Hali hii ni mpaka lini katika Elimu yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali hii ni mpaka lini katika Elimu yetu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by gfsonwin, Apr 19, 2012.

 1. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,982
  Likes Received: 1,893
  Trophy Points: 280
  Asalam Aleykum wana jf. Naomba leo niingie humu jamvini kwa namna ya tofauti kabisa kuijadili hali hii ya elim hapa kwetu Tanzania.

  Kwanza nianze kwakusema kuwa mimi binafsi ni mwajriwa serikalini katika sekta hii ya elimu, na nimekuwa hapa kwa muda wa miaka mingi. Binafsi mimi nilikuwa napenda sana kazi ya ualimu wakati ninasoma na nilibahatika kwa miaka ile kuwa mwanafunzi wa kike aliyekuja UDSM akitokea advance level kuja kusomea fani ya ualimu wa science(Bsc. Ed) ambaye nilisoma masomo ya fizikia na kemia. Kwakweli kwa wakati ule ilikuwa ni ngumu sana kuona binti anasoma masomo haya kwani yaliaminika ni magumu. Kwakua mimi nilipenda tu ualimu sikuliangalia hilo sana mimi nilichoangalia ni ile heshima ambayo wakati ule tulikuwa tunawapa waalim. Fikra hizi ziliniaminisha kuwa kusalimiwa na wanafunzi,kuaminiwa na kusikilizwa na wanafunzi ni heshima kubwa sana. Zaidi ya yote kumfundisha mtu halafu anakuja kuwa mtu wa kutegemewa kwa taifa, au kukutana na mwanafunzi wako labda ni bosi katika ofisi fulani na wewe umekwenda pale kutaka huduma basi akikusaidia ni heshima ya ajabu na ilikuwa ni fahari kwamba mwanafunzi niliyemfundisha hakuniangusha. Imani hizi ambazo hadi leo mimi napenda kuziamini basi zilifanya niipende kazi yangu ya ualimu kwa kiwango cha hali ya juu.

  Ingawa sikuwahi kusoma diploma ya ualimu, nilianzia shahada lakini pia malezi bora tuliyopewa na waadhiri wa chuo( mara nyingi hawa wa elimu hupenda kuitwa waalimu) ilitufanya kwa kiasi kikubwa kuwa na maaadli na nidham ya kazi pamoja na elimu juu ya tunachotaka kufundisha. Mambo haya kwa ujumla wake yalitufanya tuwe na ujasiri wa kazi kwa kiasi kikubwa sana.Na kwakweli tuliogopeka sana kazini kwani wengi wa waalimu walikuwa wana elimu ngazi ya diploma hivyo kwa mwenye degree basi hasa kwa masomo ya sayansi tulikuwa wachache sana. Kwa bahati mbaya sana wengi baada ya kuajiriwa kama waalim hawakufanya kazi muda mrefu wakapewa shule wawe wakuu wa shule na wengine wakapewa nafasi za kiuongozi katika wizara ya elimu.

  Kwa bahati nzuri mimi sikuondoka mapema kwenye fani hii ya ualim nilifundisha kwa muda wa miaka sita kama mwalimu wa chemistry advance na hapo nilishangaa sana ile shauku ya kuendelea kuwa mwalimu iliondoka kabisa.Nilijikuta nayachukia mazingira ya ualimu kwa kiwango kikubwa sana, lakini kwasababu sikuwa na kazi nyingine mkononi basi ilinilazimu kuomba wizara inirudishe kwenda kusoma tena. Nilipomaliza sikurudi shuleni tena.

