu 2011-02-13 11:18 Ndugu zangu watanzania, taarifa hii ya leo ktk gazeti hili na nyingi nyinginezo, zinatuthibitish ia kwamba hali ya maisha inazidi kudidimia na kuzidi kutupa sababu na nguvu za kuendelea kuwa na sababu na nguvu za kuendelea na mpango wetu wa kufanya maandamano kwa nia ya kuiondoa serikali hii iliyoshindwa kutuletea maisha bora kama walivyotuahidi. Tunayokazi moja sasa watanzania, tunayokazi moja inayotukabili, tunayokazi moja tu mbele yetu, nayo ni kushawishi watanzania ili tufanye maandamano ya amani kabisa ya kuiondoa serikali hii.
  Quote
  #11 jj 2011-02-13 11:00 Kweli mwizi akikosa cha kuiba, atachukua hata udongo ili asiondoke bure!!!! Watanzania tulipiga kelele kuhusu DOWANS ambacho kilikuwa chanzo cha mapata ya chama na wahuni wake, sasa wameamua kutumia njia mbadala kwa kusingizia ufinyu wa budget, ukifuatilia mtiririko wa habari, utagundua kuwa baadhi ya viongozi waliokuwa wakiuongelea uchumi waliutabiria kuwa mzuri, baada ya kuona DOWANS kama chanzo cha mapato kimezibwa, sasa chama kimetafuta njia mbadala ya kujipatia kipato kwaajili ya rushwa ya uchaguzi 2015! SIKU ZINAHESABIKA, WATATAPIKA hata walizokula siku za nyuma. Mungu ibariki Tanzania!
  Quote
  #10 Erasto Rich 2011-02-13 10:59 WATANZANIA TUJILAUMU WENYEWE, SISI NDO TUMESHINDWA NA CCM KTK UCHAGUZI MKUU.
  SEMENI SASA MTAKULA NINI????? MTAKULA SMILE LA JK?
  HIVYO VIWANJA VYA NDEGE MLIVYOAHIDIWA VITAJENGEKAAAA? Uongo mtupu, kama kulipa deni la uwanja wa uhuru ukarabati imekua ishu, hizo ahadi zitakuaje?
  Quote
  #9 Eng. mwakapango, E.P 2011-02-13 10:56 Haya ni matokeo ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika uchaguzi. mimi nilikuwa napendekeza pamoja na kuwa itikadi za vyama ni tofauti wagombea ubunge, udiwani watembee pamoja na kufanya mdahalo wa pamoja tutaweza kupunguza wizi wa pesa za umma. ninao wasiwasi mkubwa kuwa serikali inaanza kufilisika.
  Quote
  #8 PMN 2011-02-13 10:51 Kujichanganya kwa viongozi wetu hawa Mkullo na Gavana ni ishara ya kukosa nidhamu ya uwajibikaji wa pamoja. Wanatuchanganya sisi wananchi. Tunakosa imani kwa serikali yetu. Tunakosa imani kwa viongozi wetu. Basi, kama hivi ndivyo, tunahitaji mabadiliko. Tupate serikali thabiti.
  Quote
  #7 elibariki yerald 2011-02-13 10:46 ni kweli kama wanavyosema wachagiaji wengine hali hii ni dunia nzima, lakini..Tanzania imezidi kwanini kila baada ya uchaguzi gharama za maisha hupanda kwa kasi sana katika nchi yetu?
  hii ni kutokana serikali wakati ule wa uchaguzi walitumia fedha za serikali katika kampeni..na magazeti mengi yalisema kama vile MWANAHALISI wakionyesha vielelezo kibao lakini watnzania wengine tuliwabeza..pia hata vyama vya upinzani kama chadema na cuf walisema hayo..je, leo na ni mkweli na nani ni muongo?
  huni uhuni matumizi yalikuwa makubwa wakati uzalishaji mdogo na uchumui uko chini sana haya ni madhara makubwa.
  kama matumizi yankuwa makubwa na akiba ina kuwa ndogo , moja kwa moja.patola taifa linapungua kwasababu fedha za kigeni zinapungua kwasababu uugizaji bidhaaa toka nje unakuwa mkunbwa ,wakati usafirishaji bidhaa kwenda nje ni mdogo..nini kinatokea?
  1.pato la taifa kupungua.
  2.viwanda vya ndani kufa kwasabau bei za bidhaa zao ni kubwa kuliko za nje
  3.ukosefu wa ajira kwasababu bidhaa zao haziuziki.
  4.maumizi ya serikali huwa makubwa kwasababu hulipa fedha nyingi nje katika kuagiza vitu kuliko kusafirishwa.
  5.gharama za maisha kuwa kubwa kwasababu ya mfumuko wa bei.
  6.uzalishaji kupungua kwasababu soko huwa hali tija kwa wazalishaji kwasababu ya gharama za uendeshaji ni kubwa..

