Hali tete kwenye burudani

ZE NDINDINDI

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,892
2,000
Yaani ni balaa jamani ,wenyewe mnaliona,kumbi zimefulia,bendi zimefulia,hata wachache wanaoingia vinywaji vya kusikilizia mpaka inzi wanaingia kwenye glass.

Ila leo sikutarajia nilichokiona,nimekaa na mshkaji wangu mara sms ikaingia kwenye simu yake,kaombwa 80,000 na msanii mwenye jina kubwa tu bongo,alimrushia 50,000 msanii akapiga simu kushukuru ikabidi amuulize kulikoni tena?

Jibu ni kwamba hata kwenye bongo fleva show zimekata,zamani kila wiki unasikia makampuni ya simu yakizindua kampeni kama za jaza ujazwe lazima yafanye shows za wazi kama vile mbagala au coco beach na hata kuchukua wasanii na kuzunguka nao mikoani,sasa ni kwishney.

Anyway wachumi naomba mtusaidie inawezekana hizi ni indications za kukua kwa uchumi.
 

sayoo

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
3,227
2,000
Hizo ni dalili za kusomeka kwa namba mkuu, bado kidogo tuanze kusoma za kirumi sasa
 

mpenda arage

JF-Expert Member
Nov 10, 2015
1,380
2,000
vimada wangu zamani nilikua nawajali sana lakini siku hizi hata wakini deep, sipigi. huu upepo sio. ha ha ha ha ha
Hatariiii!! Tafadhali Nipigie, Salio lako halitoshi. Hizo ndio Meseji ambazo kwenye simu yako hazikosi!! huu upepo sio wabaidi, huu upepo n wa motooo! N wa moto kabisa!
 

Allency

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
4,930
2,000
Tajiri anatakiwa aishi kama shetani, sasa mnashangaa nini uchumi kuwa hivi?
 

chikundi

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
8,245
2,000
Kuna siku nilishuhudia bend kubwa ya dansi ikitumbuiza kiingilio bia..ni balaa.
Bendi zilikufa miaka mingi kabla hata ya utawala huu. Kwa mfano akudo impact imekufa japo jina lipo mapacha watatu imekufa chokoraa karudi twanga japo jina lipo FM akademia iliathirika zaidi baada ya mmiliki wake martin kasyanju kufariki japo bado ipo. Msondo ngoma miaka zaidi ya mitano inafanya show ya bia pale brake point ya mjini kule posta kiujumla muziki wa dansi umekufa au umeanza kufa miaka mingi nyuma lkn club bado zinafanya vizuri japo show za bingo fleva zimepungua kidogo kutokana na spirit ya kubana matumizi ya magufuli kuingia mpk kwenye mashirika binafsi. Spirit hii ndiyo itakayoleta maendeleo kwa serikali hadi mtu mmoja mmoja nchi zilizoendelea spirit ya kubana matumizi ipo karne nyingi tukumbuke ukienda kwa mzungu hukaribishwi msosi kama hukutoa taarifa n.k hii ina maanisha wazungu wako makini na matumizi lkn sio masikini. Watanzania sasa tuishi kwa budget na kufanya kazi zaidi tutaendelea na tutamkumbuka magufuli.
 

NONIYANG'WAKA

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
1,235
2,000
natamani mambo yazidi kudoda kabisa, ghalama ya msosi ipae maradufu, mvua msimu ujao ianze mwezi januari ili tuheshimiane 2020
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom