Hakuna ubaguzi kujiunga na JWTZ

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imesisitiza kwamba upimaji wa afya wa vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) hufanyika mara mbili na hakuna ubaguzi wa vijana kutoka Zanzibar.

Waziri wa Ulinzi na JKT, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema, waombaji wa kujiunga na JWTZ hupimwa afya zao ili kuhakikisha wanaweza kuhimili mafunzo ya kijeshi na kutekeleza majukumu mbalimbali ya kijeshi katika mazingira tofauti.

Dk. Mwinyi amesema, upimaji wa afya wa awali hufanyika katika vituo kunakofanyika usaili, na baada ya hapo, husafirishwa kwenda katika kituo cha kufanyia mafunzo ya kijeshi ya awali.

“Upimaji wa kina hufanyika katika kituo cha mafunzo ya kijeshi kabla ya kuanza mafunzo. Kwa kuwa upimaji huu ni wa gharama hufanyika kwa wale tu waliofaulu hatua ya awali. Wanaoonekana kuwa na matatizo ya kiafya hurejeshwa kwa gharama za jeshi hadi makwao,” amesema Waziri Mwinyi.

Waziri huyo amesema, si kweli kwamba waombaji kutoka Zanzibar pekee ndiyo hupimwa afya mara mbili bila kuhusisha na wenzao kutoka Tanzania Bara.

Alisema utaratibu wa upimaji haubagui, bali unafanyika kwa wote kufuatana na utaratibu uliotajwa.

Alisema, waombaji walioachwa baada ya kupimwa kwa mara ya pili na kuonekana na matatizo ya kiafya, walitendewa haki kwa kuwa jeshi linahitaji kuwa na wanajeshi wenye afya nzuri wanaoweza kutekeleza majukumu ya jeshi kikamilifu.

“Hii ni kwa manufaa ya jeshi na wahusika pia ikitiliwa maanani kuwa mafunzo ya kijeshi ni magumu na yanahitaji utimamu wa mwili,” alisema Dk. Mwinyi akijibu swali la Mussa Khamis Silima (Baraza la Wawakilishi).

Waziri Dk. Mwinyi alisema, utaratibu wa ajira katika Jeshi umebadilika na sasa Jeshi linaajiri vijana ambao wameshapitia mafunzo ya JKT; na vijana wanaoomba kujiunga na JKT hutakiwa kuripoti kwenye usaili wakiwa na fedha za kuwarudisha makwao endapo hawatafaulu vipimo vya afya.
 
sasa kama jeshi linaajiri vijana waliopitia JKT, sasa , vipi vijana wa Zanzibar ambao kwao hakuna JKT ? Je vipi wale waliopitia JKU kwa nini na wao wasiajiriwe ?
 
sasa kama jeshi linaajiri vijana waliopitia JKT, sasa , vipi vijana wa Zanzibar ambao kwao hakuna JKT ? Je vipi wale waliopitia JKU kwa nini na wao wasiajiriwe ?

Hao ambao hawajapita JKT hawaajiriwi kwa sababu hawajakidhi masarti (not qualified) ujue sharti muhimu ni "awe amepitia JKT"
 
Zanzibara mnataka kuvunja muungano jeshi letu mnalitakia nini cmna jeshi lenu sijui jku/kmkm
 
Back
Top Bottom