  7.uwekezaji kushuka kabisa kwasababu uzalishaji hakuna.

  kutona na hao serikali hii imeshindwa kuwasaidia wananchi wake na kuwajali kwahiyo kengele mnapigiwa mjiuzulu au kama mkiwa wakaidi ya misri na tunisia yanakuja.NAFIKIRI MNAJUA MTU MWENYE NJAA HUWAJE..KAMA HAMJUI ENYI VIONGOZI WA TANZANIA MNAOWANYANYSA WATU,BASI NI KWAMBA MU MWENYE NJAA HAOGOPI RISASI,WLAPOLIS I WALA AMRI,YOYOTE BALI HUPIGANIA HIYO NJAA YAKE NDIPO ATAKAPOTULIA...
  NA KWA TANZANIA WATU KUWAPA SHIBE NI NYIE WALAFI WA MADARAKA KUACHIA NGAZI MAPEMA KABLA WENYE NJAA HAWAJAWAJERUHI AU KUWAUA KABISA..MSICHEZE NA MTU WENYE NJAA MAANA NAPUMULIA NUSU UHAI NUSU MAISHA.....
  Quote
  #6 Mhifadhi 2011-02-13 10:35 Tunakoelekea kila mmoja atakuwa na serikali yake mwenyewe maana zile kazi za serikali watu wanazifanya wenyewe. 1. Ulinzi - naona kila mmoja ana walinzi wake nyumbani siku hizi, 2. Afya - wapi ulisikia umeugua ukiwa chilonwa ukafwata na Ambulance utatumia gari lako ama baiskeli kama ambulance. 3. Maji, kila mmoja naona anajitahidi kuvuna maji ya mbua na kuchimba kisima chake, 4. Elimu - nadhani hili sote twaona, shule zile za umma zinavyoshindwa ktk mitihani na hivyo kulazimika kwenda shule binafsi ndani na nje ya nchi, 6. ajira, tunaambiwa tujiajiri, 7. miundombinu - tunaona tunavyokwatuliw a pesa na muda kuhudumia barabara zetu haswa sisi wa vijijini na pia twaona jinsi maeneo mengi hayafikiki. 8. ukusanyaji kodi, naona uko kwetu tuu mbona kwenye dhahabu hatuelewi kama upo, 9. umeme, kwanza haupo na tunakazana na jenereta zetu na solar, 10. maisha ya uzeeni, nafikiri twafahamu tukizeeka tutaishi maisha ya namna gani kama tusipojitengene za wenyewe mapema.
  Quote
  #5 Mhifadhi 2011-02-13 10:27 Unajua taifa kuwa makini inahitaji viongozi makini, uwazi na uwajibikaji walau kwa kuanzia. Sasa Gavana anasema hali ya uchumi ni nzuri leo tunasema ni mbaya tuelewe lipi. pili kama hali hiyo ni mbaya inakuwaje tunakimbilia deni la DOWANS?!!! haiingii akilini kirahisi. Tatu hivi sisi ni taifa la namna gani ambao tutaweka trillioni 11 ktk bajeti wakati tunashindwa kupata trillioni 6?!!!. Hesabu za kawaida zinaonyesha jinsi tunavyojiyumbis ha wenyewe? Hivi serikali ni nani?!!!!
  Maswali ni mengi sana ya kujiuliza ila ninaona kuwa hata unaposikia mapinduzi ya urusi, ufaransa, marekani, na kwingine kwingi kulianzia ktk hali kama hizi. Mapinduzi hapa nayachukulia ktk maana pana ya mabadiliko ya dhati ya maisha ya watu wake. Pia mapinduzi mengi yanayofanikiwa yalianzia mijini maana ndipo maisha yanapouma zaidi, lipa nyumba nunua kila kitu? sasa ni vyema tukaanza kufikiria tunataka mapinduzi ya aina gani kwa ajili ya watu wetu. Je tunataka kuendelea kuwategemea wafadhili? ama tunataka kuwafanya watu wetu wayaweze maisha? Sasa nafahamu kwa nini kila chama cha siasa kinang'ang'ania majimbo ya mijini. hata Cairo na Alexandria ni mjini
  Quote
  #4 mfa maji. 2011-02-13 10:24 Hali hii ni ulimwengu mzima.........
  waTanzania tusishtuke wala kuogopa hali imebadilika kila nchi inalia na hali mbaya ya kiuchumi na kupanda bei bidhaa zote za Kujikimu kijamii. "SURVIVOL" Tumeshazoea hadi miaka ya 1970s 1985 enzi ya Ujamaa wetu. au tumesahau?????
  Quote
  #3 Karemu 2011-02-13 10:22 Ndugu zangu watanzania, taarifa hii ya leo ktk gazeti hili na nyingi nyinginezo, zinatuthibitish ia kwamba hali ya maisha inazidi kudidimia na kuzidi kutupa sababu na nguvu za kuendelea kuwa na sababu na nguvu za kuendelea na mpango wetu wa kufanya maandamano kwa nia ya kuiondoa serikali hii iliyoshindwa kutuletea maisha bora kama walivyotuahidi. Tunayokazi moja sasa watanzania, tunayokazi moja inayotukabili, tunayokazi moja tu mbele yetu, nayo ni kushawishi watanzania ili tufanye maandamano ya amani kabisa ya kuiondoa serikali hii.
  Quote
  #2 mswahili safi 2011-02-13 10:19 pole pole
  Quote
  CHANZO:MWANANCHI