  mwana Jf nimeeleza hayo kwa ufupi ili uje upate picha kamili ya hali ya elimu ambayo hadi leo hairekebishiki. sababu zilizonifanya niondoke kwenye fani ya elimu wala sitaona haya kuzisema ni:-

  kipato kidogo. Mshahara wa mwalim ngazi ya degree ulikuwa ni TGSD D. Kima hiki kilikuwa kama sh 160000/= na ambapo kikikatwa basi unajikuta unapokea kiasi kama 90000/= au zaid kidogo. Mshahara huu ulikuwa mdogo sana ukilinganisha na mtu wa elimu kama hii aliyekuwa anafanya kazi katika taasisi nyingine serikalini. Kwakele nyingi sana raisi Kikwete aliunda tume ya kurekebisah mishahara na ndipo mishahara ngazi hii ikapanda hadi sh 270000/=miaka ya 2006 kama sikosei. Lakini ingawa umepanda mshara huu hauna maslahi kwa mwalimu hata kidogo. Leo mshahara wa ngazi ya TGSD D ni kama sh 470000/= tu katika mazingira haya ya leo mshahara huu ni kama hakuna kitu.

  Ni ukweli kuwa mishahaa ya watumish wa umma serikalin ni midogo wala haitofautiani sana na hapa na naipongeza serikali kwa kuliona hili na kulirekebisha tofauti na kipindi cha nyuma. Lakini pia maisha ya mwalimu bado yanazidi kuwa magumu. Mtumisha mwingine ataenda hata semina, atapewa overtime, ili kumpa motisha kazini lakini siyo mwalimu. Matokeo yake mwalim anaish kwa kutegemea mshahara maisha yake yote. Tena imefikia mahali hata zinapokuwepo semina za capacity building mwalim halipwi inavyotakiwa mwalimu huyu utakuta anaambiwa shule haina hela hivyo ataambulia kupewa sh 10000/= kama nauli ya kuja kwenye semina. Hiyo pia haitosh kali ni hii ya waali kwenda kusimamia mitihani, kiukweli anatakiwa apewe per dm yake cha kushangaza utakuta analipwa sh 1000 kwa script moja atakayosahihisha. kwahiyo kama akisahihisha 100 atapata sh 100000/= kwa kazi ambayo amekaa chini na kuumia mgongo na kuwa mbali na familia yake.

  mamlaka ya TSD, sina ubaya kabisa na chombo hiki ambacho kazi yake ni kuratibu ajira za waalimu. Kinachonishangaza ni kwamba keo hii ninyi TSD mkiulizwa hivi mwalim mwenye masters degree anatakiwa alipwe sh ngapi mtasema? jamani huu ni ukweli nawaambia katika scheme of salaries mwalim wa ngazi ya masters hatambuliki tena ukienda wana kuuliza sasa hebu tuangalie kati ya ngazi hii hadi nagazi hii. sasa mimi huwa najiuliza zaid ya waalimu wa vyuo vikuu na ambao ninyi hamna mamlaka nao, hawa wengine wapo hadi we phd lakin hamuwez kuwalipa kweli hii ni sahihi? je hivi mwalimu hapaswi kufurahia matunda ya elimu yake?
  cha ajabu kwa hawa TSD ni hiki hapa leo hii mwalim akienda kujisoendelez mathalan alikuwa anapokea mshahara ngazi TGS F lakini alikuwa na diploma basi akirudi na degree yake ataambiwa aanzie kama fresh graduate au kama new employee hivyo anarudishwa nyuma hadi TGS D. SASA mimi najiuliza hii ni secular gani na kwanini haiangalii maslahi ya mwalimu kama mwalimu. katika sekta ambazo huwa zinanishangaza ni hii ya elimu, unaweza kukuta mtu anacheo kikubwa sana lakini mshahara wake unashangaza sana. kwanini lakini? au ni kwamba waalim wanatakiwa wawe wa diploma tu katika hili taifa? Yawezekana kweli secular hii ilitengenezwa wakati waalim wengi wakiwa na kiwango hiki cha elimu lakin je kwanini sasa msiibadilishe ili kuendana na hali halisi ya nchi?

