Mvua kubwa zinazoendelea jijini mida ya saa moja asubuhi
Ayusema mimi nikiwa naelekea kibaruani viatu mkononi maji yamejaa mpaka kufunika barabara.
Ghafla nasikia honi ya gari ikipigwa kwa fujo, niligeuka kwa hasira nikitaka kuachia mvua ya matusi, kioo cha gari aina ya Verosa kilishushwa na mrembo ndani yake akasema "Pole kaka panda nikuvushe mpaka barabarani" Nikamjibu "Ahsante dada sitailowesha gari yako?"
Akajibu 'Usijali".. pepesa pesa za kiwizi kumcheck ni bonge la mrembo.
Nikatulia zangu taratibu nikifuta maji niweze vaa viatu vyangu.
Kaka waitwa nani na wafanya kazi wapi? Nikamjibu naitwa Ayusema ni IT Technician company moja ipo maeneo ya msasani ndo nakoelekea....
Akaniangalia halafu akatabasamu kisha akasema yeye anaitwa Vivian ni Accountant company moja ya mafuta hapa mjini..
Huku kwetu umefuata nini? nilimuuliza huku nkimshangaa, akasema alimleta shangazi yake mtaa wa pili na aliponikuta ila yeye anaishi Masaki karibu na Howard Humprey company kama naijua na ndo anakoelekea...
Nikamjibu nshawahi kwenda kufanya installation ya network system katika company hiyo napajua vizuri sana..
Huku nikiwaza kimoyo moyo leo nimepona kugombea gari na mvua hii..
Akasema "Nyie watu wa IT mna vipaji kweli.. nina IPAD inagoma kuconnect internet chukua kadi yangu then ukiwa na muda nitafute unirekebishie"
Nikamjibu "hata hivo naenda kibaruani ku handover duties then narudi home, naanza leave leo ya week moja..
Akatabasam then "itakuwa njema ukinitafuta asubuhi hii mie nipo off leo" Nikamwambia nashuka hapo mbele kabla hujafika Ubalozi wa Marekani...
Nikimaliza ntakucheck... Poa poa hope to see ya later... Ok byee
Baada ya saa moja nilimvutia waya kilichotokea huko kwake..................
Itaendelea