  Maisha kuendelea kuwa magumu

  Na Waandishi wetu
  13th February 2011

  [​IMG] Bei za bidhaa muhimu hazikamatiki
  [​IMG] Mafuta yategemea bei ya soko la dunia
  [​IMG] Thamani ya shilingi yazidi kuporomoka
  [​IMG] Bei ya sukari yazidi kupaa ingawa ni adimu [​IMG]
  Huduma za Nishati na Maji (Ewura).
  [FONT=&quot]Wakati nchi ikikabiliwa na tatizo la nishati ya umeme na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu, petroli, dizeli na mafuta ya taa, nazo zimepanda hadi kuvuka bei ya kikomo iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).[/FONT]
  [FONT=&quot]Bei hizo zimepanda ikiwa ni takribani miezi miwili tu tangu Tanesco ilipopandisha umeme kwa asilimia 18.5, ambao hata hivyo haupatikani.[/FONT]
  [FONT=&quot]Taarifa ya bei elekezi iliyotolewa na Ewura Februari 5, mwaka huu, inaeleza kwamba dizeli bora (ppm 5000 na ppm 500), ilipaswa kuuzwa kwa kati ya sh 1,770 hadi 1,902 lakini kwenye vituo vya mafuta inauzwa sh 1,931.[/FONT]
  [FONT=&quot]Uchunguzi wa NIPASHE JUMAPILI, umebaini kwamba vituo [/FONT]
  [FONT=&quot]Inatoka Uk. 1[/FONT]
  [FONT=&quot]vya BP vinauza dizeli na petroli imepanda na kuvuka bei ya kikomo iliyowekwa na Ewura.[/FONT]
  [FONT=&quot]Katika vituo kadhaa vya kampuni hiyo, mafuta ya petroli yanauzwa sh 1,919 wakati mafuta ya taa yanauzwa sh 1,531 kinyume na bei elekezi inayoonyesha bei ya kikomo kuwa ni sh 1,370.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu, alisema bei ya bidhaa hiyo muhimu itashuka kama shilingi ya Tanzania itaimarika.[/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema kuwa bei zimepanda kutokana na kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani pamoja na kupanda kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia ambapo pipa moja la mafuta machafu imepanda hadi dola za Marekani 100.[/FONT]
  [FONT=&quot]“Hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuuza mafuta juu ya bei ya kikomo tuliyoitoa sisi na kama yupo basi akigundulika tutamchukulia hatua mara moja,” alisema Masebu.[/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema mwaka 2009, bei ya mafuta ghafi ilishuka hadi dola 34 kwa pipa lakini imepanda kutokana na hali ya soko la dunia.[/FONT]
  [FONT=&quot]Aliongeza kwamba mafuta yameendelea kupanda bei kutokana na kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania na kodi mbalimbali.[/FONT]
  [FONT=&quot]Bei za petroli katika vituo vya mafuta inafukuzana na ile ya kikomo ambayo inaeleza kwamba kwa mkoa wa Dar es Salaam inapaswa kuuzwa kwa kati ya sh. 1,722 na 1852 lakini kwenye vituo vya mauzo, inauzwa kwa kati ya sh. 1,830 hadi 1,860.[/FONT]
  [FONT=&quot]Katika kituo cha Lake Oil, petroli inauzwa sh. 1,830 wakati dizeli ikiwa ni 1,730 na mafuta ya taa ni sh. 1,250.[/FONT]
  [FONT=&quot]Oilcom petroli ni sh. 1,850, dizeli 1,800 na mafuta ya taa 1,250, Bigbon petroli ni sh. 1,800, dizeli 1,750 na mafuta ya taa 1,220.[/FONT]
  [FONT=&quot]Katika kituo cha Total, petroli ni sh. 1,850, dizeli ni sh. 1,815 wakati katika kituo cha Victoria petroli ni sh. 1,850 na dizeli ni 1,800.[/FONT]
  [FONT=&quot]Baadhi ya wenye viwanda wameeleza kwamba licha ya mgawo wa umeme, wanakumbana na tatizo lingine kubwa la kupanda kila siku kwa bei ya mafuta ya dizeli na hivyo gharama za uzalishaji viwandani kupanda kila siku huku bei ya bidhaa sokoni ikibaki ilele.[/FONT]
  [FONT=&quot]“Kwa hakika, serikali ni lazima ilitafutie ufumbuzi wa haraka hili tatizo la umeme ili kuokoa uchumi wa nchi, vinginevyo hali itakuwa mbaya zaidi kiuchumi,” alisema.[/FONT]
  [FONT=&quot]Wananchi wa kawaida, wamelalamikia kuoza kwa akiba ya vyakula kwenye majokofu, biashara ndogondogo kama saluni, wauzaji wa vinywaji na kuongezeka kwa uhalifu ikiwemo vibaka kutokana na mji kuwa kizani.[/FONT]