  Sehemu nyingine inayotia kichefuchefu ni CWT mimi natamani hata leo chama hiki kifutwe. Hakina maslah kwa mwalim hata kidogo. wamekuwa kwao wanang'ang'ania madai ya walimu tu pesa wanazodai wanaacha na mambo mengine ya msingi kabisa. Sijui wanaridhika na hali hii. jamani kila mwezi mwalim anakatwa hela kwa ajili ya cwt na ni chama ambacho leo hii ukikifanya kiwe cha siasa basi kitakuwa na wafuasi wengi sana lakini ni chama ambacho hakina nguvu kabisa na hakijui majuku yake.Sijui wanaridhika na mass failure ya wanafunzi, hawajawahi hata siku moja kutetea mazingira magumu walimu wanayofanyia kazi, shuleni chaki hakuna, madarasa mabovu, ela za ruzuku hakuna shule kila mara zinaish kwa mwendo wa kuwa madeni tu.Inafikia wakati hata mwalim kufikiria mbinu mbadala za kufundishia unashndwa manake ukifikiri hivyo basi utoe hela yako mfukoni ili kufanikisha. vinginevyo ubaki na staili ya kuimba uboni basi. Hayo masomo ya vitendo ndio usiseme mwanafunzi anafanya mara 2 tu tena hapa ni kwa shule inayojitahdi sana vinginevyo wanajifunza kinadharia na siku ya mtihani wanafanya kwa vitendo. CWT wamekaa kimya kabisa tena kama hao viongozi wa juu ndio kabisa wao wanasubiri tu kupokea hela hali wakiacha hali ikiendelea kuwa tete. maslahi ya waalim hawayatetei wamebaki kuwa wanasiasa kuliko kuwa watetezi wa waalim.

  Ningekuwa na uwezo ningeigawa CWT primary iwe na ya kwao na sekondar iwe na ya kwao. Hii ni kwasababu walimu wengi wa msingi ndio viongozi huku na hawa wengi ni wake wa makatibu wakuu, wakurugenzi, mawaziri na watendaji wakuu serikalini ambao kila mnachokipanga wao wanakwenda kuwaambia waume zao kisha kesho yake mnajikuta mnagonga mwamba. MOD naomba usinipe BAN acha niseme haya ili jamani tujue nini tunachokifanya na wapi tunakwenda.Waalim weng wa sekondari wanaonekana kuwa hatari kwa CWT kwan ndio vijana na wamesoma zaidi sasa ili kujihami hawatakiwi kabisa kushika nafasi za juu za uongozi huko CWT. na ikitokea unagombea jua lazima ushindwe kama ni mwalimu wa sekondari. Sasa kuna faid gani ya kuwa na nayo kama haiwez kutetea? SIkutaga kuamin kuwa CWT ilianzishwa na nguvu ya CCM nilijiaminisha kuwa ni nguvu ya waalim wenyewe na kwamba kiko huru kumbe walionielekeza mwanzo kuwa ni nguvu ya CCM walikuwa sahihi. Manake haiwezekani kwa chama kama hiki kishindwe hata kutoa tamko linaloeleweka.

  watanzania wenzangu majuzi hapa tulishuhudia mgomo wa madaktari na ulituumiza sana lakini mimi nilisema bora ili serikali ijifunze, na ningekuwa mimi ni kiongozi wa CWT ningetoa tamko kuhusiana na hali ile kwani mwalimu huyu anakesha darasani kumfundisha mwanafunzi ambaye yeye kwa wakati huo akiugua akienda hosp hana wa kumtibu. sasa hapa lazima pangepatikana suluhu tu na ukweli nasema ningeitisha mgomo ambao kwa umoja wetu tungeishinikiza serikali ingelegeza uzi. ingepiga mnada ashangingi yake ili kuinusuru nchi. Kinyume chake mwalimu mnyonge wa watu alikuwa anakwenda shule ilihali anajua akiugua hana pa kukimbilia na CWT ipo. Chama ambacho hakiwezi kuhoji pale hela zinapofujwa na serikali na kuacha wanachama wake wakiwa maskini? hizo areazi unazosikia waalim amedai wengine miaka sita na wengine wanapandishwa cheo, lakini hawapokei mishahara ya vyeo wanavyovitumikia. na cwt iko kimya kweli jamani.
   
Loading...