Halahala CCM na Nchemba wenu!

Halahala CCM na Nchemba wenu!

Hivi aliishia wapi aliposema tumwombee ana siri nzito juu ya chadema............????

Kwani anaona shida gani kujiombea mwenyewe? Bila shaka amegundua Biblia inasema maombi ya asiye haki ni chukizo kwa Mungu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Magamba wanaona lakini hawaamini, ngoja wananchi wa Liwale wasambae nchi nzima.Mbunge anaacha kueleza matatizo ya maji huko mtera anamtusi Dr.Slaa lol!
 
mwigulu tena....
ni kweli anafikiria maendeleo au ubishi na lugha mbovumbovu ??!!.
 
BIBLIA ndio kitabu kitakatifu tuu kwenu? CHADEMA utawajua tu!

Kwani ukimuuliza Mwingulu Nchemba atakuambia sio BIBLIA kwake??? DON'T PICK and CHOOSE RELIGIOUS BOOKS TRUTH MATTERS!!!!

Hapa ni Mahali pa SIASA; DINI ni IMANI BINAFSI!!!
 
Kuna methali isemayo: “Mchimba kisima huingia mwenyewe.” Maana yake mtu anayemchimbia mwenziye shimo kwa dhamira mbaya huishia kuingia mwenyewe.

Methali hii hutumiwa kumshauri mtu anayekusudia kumfanyia ubaya mwenzake kuwa huenda ubaya huo ukamrudia yeye. Kama jinsi kuku aliyechinjwa anavyotapatapa kabla ya kufa, ndivyo kilivyo sasa CCM. Kinatumia kila njia kujiokoa. Ndio maana Bunge latumika kuwashambulia wapinzani, hususan Chadema, kana kwamba si wawakilishi halali wa wananchi!

Katika kikao cha 10 cha Bunge lililopita, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba aliifananisha bajeti kivuli iliyoandaliwa na upinzani kama takataka akiwauliza wapinzani walisomea wapi uchumi. Kama hiyo haikutosha, akaitupa chini nakala ya bajeti ya Kambi ya Upinzani aliyokuwa nayo mkononi!

Wabunge wa CCM walitumia wingi wao kushangilia kwa vifijo, vicheko, kubeza na kugonga meza. Si Spika wala Mnadhimu Mkuu wa Serikali Bungeni, William Lukuvi aliyekemea kitendo hicho.

Ingekuwaje kama hotuba ya bajeti ya serikali ingetupwa chini na mbunge wa upinzani?

Bunge si ukumbi wa mipasho, kejeli, kuzomeana wala kulala. Wabunge wanapaswa kuwakilisha kero za wananchi ili zishughulikiwe na serikali. Si mahala pa kutetea sera za vyama zisizokuwa na tija kwa wananchi, wala serikali inapokosea.

Hiyo si maana ya uwakilishi. Wabunge wakumbuke ahadi walizotoa walipokuwa wakiomba kura; baadhi yao wakipiga magoti majukwaani na kuamkia ‘shikamoo’ hata kwa vijana wadogo!

Kikao cha 11 cha Bunge la Bajeti ya mwaka 2013/2014 yamezuka mauzauza mengine, kinara akiwa yuleyule Mwigulu Nchemba. Songombingo hilo lilianza baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kuwasilisha maoni ya kambi yake akisema:

“Umeibuka uchochezi mpya wa kisiasa wenye ubia kati ya chama tawala na vyombo vya dola na kinachoitwa ugaidi. Kambi yangu inashangazwa na uhodari wa serikali kuchukua hatua kwa suala la mtu aliyebambikiwa kesi ya ugaidi kwa ushahidi wa kughushi kuwa yeye ndiye gaidi.”

Akasema kambi yao inasikitika kuona waliokuwa wakiwasiliana na hao wanaoitwa magaidi ambao pia ni viongozi wa CCM na washirika wao hawajachukuliwa hatua yoyote. “Tunaulaani mkakati

huu wenye nia ovu ya kufifisha demokrasia hapa nchini. Mpango huu haramu hautafanikiwa.”

