Halahala CCM na Nchemba wenu!

Halahala CCM na Nchemba wenu!

Django

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
354
Reaction score
147
Kuna methali isemayo: “Mchimba kisima huingia mwenyewe.” Maana yake mtu anayemchimbia mwenziye shimo kwa dhamira mbaya huishia kuingia mwenyewe.

Methali hii hutumiwa kumshauri mtu anayekusudia kumfanyia ubaya mwenzake kuwa huenda ubaya huo ukamrudia yeye. Kama jinsi kuku aliyechinjwa anavyotapatapa kabla ya kufa, ndivyo kilivyo sasa CCM. Kinatumia kila njia kujiokoa. Ndio maana Bunge latumika kuwashambulia wapinzani, hususan Chadema, kana kwamba si wawakilishi halali wa wananchi!

Katika kikao cha 10 cha Bunge lililopita, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba aliifananisha bajeti kivuli iliyoandaliwa na upinzani kama takataka akiwauliza wapinzani walisomea wapi uchumi. Kama hiyo haikutosha, akaitupa chini nakala ya bajeti ya Kambi ya Upinzani aliyokuwa nayo mkononi!

Wabunge wa CCM walitumia wingi wao kushangilia kwa vifijo, vicheko, kubeza na kugonga meza. Si Spika wala Mnadhimu Mkuu wa Serikali Bungeni, William Lukuvi aliyekemea kitendo hicho.

Ingekuwaje kama hotuba ya bajeti ya serikali ingetupwa chini na mbunge wa upinzani?

Bunge si ukumbi wa mipasho, kejeli, kuzomeana wala kulala. Wabunge wanapaswa kuwakilisha kero za wananchi ili zishughulikiwe na serikali. Si mahala pa kutetea sera za vyama zisizokuwa na tija kwa wananchi, wala serikali inapokosea.

Hiyo si maana ya uwakilishi. Wabunge wakumbuke ahadi walizotoa walipokuwa wakiomba kura; baadhi yao wakipiga magoti majukwaani na kuamkia ‘shikamoo’ hata kwa vijana wadogo!

Kikao cha 11 cha Bunge la Bajeti ya mwaka 2013/2014 yamezuka mauzauza mengine, kinara akiwa yuleyule Mwigulu Nchemba. Songombingo hilo lilianza baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kuwasilisha maoni ya kambi yake akisema:

“Umeibuka uchochezi mpya wa kisiasa wenye ubia kati ya chama tawala na vyombo vya dola na kinachoitwa ugaidi. Kambi yangu inashangazwa na uhodari wa serikali kuchukua hatua kwa suala la mtu aliyebambikiwa kesi ya ugaidi kwa ushahidi wa kughushi kuwa yeye ndiye gaidi.”

Akasema kambi yao inasikitika kuona waliokuwa wakiwasiliana na hao wanaoitwa magaidi ambao pia ni viongozi wa CCM na washirika wao hawajachukuliwa hatua yoyote. “Tunaulaani mkakati

huu wenye nia ovu ya kufifisha demokrasia hapa nchini. Mpango huu haramu hautafanikiwa.”

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara) na ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alichachamaa na kusema kwa hisia kali: “Watu wanapanga ugaidi halafu wanaachwa tu, nashukuru Mbowe hayuko hapa nadhani atakuwa amekamatwa (na Polisi) pamoja na Katibu wake kwa kuwa wao ndio wamekuwa wakiwasiliana na aliyekuwa amepanga ugaidi.”

Wakati Nchemba akitoa shutuma zake dhidi ya Chadema, Mbowe alikuwa jijini Dar es Salaam katika maandalizi ya mkutano wa mafunzo na mipango ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) na Kongamano la Katiba Mpya kwa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani. Ni tofauti kabisa na kauli ya Nchemba kuwa anadhani ‘Mbowe atakuwa kakamatwa … ’.

Nchemba akadai yu tayari kutoa ushahidi Bungeni, Polisi na hata Mbinguni! Hakuwa akiishawishi Polisi imkamate Mbowe? Kuhusu kutoa ushahidi Mbinguni, ni lini Mwenyezi Mungu alimwita mwanadamu yeyote kwenda kutoa ushahidi? Nani anamdanganya Mwigulu kuwa Mbinguni kuna mahakama inayohitaji mashahidi wa duniani kwenda kuthibitisha mashitaka? Tusubiri, labda wa kwanza atakuwa Mwigulu Nchemba!

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akitumia Mithali 27:22 katika Biblia Takatifu: “Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano , upumbavu wake hautamtoka,” alisema serikali ina tatizo kwa kuwa kuna akili ndogo inayotawala vichwa vikubwa.

