Hali ya barabara kwa wakazi wa Mwanagati inasikitisha

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,820
4,573
Habari Wakuu,

Yaani inapotokea mvua katika jiji la Dar es Salaam ni kama adhabu kwa wakazi wa Mwanagati kuanzia kipande cha Kwa Mparange mpaka kituo Cha mwisho cha daladala Cha Mwanagati. Barabarani mbovu na haipitiki kwa urahisi.

Daladala zinalazimika kupandisha nauli, na Hata baadhi ya wamiliki magari wanalazimika kupaki magari yao, kuyaepusha kuharibika kwa hali ya barabara hii.

Safari ya nusu saa unalazimika kutumia saa zima kwa sababu magari yanatembea kwa kunyata.

Mbunge na viongozi wote tunaomba muangalie tatizo hili! Ukizingatia sasa Mbunge wa huku ni Waziri wa Ardhi tumatumaini barabara hii itafanyiwa kazi maana tuliambiwa bajeti tayari imetengwa. Mbunge Jerry Silaa tunaomba isiwe story kama za Vijiweni.

Hizi hapa chini ni baadhi ya picha ya hali ilivyo.







Pia soma: Baada ya kelele za Wananchi, barabara ya Mwanagati yaanza kutengenezwa
 
Mko kijijini dar es salaam mpaka mseme hapo bado sana
 
Barabara ya mbande msongola ndo haifai kabisa yaani mpaka unajiuliza kama hii nchi Ina wawakilishi
 
Ila Mwanagati wamejenga wenye hela inakuwaje mnapiga kelele hivyo?
 
bado mpaka tuseme hatujasema bado. Hujapita ya kivule kwenda Msongola ni aibu. Huyu mbunge wallahi hatorudi uchaguzi ujao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…