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara) na ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alichachamaa na kusema kwa hisia kali: “Watu wanapanga ugaidi halafu wanaachwa tu, nashukuru Mbowe hayuko hapa nadhani atakuwa amekamatwa (na Polisi) pamoja na Katibu wake kwa kuwa wao ndio wamekuwa wakiwasiliana na aliyekuwa amepanga ugaidi.”

Wakati Nchemba akitoa shutuma zake dhidi ya Chadema, Mbowe alikuwa jijini Dar es Salaam katika maandalizi ya mkutano wa mafunzo na mipango ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) na Kongamano la Katiba Mpya kwa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani. Ni tofauti kabisa na kauli ya Nchemba kuwa anadhani ‘Mbowe atakuwa kakamatwa … ’.

Nchemba akadai yu tayari kutoa ushahidi Bungeni, Polisi na hata Mbinguni! Hakuwa akiishawishi Polisi imkamate Mbowe? Kuhusu kutoa ushahidi Mbinguni, ni lini Mwenyezi Mungu alimwita mwanadamu yeyote kwenda kutoa ushahidi? Nani anamdanganya Mwigulu kuwa Mbinguni kuna mahakama inayohitaji mashahidi wa duniani kwenda kuthibitisha mashitaka? Tusubiri, labda wa kwanza atakuwa Mwigulu Nchemba!

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akitumia Mithali 27:22 katika Biblia Takatifu: “Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano , upumbavu wake hautamtoka,” alisema serikali ina tatizo kwa kuwa kuna akili ndogo inayotawala vichwa vikubwa.

Kauli hiyo ilimnyanyua Mnadhimu Mkuu wa Serikali Bungeni, William Lukuvi na kusema Msigwa na mwenzie Wenje (wote Chadema) walikiuka kanuni za Bunge kutokana na matamshi yao. Pia aliungwa mkono na Naibu Spika, Ndugai akiwasihi wabunge kuacha kutumia lugha chafu. Wenje alisema serikali iliyo madarakani haina uwezo wala ujuzi na imepoteza imani ya watu kwa kushindwa kuwatatulia matatizo yao.

Huko nyuma, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) akionesha ushahidi wa CD mbili alizokuwa nazo mkononi, alisema katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) udini umejikita kiasi kwamba wanafunzi wa dini tofauti hawawezi kulala chumba kimoja na kuhadharisha kuwa jambo hilo linahatarisha kuigawa jumuiya ya Chuo hicho.

Kauli hiyo ilimnyanyua Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM) Juma Nkamia na kusema “kama tatizo ni dini za wakuu wa UDOM, Maprofesa Idrissa Kikula na Shaban Mlacha, huo ni uchochezi” na kuongeza kuwa “hizo kanda zinazosemwa kuhusu udini ni za uchochoroni, tuachane nazo.” Kanda zinazochochea udini nchini ziachwe kwa madai kuwa ni za ‘vichochoroni?’ Hajui kuwa mwanzo wa mvua ni mawingu?

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Chadema) aliingilia kati na kuuliza: “na (kanda) za Lwakatare je?” Akajibiwa na Juma Nkamia: “Siongei na m-mbwa bali nazungumza na mwenye m-mbwa!” Tafsiri yake Mbilinyi ni m-mbwa na mwenye m-mbwa ni viongozi wa Chadema!

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM) akiichambua hotuba ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni aliwarushia vijembe viongozi wakuu wa Chadema kwamba kuna wabunge wenye mimba zisizotarajiwa Bungeni! “Kuna watu wanataka kuvuruga nchi wakati wana watoto wachanga.

Mimi mtoto wangu wa mwisho ana miaka minane halafu Dk. Slaa wa kwake sijui ana wiki ngapi. Hawa wapinzani tuachieni mimi na Nchemba Mwigulu.”

Dk. Slaa, Katibu Mkuu wa Chadema aliingizwaje kwenye malumbano ya Bungeni wakati si Mbunge na wala hakuwapo hata kwenye jukwaa la wageni waalikwa kama si chuki binafsi dhidi yake? Huyu ndiye Livingstone Lusinde, ambaye hata kwenye kampeni za ubunge kule Arumeru Mashariki mwaka jana alitumia lugha za matusi na mwishowe mgombea wao (CCM) akaanguka mweleka wa mende.