Kauli hiyo ilimnyanyua Mnadhimu Mkuu wa Serikali Bungeni, William Lukuvi na kusema Msigwa na mwenzie Wenje (wote Chadema) walikiuka kanuni za Bunge kutokana na matamshi yao. Pia aliungwa mkono na Naibu Spika, Ndugai akiwasihi wabunge kuacha kutumia lugha chafu. Wenje alisema serikali iliyo madarakani haina uwezo wala ujuzi na imepoteza imani ya watu kwa kushindwa kuwatatulia matatizo yao.

Huko nyuma, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) akionesha ushahidi wa CD mbili alizokuwa nazo mkononi, alisema katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) udini umejikita kiasi kwamba wanafunzi wa dini tofauti hawawezi kulala chumba kimoja na kuhadharisha kuwa jambo hilo linahatarisha kuigawa jumuiya ya Chuo hicho.

Kauli hiyo ilimnyanyua Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM) Juma Nkamia na kusema “kama tatizo ni dini za wakuu wa UDOM, Maprofesa Idrissa Kikula na Shaban Mlacha, huo ni uchochezi” na kuongeza kuwa “hizo kanda zinazosemwa kuhusu udini ni za uchochoroni, tuachane nazo.” Kanda zinazochochea udini nchini ziachwe kwa madai kuwa ni za ‘vichochoroni?’ Hajui kuwa mwanzo wa mvua ni mawingu?

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Chadema) aliingilia kati na kuuliza: “na (kanda) za Lwakatare je?” Akajibiwa na Juma Nkamia: “Siongei na m-mbwa bali nazungumza na mwenye m-mbwa!” Tafsiri yake Mbilinyi ni m-mbwa na mwenye m-mbwa ni viongozi wa Chadema!

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM) akiichambua hotuba ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni aliwarushia vijembe viongozi wakuu wa Chadema kwamba kuna wabunge wenye mimba zisizotarajiwa Bungeni! “Kuna watu wanataka kuvuruga nchi wakati wana watoto wachanga.

Mimi mtoto wangu wa mwisho ana miaka minane halafu Dk. Slaa wa kwake sijui ana wiki ngapi. Hawa wapinzani tuachieni mimi na Nchemba Mwigulu.”

Dk. Slaa, Katibu Mkuu wa Chadema aliingizwaje kwenye malumbano ya Bungeni wakati si Mbunge na wala hakuwapo hata kwenye jukwaa la wageni waalikwa kama si chuki binafsi dhidi yake? Huyu ndiye Livingstone Lusinde, ambaye hata kwenye kampeni za ubunge kule Arumeru Mashariki mwaka jana alitumia lugha za matusi na mwishowe mgombea wao (CCM) akaanguka mweleka wa mende.

Kauli ya Lusinde kuwa “Hawa wapinzani tuachieni mimi na Mwigulu” ndivyo walivyoahidi walipokuwa wakiomba kura majimboni mwao? Au wanatumwa na chama chao (CCM) kuwashughulikia wapinzani badala ya kuwasilisha kero za wananchi? Huu ndio uwakilishi wa wananchi Bungeni? Ukimya wa CCM kwa wabunge wake unamaanisha nini?

Mwalimu Nyerere alipata kusema: “Wenye mawazo tofauti na serikali, hata wawe wachache kiasi gani, lazima wapewe haki ya kutoa mawazo yao katika kujadili hoja bila hofu ya kusumbuliwa. Mawazo yao yashindwe tu kwa hoja na si kwa vitisho na nguvu.”

Nampongeza Spika Anne Makinda alipowaambia Wabunge: “Badala ya kujadili hotuba mnajadili matusi. Mmevaa suti vizuri kabisa lakini mnatoa matusi midomoni mwenu. Mtu ukivaa rasmi namna hii halafu unatoa matusi yasiyofanana na wewe inakuwa aibu kabisa. Mtu yeyote akitukana namwita askari, anachukuliwa humu ndani anakwenda n-nje.”

Biblia Takatifu yasema: “Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafula, wala hapati dawa. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua.

Tena: “Hakika binadamu ni ubatili, na wenye cheo ni uongo; katika mizani huinuka; wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili. Msiitumainie dhuluma, wala msijivune kwa unyang’anyi; mali izidipo msiiangalie sana moyoni. Mara moja amenena Mungu, mara mbili nimeyasikia haya: ya kuwa nguvu zina Mungu, na fadhili ziko kwako, Ee Bwana; maana ndiwe umlipaye kila mtu sawasawa na haki yake.

Viongozi wa CCM na serikali wakisoma mistari hii kwa tafakuri bila kujali dini zao, wala kuendeleza chuki, dharau na udini unaoendelea kusitawi nchini, huenda watazinduka.

