Hali si shwari Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali si shwari Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MBANINO, Jun 6, 2011.

 1. M

  MBANINO Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hali inazidi kuwa ngumu kwa Menejimenti ya Juu ya Ofisi hii ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kufutia mgawanyiko mkubwa ambao umetokea.

  Hali hii imejitokeza baada ya wakaguzi wa kanda wapatao 11 kutoa waraka wenye kuonyesha malalamiko mbalimbali na kuuelekeza kwa CAG Bw. Utouh kwa ajili ya kupata majibu yake.

  • Miongoni mwa malalamiko hayo ni kwa wao kutokutendewa haki stahiki kutokana na nafasi zao ambazo wangeweza kupatiwa ikiwa ni pamoja na kupatiwa malipo ya pango la nyumba na fenicha za ndani pindi tu unapoteuliwa.
  • Kingine kinacholalamikiwa ni upandishwaji wa vyeo unaofanyika kiholela bila ya kuangalia sifa za msingi za wahusika wakuu. Mfano mkubwa ikiwa ni wale waliopandishwa vyeo na kuwa Principal Auditors ambao hata utendaji wao wa kazi ni questionable. Wamejaribu kuonyesha ya kwamba karibu wote waliopandishwa cheo hicho hawana rekodi yoyote ile ya kazi zaidi ya kukaa ofisini kwa muda fulani ambao unawaruhusu kupanda vyeo hivyo. Ila hawana kitu chochote kile walichokifanya kwa ofisi zaidi ya kuwatumia wengine katika kutimiza malengo yao.
  • Suala lingine lililalamikiwa na Wakaguzi hawa wa kanda ni la ukabila uliokithiri. Hili ni donda ambalo linaitafuna ofisi hii vibaya sana. Ukabila umekuwa kigezo cha msingi kabisa katika kupanda cheo na pia kupata post ambazo ni nzuri na za msingi. Uongozi wa juu umekumbatia ukabila kwa kiwango kinachotisha kabisa na hivyo kusababisha wafanyakazi wengi kupoteza ari ya kazi. Tatizo hili kwa uwazi kabisa linaweza kueleza ni kwa nini vyeo vilivyopandishwa vinalalamikiwa sana.
  • Uchafu uliokithiri katika jengo la Makao Makuu. Hili ni tatizo kubwa sana. Vyoo ni vichafu, vingi vimefungwa na hakuna anayejali, sababu kubwa ya kufungwa kwa vyoo hivi ni kushindwa kuvikarabati huku ikijulikana wazi ya kwamba bajeti ya ukarabati ilitengwa (fedha hizo zimeenda wapi?; kampuni ya usafi na yenyewe inafanya kazi gani?). Imekuwa ni jambo la hatari kwa afya ya walio wengi kutumia vyoo hivi lakini kikubwa zaidi tusisahahau hawa ni watu wanao kagua wengine.
  • Safari zisizo na tija za Mkurugenzi wa Utawala, Mama Lyimo. Huyu, amelalamikiwa kwa kushindwa kutulia ofisini na kutekeleza wajibu wake wa msingi na kuishia kusafiri maeneo tofautitofauti pasipo kujali ni nini kinatakiwa kifanyike nyumbani. Kama utaratibu wa ku-limit safari za watendaji serikalini unafanyika iweje mtu mmoja atumie zaidi ya nusu nzima ya mwaka kufanya safari nje ya nchi na miezi mingine kufanya safari ndani ya nchi na kuwa ofisini? Anafanya kazi saa ngapi na ni kweli maslahi ya watumishi anayajali?
  • Manunuzi ya ajabu na yenye kutia mashaka makubwa yanafanyika huku yakiwa na baraka ya wakubwa. Jamani wale ndugu zetu wanaokagua mambo ya manunuzi Ofisi hii hamjaimulika?
  My take:
  Kila mtu anafahamu utendaji mzuri wa Bw. Utouh, lakini lazima tukubali ya kwamba madhaifu mengi yanayoainishwa na Wakaguzi wa Kanda 11 wa Ofisi ya Ukaguzi ni ya msingi na anatakiwa ayafanyie kazi.
  • Ni aibu kuwa na ukabila uliokithiri katika zama hizi, ni aibu kubebana katika zama hizi, ni aibu kujishughulisha na mambo yanayoshusha hadhi ya Ofisi. Ni kwa nini usiwatumie kikamilifu watendaji wako wazuri na wenye juhudi katika kazi na kuishia kubebana?
  • Ni kwa nini usiiangalie ofisi kwa miaka 10 ijayo na kuishia kuibomoa tu? Ni kwa nini idara zingine za serikali zisiingilie kati na kufanya uchunguzi wa kina na kisha kuisafisha ofisi hii inayoonekana kuaminiwa na wananchi huku mambo yakiwa yanaenda kombo?
  • Ni sehemu gani (idara au kitengo) ndani ya ofisi hii ya Taifa ya Ukaguzi inaendeshwa kwa ufasaha pasi na ubabaishaji? Ni nini kitatupa imani ya kwamba Ofisi inasonga mbele wakati ni wazi kabisa hakuna kinachotendeka kwa haki?
  Bw. Utouh, linda heshima yako (ndani ya Ofisi) inayozidi kuporomoka kwa kutazama haya yanayofanyika nyumbani kwako. Watu wanayaona, asilimia kubwa ya uongozi wa ofisi ni watendaji dhaifu wasio na uwezo. Tuache kulindana tuanze mwanzo mpya na huu utawezekanika kwa kusafisha tu uongozi wa juu kabisa wa ofisi hii.
   
 2. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  nina imani tutafika tunapokwenda....waache wale weee mwishowe watavimbiwa watatuachia nchi yetu
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Daah hatari ! Kama hali ni hiyo ? Si mchezo.
   
 4. M

  MBANINO Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Itnoject: Ni kweli tutafika, ila kumbuka tutafika tukiwa na maumivu makali sana. Hawa ni watu na watumishi wa umma tuliowaamini na kuwapa dhamana ya kukagua matumizi ya mali za umma na leo hii wao ndio wanafanya mambo yakutisha kiasi hiki ni wapi tunakwenda?

  Nguvumali: Hiyo ndio hali, yamkini Tanzania tunahitaji mabadiliko makubwa katika kila nyanja, hali ni mbaya sana.
   
Loading...