  [FONT=&quot]Wakati nishati zikiwa juu, bei ya vyakula inazidi kupaa kwa kasi kubwa jijini Dar es Salaam, Sukari inaongoza kwa kuuzwa bei ya juu na kwenye maduka bidhaa hiyo imeanza kupotea.[/FONT]
  [FONT=&quot]Uchunguzi wa NIPASHE JUMAPILI uliofanyika katika maduka na masoko katika maeneo mbalimbali, umebaini kuwa sukari licha ya kuuzwa kwa bei ya juu, imeanza kupotea baada ya wafanyabiashara kuanza kuificha.[/FONT]
  [FONT=&quot]Uchunguzi huo ambao uliofanyika katika Wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke, imebainika bei ya mfuko mmoja wa sukari wa kilo 25 unauzwa sh 80,000 kwa bei ya jumla kutoka sh 40,000 ikiwa imepanda maradufu huku kilo moja ikiuzwa kati ya sh 1,700 hadi 2,000. Baadhi ya wafanyabiashara wamesema, kupanda kwa bei hiyo inatokana na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kuficha shehena ya sukari ili kujipatia faida kubwa.[/FONT]
  [FONT=&quot]Frank Samson mfanyabiashara wa Temeke, alisema kutokana na kununua mfuko mmoja wa sukari kwa gharama kubwa, imewabidi kuuza Sh 2,000 kwa kilo moja angalau waweze kupata faida.[/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema upatikanaji wa bidhaa hiyo imekuwa mgumu kiasi inawabidi kulipa pesa siku mbili kwa wasambazaji wakubwa kabla ya kupata bidhaa hiyo.[/FONT]
  [FONT=&quot]“Sukari kwa sasa imeanza kupotea inatubidi tuwapelekee kwanza pesa wasambazaji na kisha baada ya siku mbili tunakwenda kuchukua mzigo, hii ni tofauti na huko nyuma kwani walikuwa wakitulitea kwenye maduka yetu,” alisema Samson.[/FONT]
  [FONT=&quot]Akizungumzia hali hiyo, Ofisa mmoja wa Bodi ya Sukari nchini ambaye hakutaka kutaja jina lake liandikwe gazetini kwa sababu yeye sio msemaji, alisema kwamba kuwepo kwa uhaba wa sukari kuna uwezekano wa viwanda nchini kuzalisha chini ya uwezo kutokana na ukosefu wa umeme.[/FONT]
  [FONT=&quot]“Kuna mambo mengi yanayosababisha bidhaa kama sukari kupungua, moja ni hili tatizo la mgawo wa umeme ambapo viwanda vinajikuta vikizalisha chini ya uwezo,” alisema.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo, katika masoko ya Tandika, Kariakoo na Tandale inaonyesha bei ya vyakula imepanda kwa kasi katika wiki sita zilizopita.[/FONT]
  [FONT=&quot]Imebainika kwamba gunia moja la mchele linanunuliwa kati ya sh. 100,000 hadi 120,000 kutoka sh 80,000 hapo awali.[/FONT]
  [FONT=&quot]Unga umepanda kutoka sh. 13, 000 kwa mfuko wa kilo 25 hadi sh. 15,000, mafuta ya kupikia ya lita 20, sasa ndoo moja inanunuliwa Sh 50,000 kutoka 30,000 mwishoni mwa mwaka jana.[/FONT]
  [FONT=&quot]Unga wa ngano umepanda kutoka 20,000 hadi kufikia Shilingi 25,000 kwa mfuko wenye ujazo wa kilo 25.[/FONT]
  [FONT=&quot]Pamoja na hayo, bei ya vyakula kama maharage, kunde na choroko zimeonekana kuwa katika hali ya kawaida kwa miezi kadhaa kwenye masoko hayo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mwenyekiti wa Soko la Tandale, Sultan Kuyambo, amesema pamoja na kupanda kwa bei ya baadhi ya bidhaa katika soko lake, bado upatikanaji wa chakula umekuwa mzuri katika kipindi hiki cha kiangazi na kuwataka wananchi kutokuwa na hofu ya kupungua kwa chakula.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mhadhiri mwandamizi katika chuo cha Mtakatifu Augustine, Profesa Mwesiga Baregu, alisema kama taifa hatujaweka mikakati mahususi katika kukabiliana na matatizo hayo ikiwemo sera.[/FONT]
  [FONT=&quot]"Tumekuwa tukiangalia nishati kwa njia ya zimamoto, hatuna mikakati madhubuti ikiwemo kutumia jua kama chanzo kimojawapo cha umeme," alisema Profesa Baregu. [/FONT]
  [FONT=&quot]Imeandikwa na Zuhura Masudi, Mary Geofrey na Moshi Lusonzo.[/FONT]
  CHANZO;NIPASHE