Kauli ya Lusinde kuwa “Hawa wapinzani tuachieni mimi na Mwigulu” ndivyo walivyoahidi walipokuwa wakiomba kura majimboni mwao? Au wanatumwa na chama chao (CCM) kuwashughulikia wapinzani badala ya kuwasilisha kero za wananchi? Huu ndio uwakilishi wa wananchi Bungeni? Ukimya wa CCM kwa wabunge wake unamaanisha nini?

Mwalimu Nyerere alipata kusema: “Wenye mawazo tofauti na serikali, hata wawe wachache kiasi gani, lazima wapewe haki ya kutoa mawazo yao katika kujadili hoja bila hofu ya kusumbuliwa. Mawazo yao yashindwe tu kwa hoja na si kwa vitisho na nguvu.”

Nampongeza Spika Anne Makinda alipowaambia Wabunge: “Badala ya kujadili hotuba mnajadili matusi. Mmevaa suti vizuri kabisa lakini mnatoa matusi midomoni mwenu. Mtu ukivaa rasmi namna hii halafu unatoa matusi yasiyofanana na wewe inakuwa aibu kabisa. Mtu yeyote akitukana namwita askari, anachukuliwa humu ndani anakwenda n-nje.”

Biblia Takatifu yasema: “Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafula, wala hapati dawa. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua.

Tena: “Hakika binadamu ni ubatili, na wenye cheo ni uongo; katika mizani huinuka; wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili. Msiitumainie dhuluma, wala msijivune kwa unyang’anyi; mali izidipo msiiangalie sana moyoni. Mara moja amenena Mungu, mara mbili nimeyasikia haya: ya kuwa nguvu zina Mungu, na fadhili ziko kwako, Ee Bwana; maana ndiwe umlipaye kila mtu sawasawa na haki yake.

Viongozi wa CCM na serikali wakisoma mistari hii kwa tafakuri bila kujali dini zao, wala kuendeleza chuki, dharau na udini unaoendelea kusitawi nchini, huenda watazinduka.

Mungu Ibariki Tanzania, Dumisha Uhuru na Umoja, Wake Kwa Waume na Watoto, Mungu Ibariki, Tanzania, Na Watu wake.”
Hii ni tafakuri makini sana ambayo mwandishi ameiandika kwa uhodari mkubwa.

Naamini kwa wanaCCM makini na wasio wanafiki, wataufanyia kazi waraka huu, lakini kwa wale tunaoweza kuwaita sikio la kufa, kama kawaida yao, najua wataupuuzia!!
 
Yaani hakuna mtu ninayemdharau humu duniani kama nchemba.
"Eti anasema watanzania naomba mniombee nina jambo zito nataka lisema" huyu jamaa ni punguani. Siku hz vi id vyake vya shelui, utaifakwanza na shumbi madelu havitumii tena.
 
Yaani hakuna mtu ninayemdharau humu duniani kama nchemba.
"Eti anasema watanzania naomba mniombee nina jambo zito nataka lisema" huyu jamaa ni punguani. Siku hz vi id vyake vya shelui, utaifakwanza na shumbi madelu havitumii tena.

Baada ya watu kushtukia ID zake ameacha kwanza. Sasa anatengeneza nyingine mpya. Mtaziona tu. Yeye na CCM yake ni janga la kitaifa.
 
Sasa Lusinde na Mwigulu kuachiwa Chama (CCM) ni janga. Ni sawa na Akili ndogo kuongoza akili kubwa. Hii ni ya kwanza kuishuhudia ktk enzi hizi za siasa Tz. Let us see.
 
hofu yangu mimi si Mwigulu, Hofu yangu mimi sio Lusinde wala ccm wala chadema. Hofu yangu mimi ni kwa hawa wanao amini udini kuliko kitu kingine. kuna watu hum jf uwezo wao wakufikiri ni mdogo sana kila jambo wao ni udini tu.
 
ccm inawafanya watanzania kuwa wenda wazimu
 
Back
Top Bottom