Hali ya kibiashara hairidhishi, biashara zaendelea kufungwa!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
16,108
25,982
Nina nukuu gazeti la Mwananchi tar 24 Jan 2017.

Hali ya biashara nyingi kudorora si suala la kuuliza tena, ni dhahiri. Hali ya kibiashara nchini si tu imedorora lakini hata ajira kutoka biashara hizo inaendelea kuwa mbaya.

Cha kushangaza ni Serikali kutokuwa na majibu ya kujitosheleza kwanini hali hii. Waziri Dr Mpango alinukuliwa kuwa kufungwa kwa biashara hizo , ati hata yeye hajui kwa nini.

That's too much!

Nafikiri serikali sasa ina watendaji wanaoishi mawinguni, hawasikii kilio cha wadau wake. Kufungwa kwa biashara ina maana hata kodi haiwezi kukusanywa, hivyo serikali kukosa mapato yake.

Lakini litazame suala lenyewe kwa jicho la tatu.
We are in a visciuos circle!!!

Kodi zinaua uchumi kwa sasa hivi, hili ni dhahiri. Tumeona wimbi la makampuni ya uchimbaji madini yakisema ati yanafunga uchimbaji kwa sababu madini ati yamepungua!

Sidhani kuwa hili ni kweli, wanafunga kwa sababu ya kodi kubwa. Mimi nasema si kwamba wasilipe, hapana walipe satahiki.

Kwa biashara ndogo ndogo wasioweza kuhimili msukosuko wa kodi, swala ni moja tu-kufunga biashara, kodi hazilipiki!

Kwa wale wenye uelewa wa kodi za TRA na sharia zake ziko kama ifuatavyo:
  • Kuna kodi yenyewe
  • Ikicheleweshwa, kuna fine inayotozwa juu yake
  • Baada ya fine, kuna riba ya deni lenyewe
Kwa uzoefu ukibebeshwa hayo mambo matatu kwa mpigo, huna jinsi, unafungasha virago kibiashara!! Hiyo ndo viscious circle tuliyoiingia

Zijue sababu za kufungwa biashara 2,000

pic+kufungwa+biashara.jpg

Picha ya Mtandao

Kwa ufupi
  • Wadau hao wamependekeza kuimarishwa kwa mazingira ya biashara na kuboreshwa kwa uhusiano kati ya wafanyabishara na Serikali.
  • Awali, taarifa ya utekelezaji wa bajeti kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ilibainisha kuwa kati ya Agosti na Oktoba, 2016 kulikuwa na wimbi la kufungwa biashara, ingawa alisema wizara haikupata sababu za wafanyabiashara kuzifunga.

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi
ebahemu@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Hali ya kufungwa kwa biashara 2,000 katika miji ya Dar es Salaam na Arusha imewaamsha wadau wa uchumi, ambao wameeleza kiini cha kuporomoka huko.

Wadau hao wamependekeza kuimarishwa kwa mazingira ya biashara na kuboreshwa kwa uhusiano kati ya wafanyabishara na serikali."

Waziri Dr Mpango alinukuliwa kutoelewa kwa nini biashara zinafungwa
 
Huwezi kuendelea kufanya biashara kihalali katika awamu ya 5 wakati ulizoea kufanya magumashi huko nyuma! Asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa Kariakoo mlichokuwa mnafanya haikuwa Siri. Matokeo yake ndio haya yanayoendelea sasa. Tulipe Kodi tujenge Taifa kwa manufaa ya Watanzania wote.
 
Ulipe kodi ujenge Taifa, while kuna mfumuko wa bei? Watu msio na uelewa wa mambo mnajazwa sana upepo na cheap politics unapoambiwa hali ya uchumi kama Taifa ni mbaya fanya analysis ndipo upate nguvu ya kuchangia humu.
Jiulize doller thamani yake dhidi ya shilling ipoje
Unga bei yake sh ngapi
Mchele je
Njoo na exportation na importation charges zafikia sh ngapi? Country minerals production zinakuwa kwa kiasi gani? Nchi na kuvutia wawekezaji wa nje na ndani sera zao zipoje? Migogoro na wafanyabiashara wakubwa haishi tu rejea Dangote, Njoo na Manji saga.

Jf inabidi wenye zero minded kama wewe mpewe ban...Hatujawahi kuwa na member hawafikirii kwa kina namna hii.
 
Huwezi kuendelea kufanya biashara kihalali katika awamu ya 5 wakati ulizoea kufanya magumashi huko nyuma! Asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa Kariakoo mlichokuwa mnafanya haikuwa Siri. Matokeo yake ndio haya yanayoendelea sasa. Tulipe Kodi tujenge Taifa kwa manufaa ya Watanzania wote.
Umeshawahi kufanya biashara?
 
We kaa utulie mambo yatajipa tu, ukisoma kemia kuna kila kitu ndani yake; uchumi, sheria, biashara, diplomasia, nk. Sasa kiranja mkuu anayo PhD ya kemia kila kitu anajua hahitaji ushauri tumpe muda tu.
 
