KERO Hali ya Barabara ya Kibaha Mailimoja Mitaa ya Kwa Mang’umbi inasikitisha

KERO Hali ya Barabara ya Kibaha Mailimoja Mitaa ya Kwa Mang’umbi inasikitisha

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Hali ya barabara Kibaha Mailimoja, Mitaa ya Kwa Mang’umbi hadi Tankini, leo Desemba 28, 2025, ni ya kusikitisha, mara nyingi mvua inaponyesha inakuwa haipitiki kirahisi na hivyo kusababisha kero kubwa kwa usafiri wa kila aina wakiwemo watembea kwa miguu.

Wananchi tunajiuliza, viongozi wapo wapi? Barabara hii ni muhimu kwa maisha ya kila siku, lakini changamoto inazidi kuongezeka, kila mwaka Viongozi wa Kibaha na Pwani kwa jumla wanatuahidi kuwa itaboreshwa na wakati mwingine kupitisha greda kuikwangua, baada ya hapo hakuna kinachoendelea, shida ilirudi wanaanza kufanya yaleyale ya kuikwangua na ahadi nyingi.

Soma: Kairuki: Nitahakikisha barabara za jimbo la Kibaha kujengwa kwa lami
IMG_3482.jpeg

1766918693641.png


1766918731570.png


1766918762314.png

IMG_3483.jpeg

1766918852357.png


1766918928407.png
 
Kibamba hali kadhalika ni mateso tu Mvua zikipiga unaweza jikuta kibaruani hufiki kwa wakati, na hata mnapo kuwa na mgonjwa ni mtihani sana. Unaiona Hospital Mloganzile ile pale lakini kuifikia ni mtihani.
 
Amani muhimu kuliko barabara washenzi nyie acheni taharuki..!!
 
Back
Top Bottom