Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,382
- 38,652
Leo na jana nimefanya utafiti kwenye Stendi kuu ya Iringa na kugundua kwamba Kampuni za usafirishaji abiria toka Iringa kwenda Dar es salaam na Dodoma ama zimepunguza safari za kwenda huko ama zimesitisha kabisa safari hizo.
Kampuni kama Sanya One wao wamesitisha kwa muda safari zao za kwenda Dar es salaam kwa kukosa abiria wa kutosha, wakati kampuni zingine kama Osaka wao wameshusha kiwango cha fedha kampuni inazochukua kwa kila abiria na kuongeza posho kwa wapiga debe wanaotafuta abiria.
Wapiga debe nilioongea nao wamesema inawezekana hali mbaya ya uchumi inalazimisha watu kutosafiri bila ya kuwa na sababu za msingi ama hata kupunguza idadi ya wanaosafiri toka kwenye familia moja!