Mungu Ibariki Tanzania, Dumisha Uhuru na Umoja, Wake Kwa Waume na Watoto, Mungu Ibariki, Tanzania, Na Watu wake.”
 

Attachments

  • PICHA PAGE 3, APRILI 2013.jpg
    PICHA PAGE 3, APRILI 2013.jpg
    21.1 KB · Views: 309
Watakoma.
Kiboko yao ni 2015. Ngoja wajishebedue tu.
Wako wapi akina dialo, masha na vibaraka vingine? Nguvu ya umma itawapapasa na kuwavunjavunja na kubaki historia. Just wait 2015 is coming
 
Nimesikitika kwa sauti kubwa wao waache tu mwaka 2015 CCM ndo watakuwa chama cha upinzani sijui watakimbilia wapi... mashimo yote wanayochimba lazima wadumbukie wenyewe 2015 waache waendelee kushangilia kwa nguvu Bungeni.... kuna siku hata wakijiunga wao wenyewe wakianzisha chama hakitasajiliwa.
 
Watakoma.
Kiboko yao ni 2015. Ngoja wajishebedue tu.
Wako wapi akina dialo, masha na vibaraka vingine? Nguvu ya umma itawapapasa na kuwavunjavunja na kubaki historia. Just wait 2015 is coming

Ni kweli maana kuna msemo unasema ( WHEN SPIDER WEBS UNITE THEY CAN ENTANGLE A LION )
na sisi tunasema PEOPLE'S POWER...TOGETHER WE CAN CHANGE OUR NATION
 
Ndugu yangu [MENTION] Django [/MENTION]

Kwa kweli haya yote uliyoyasema ni umiza kichwa kwa CCM. Wanaelewa kila kitu lakini Wabunge wa CCM wapo Bungeni kwa ajili ya kulinda chama na siyo kwa ajili ya maslahi ya wananchi waliowachagua.

Ni wakati umefika kwetu wananchi kutenga Pumba na mchele.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
"Hizi ni siasa za maji taka Siziwezi" by Rostam Azizi
 
nawewe si uweke ya kitabu chako unachoona ni kitakatifu? sasa kama yeye ni mkristu unataka asome kuruani? think critically, usilazimishe mambo.
 
Hivi inavyotokea baada ya kikao bha bunge wanatangaziana wabunge wa magamba wakutane na mkutano ndo wanashauriana na kuteua vinara wa kutukana bungeni badala ya kujipanga kujibu hoja zinazowakabili na huwa wanashindwa kuzitendea haki maana badala ya kuzijibu wanaishia kutukana na kuachana na hoja iloko mezani
 
mungu atusaidie na kutuvusha salama, maana hawa ccm wanataka kutumaliza.
 
aliwazalo mjinga ndilo litakalo mtokea hofu na mashaka ya ssm juu ya cdm ni ya kuonesha jinsi gani wanawaza kuondoka madarakani mwigulu mwisho wake wa siasa utakuwa mfupi sana, siko la kufa halisikii dawa ssm wameonywa badilikeni hawtaki let them out 2015 viva chadema!.
nawewe si uweke ya kitabu chako unachoona ni kitakatifu? sasa kama yeye ni mkristu unataka asome kuruani? think critically, usilazimishe mambo.
 
Kwetu kuna msemo kuwa "ULUTEGA MUKASHO LWIJA NA NYOKO"(ukiweka mtego wa kumuua mama wa kambo,mtego huo uishia kumuu mama mzaz wako)
ccm litakalo wapata 2015 ni janga.
Spika na naibu wake ni janga la nchi
 
Hivi aliishia wapi aliposema tumwombee ana siri nzito juu ya chadema............????
 
mazishi ya ccm yalishaanza 2010 jimbo la Mbulu, 2015 ni kuhitisha tu.

DEMOKRASIA YA KWELI IKO MBULU by Mwl Nyerere
 
Inasikitisha na kuzidisha hasira dhidi ya CCM. Mungu atondolee hawa wakoloni
 
Hivi hamuwezi kujadili bila kutaja neno "CCM" humu?nimelichoka jina hili na kila nilisikiapo naumia kichwa kwa kukumbuka matatizo yote ya mtz kama umeme,maji,nauli juu,ufisadi,ardhi kuporwa,matusi bungeni,ugaidi,udini,n.k!hebu semeni tu "hawa majambazi"ili mnisaidie kichwa kisiume jamani!
 
Huu ni mpango wa mungu. Amewafanya vichwa vigumu ili yatimie, ccm mnajichimbia kaburi wenyewe, sawa na mtu anayefirika hawezi kujifaham mpaka acc zake zisome nill.
 
Back
Top Bottom