  Ni kweli Tanzania haina cha kujifunza Misri?
  [​IMG]
  Salehe Mohamed

  [​IMG] JUZI aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak, aliamua kuachia urais baada ya baadhi ya wananchi kufanya maandamano kwa takriban wiki mbili wakimshinikiza kiongozi huyo aachie madaraka.
  Wamisri waliamua kufanya hivyo baada ya kuona maisha yao yakizidi kuwa magumu huku ya viongozi wao pamoja na marafiki wa Mubarak wakineemeka kila kukicha.
  Nguvu ya umma ndiyo iliyomfanya Mubarak ambaye amekaa madarakani kwa miaka 30 kukiachia kiti chake ingawa awali aliwadharau wananchi waliokuwa wakiandamana.
  Baadhi ya watu hapa nchi wameshaanza kusema kuwa Tanzania haina cha kujifunza kutoka Msri, kisa eti ina demokrasia na inabadilisha viongozi kila baada ya miaka mitano.
  Ni unafiki kusema Tanzania haina cha kujifunza kutoka Misri, vipo vitu vingi vya kujifunza kutoka Misri.
  Mosi, Jeshi la nchi hiyo kwa muda wote halikuwa limetumia maji ya kuwashasha, risasi, virungu kuwatanya waandamanaji waliokuwa wakitimiza haki yao.
  Walijua kuwa suluhu kamwe haiwezi kupatikana kwa mabomu, virungu na risasi kama ilivyotokea Arusha, Dodoma na kwingineko hapa nchini.
  Jeshi la Tanzania limekuwa mstari wa mbele kutembeza virungu kwa waandamanaji wanaodai haki zao kwa njia za amani iwe wanafunzi, wanasiasa, walimu na wengineo.
  Hapo kuna funzo kuwa nguvu ya umma kamwe haiwezi kuzimwa kwa risasi, mabomu, virungu kama wanavyofanya askari wa Tanzania.
  Askari kuwa vibaraka wa chama tawala ni kujidhalilisha, kuminya demokrasia na haki za wananchi ambazo zinataka mtu awe huru kutoa maoni yake bila kubughudhiwa.
  Funzo la pili, tunalolipata ni kuwa viongozi kama wataendelea kutafuna rasilimali za wananchi huku wahusika wakitopea kwenye dimbwi la umaskini, nchi haiwezi kukalika.
  Viongozi wa Tanzania wanaishi maisha kama vile wapo peponi, pengo kati ya walionacho na wasionacho linazidi kuwa kubwa na kama hatua madhubuti hazitachukuliwa, ipo siku rais atakayekuwapo madarakani atafukuzwa na nguvu ya umma.
  Inawezekana watu wakajidanganya kuwa Wamisri walichoshwa na muda mrefu aliokaa madarakani rais wao, lakini ukweli ni kuwa walichoshwa na hali ngumu ya maisha.
  Leo hii hapa nchini kilo moja ya sukari ni sh 2,000, mchele 1,500, dizeli 1,800, petroli 2,000, umeme umeongezeka bei lakini haupatikani (mgawo).
  Kuna wananchi ambao hawana uhakika wa mlo mmoja kwa siku, lakini viongozi wao kila kukicha ni kulipana posho kwenye warsha, semina, mikutano na safari zisizo na tija kwa walalahoi.
  Nilimsikia Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, January Makamba, akisema kuwa wajumbe wa kamati hiyo iliyopita walikuwa wakilipwa sh milioni moja wanapokwenda kutembelea Bwawa la Mtera, Kihansi na mengineyo.
  Kimsingi ni kuwa kuna matumizi mengi yasiyo na maana yanayofanywa na viongozi wetu, ambao baada ya kuwachagua wamejisahau na kujiona ni mungu watu na kibaya zaidi hufikiria kujinufaisha zaidi.
  Katika mazingira kama haya, kwa nini wananchi waendelee kuwa wapole na wavumilivu kwa viongozi wao ambao kila kukicha wamekuwa vinara wa kubadilisha magari na kuwapeleka watoto wao nje ya nchi kusoma?
  Matokeo ya shule za sekondari yaliyotolewa hivi karibuni yalionyesha kuwa shule za walalahoi ndizo wanafunzi wake waliofeli zaidi, kisa hazina walimu, madawati, vifaa vya kufundshia na kusomea.