Huwezi kuendelea kufanya biashara kihalali katika awamu ya 5 wakati ulizoea kufanya magumashi huko nyuma! Asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa Kariakoo mlichokuwa mnafanya haikuwa Siri. Matokeo yake ndio haya yanayoendelea sasa. Tulipe Kodi tujenge Taifa kwa manufaa ya Watanzania wote.
Mkuu inaelekea wala hujui biashara nchi zinaendaje kiuhalisia.
Afya kiuchumi kwa serikali ni kodi hilo halipingiki.
Lakininkodi inapokuwa mzigo udiobebrka , mzigo huo unsutua usije kukuua bure.
Mpaka hapo hata mtoto mdogo ataelewa.
Siyo siri kodi karibia 80% ya serikali inatoka mkoa wa DSM.
Na kodi hiyo inatokana na hao hao wanaofunga biashara sasa hivi kutokana na mzigo mkubwa wa kodi.
Haihitaji PhD kulielewa hili, lakini sioni jinsi mapato ya serikali kutokana na kodi kuongezeka.

Nafikiri unapata sasa upeo wa tatizo ambalo wewe na Dr Mpango hamulielewi.
 
Mkuu inaelekea wala hujui biashara nchi zinaendaje kiuhalisia.
Afya kiuchumi kwa serikali ni kodi hilo halipingiki.
Lakininkodi inapokuwa mzigo udiobebrka , mzigo huo unsutua usije kukuua bure.
Mpaka hapo hata mtoto mdogo ataelewa.
Siyo siri kadi karibia 80% ya serikali inatoka mkoa wa DSM.
Na kodi hiyo inatokana na hao hso wanaofunga biashara sasa hivinkutokana na mzigo mkubwa wa kodi.
Haihitaji PhD kulielewa hili, lakini sioninjinsi mapato ya serikalinkutokana na kodi kuongezeka.

Nafikiti unapata sasa upeo wa tatizo ambslo wewe na Dr Mpango hamulielewi.
Wewe unayejua masuala ya kibiashara naomba unieleweshe mkuu. Mnapingana na uchafu wa Kariakoo kila kukicha ilhali ukweli mnaujua. Mbona asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa kiAsia wameweza ku adjust na kuendelea na biashara hizo hizo!? Mnataka kulaumu serikali kwa kila Jambo.
 
Huwezi kuendelea kufanya biashara kihalali katika awamu ya 5 wakati ulizoea kufanya magumashi huko nyuma! Asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa Kariakoo mlichokuwa mnafanya haikuwa Siri. Matokeo yake ndio haya yanayoendelea sasa. Tulipe Kodi tujenge Taifa kwa manufaa ya Watanzania wote.
Hivi wewe unajua kujenga nchi ni kujenga magorofa na barabara za lami. Kujenga nchi ni kuimarisha maisha ya mwananchi, sasa kama unamkandamiza mwananchi alafu unasema unajenga nchi, sijui iyo ni principle gani ya uchumi.
 
Wala Rushwa mmeshikwa pabaya sana awamu hii. Jina lako linajieleza.
 
Wewe unayejua masuala ya kibiashara naomba unieleweshe mkuu. Mnapingana na uchafu wa Kariakoo kila kukicha ilhali ukweli mnaujua. Mbona asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa kiAsia wameweza ku adjust na kuendelea na biashara hizo hizo!? Mnataka kulaumu serikali kwa kila Jambo.
Mkuu naona uko mbali sana katika kuelewa hali ya kibiashara nchini.
Jiridhishe na ukweli kwamba wafanyabiashara wa ki asia wana mitaji mikubwa zaidi kibiashara, na wamo kwenye biashara kwa muda mrefu zaidi.
Kodi inakokotolewa kutokana na mahesabu ya kibiashara.
Siyo siri vile vile kwamba makampuni ya ki asia siyo walipaji wakubwa wa kodi kulingana na ukubwa wa biashara zao.
Sababu ni nini?
Sababu ni kuweka vizuri sana a paralle set of company business books.
Hili wengi wanalifahamu sana hata TRA wanalijua hilo.
 
Nina maneno mawili tu kwako mkuu ..."Business Acumen".Tafakari bila mihemko utanielewa.
 
Kama asilimia kubwa za mapato ya serikali ni kodi kutoka kwenye biashara na hizo biashara ndio zinafungwa kiuchumi nchi inaelekea wapi? Wasomi wa uchumi tuelezeni.
 
T

Tukiongelea cooked books of accounts I dont think you will have the capacity to differentiate from the two, the hallmark of many asian businesses.
Unajuaje Kama sina capacity ya kutofautisha!? Usikariri wala usipime mkuu. Nakujibu kutokana na level yako..ukitaka twende kina kirefu tunaenda. Maana wengi humu wamezoea kejeli na matusi,ndio maana huwa naandika kwa level yao ya uelewa ili kuwapunguzia machungu ya kutafakari Punch lines beyond its initial scope.
 
Back
Top Bottom