  Viongozi wamekuwa wakigawana rasilimali za taifa kwa masilahi yao tena kwa kisingizio cha uwekezaji wa hovyo kabisa, mfano hai ni kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.
  Leo hii taifa limo gizani na bado tunadaiwa kiasi cha sh bilioni 94 kutoka kampuni ya Dowans, je, viongozi wetu wataweza kuhimili nguvu ya umma ikiamua mabadiliko?
  Uongozi umekuwa biashara, mtu asiyenazo hawezi kuupata, labda kama utasaidiwa na wenye nazo ambao pia watakufanya uwe mtumwa wao.
  Tanzania ya sasa, chama tawala kimekuwa msimamizi mkuu wa ufisadi na utafunaji wa rasilimali za umma huku kikiwaziba midomo wale wote waoonekana kuwa mstari wa mbele kutetea masilahi ya umma.
  CCM sasa inatumia nguvu kubwa kukabiliana na wapinzani, tena kwa mbinu chafu badala ya kujikita katika kuwaletea maendeleo wananchi.
  Wanafunzi wa vyuo vikuuu wakiandamana kudai mikopo wanapigwa mabomu, risasi na kumwagiwa maji ya kuwasha, badala ya kusikilizwa na kutafutiwa njia za kutatua tatizo husika.
  Katika mazingira ambayo hakuna barabara nzuri, maji, huduma za afya, elimu wananchi watawezaje kuvumilia wachache waendelee kutafuna rasilimali za taifa?
  Funzo la tatu tunalopata ni kuwa ubabe kamwe hauwezi kuzima nguvu ya umma kama alivyofikiri Mubarak.
  Tanzania ya leo haina haki, ya mtu binafsi au taasisi, kinachoangaliwa ni uwezo wa kimadaraka wa mtu au jamaa aliye karibu naye.
  Taasisi za serikali zimekuwa nyonyaji kwa wananchi ambao kimsingi ndio wenye kuwalipa mishahara na kugharimia shughuli nyingine za serikali
  Chaguzi mbalimbali zimefanyika lakini wanaoziongoza waliamua kupindisha matokeo ili kuwanufaisha wengine na cha kukera zaidi vyombo vya dola vilikuwa mstari wa mbele kutoa vitisho.
  Wananchi hawawezi kuvumilia milele uonevu wa aina hii, ipo siku watafanya kama Misri na kama viongozi wakiwatumia askari, basi kuna kila dalili damu ya watu wengi zaidi itamwagika.
  Funzo la nne ni kuwa Tanzania imevamia mifumo ya uchumi huria kwa kutumia uhalifu wakati mifumo hii inataka mfumo madhubuti wa kisheria wenye serikali makini inayofanya kazi kama mwamuzi, na ndiyo maana tuna rushwa, umaskini, kukata tamaa na watu kuoneana vijicho kwa sababu ya kupigwa mabao mchana kweupe.
  Chuki pia imejengeka na ndiyo maana wengine wanakwambia kwamba machungu yao yanatokana na dini yao na si utawala mbovu.
  Viongozi wetu wanajilimbikizia mali ikiwemo magari, fedha, nyumba ardhi na vinginevyo, huku wanyonge wakilalamika kupokwa viti hivyo.
  Vigogo hao ndio wenye kuchota mabilioni kupitia mikataba ya ununuzi wa ndege ya rais, rada ya jeshi na helikopta zake, mikataba ya madini na vingine vingi.
  Kibaya zaidi, wameamua kurithishana madaraka ili waendelee kutafuna rasilimali za taifa mpaka kiama, mwananchi wa kawaida atavumilia vipi haya?
  Leo hii chama tawala kimekuwa cha kifamilia, yaani mtoto, baba na mama wote wana sauti kwa watendaji wa serikali bila kujali miiko ya uongozi au kutofautisha majukumu ya kifamilia na majukumu ya kitaifa.
  Katika mazingira haya ya askari kutumia nguvu kulinda masilahi ya chama tawala, tunaweza kufika salama huko tuendako? Tusidanganyane, tuna mengi ya kujifunza kutoka Misri.
  Watawala ambao hawataki kujifunza kutoka Misri, bila shaka wanatakiwa kuondolewa madarakani kwa mawe, matusi na kelele za wananchi!
  Nawasihi viongozi wetu waamini, watumie rasilimali zilizopo kwa masilahi ya wananchi, la sivyo kiama cha Misri, Tunisia na hivi sasa Algeria kitakuja muda si mrefu.
  CHANZO:TANZANIA DAIMA

  [​IMG]
   
 2. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mi nashangaa watz tunavyojifananisha na Tunisia na Misri. Kul watu walikuwa na Umoja hapa kutokana na maslahi watu wamegawanyika sana. Pia majeshi yalikuwa contained hasa Misri huku Bongo polisi wataua watu wote
   
 3. regam

  regam JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi wajameni mnadhani haya yoooote yanayoandikwa katima mathreads hapa hawajui? Wanayajua fika! Mie naona kama tunajipotezea muda tuuu. Siku moja nilikuwa nafanya presentation ya namna ya kuinia sekata ya kilimo. Walikuwepo makatibu wa wizara pamoja na wawakilishi kutoka ikulu. Cha ajabu baada ya kumaliza waliniambia kwamba wanajua hayo mapendekezo toka zamani. Walinipatia na baadhi ya vitini vinavyoonyesha namna mbalimbali ya kuendeleza hiyo sekta.
  My take:
  Walioko huko juu wakiwemo policy makers and facilitators tolikuwa nao mtaani, wanafahamu kila kitu ila wakipata nafasi hizo sijua wanarogwa?
   
 4. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2016
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,112
  Likes Received: 1,742
  Trophy Points: 280
  Aiseee
   
 5. Gut

  Gut JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2016
  Joined: Jan 18, 2016
  Messages: 2,668
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Naona mnafukua makaburi.
   
 6. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2016
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,894
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280
  Baada ya yote Mungu atasimama nakuitetea serikali ya Mh Magufuli. Take from me Kama mnafikiri atashindwa imekula kwenu.
   
Loading...