Hakuna "trade war" baina ya Kenya na Tanzania

Hakuna "trade war" baina ya Kenya na Tanzania

kunze

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2016
Posts
400
Reaction score
472
Ndugu wananchi wa Kenya na Tanzania,kwa takribani wiki mbili sasa,kumekuwepo na UPOTOSHAJI (usiojulikana malengo yake) kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu kuibuka kwa "VITA YA KIBIASHARA" kati ya Kenya na Tanzania. Taarifa hizo zinaposha kwamba,kulikuwa na ucheleweshaji wa malori 15 yaliyosheheni NGANO kuingia Kenya kupitia mpaka wa Namanga kadhalik na uingizwa wa MCHELE kupitia mpaka wa Isebania.

Ubalozi wa Kenya nchini Tanzania,unapenda kuchukua fursa hii kuifahamisha jamii ya nchi hizo mbili,vyombo vya habari,viwanda,waingizaji bidhaa,taasisi za serikali na wadau wote kwa ujumla kuwa,madai hayo kuhusu vita hiyo,ni upotoshaji mtupu,uzandiki na jaribio la kuharibu mahusiano mwema baina ya nchi hizi mbili uliojengwa na wasisi wa mataiafa haya,miak mingi iliyopita.

(I) NGANO ILIYOSHIKILIWA KWA MUDA MFUPI KWENYE MPAKA WA NAMANGA.

Ni kweli,malori 15 yalishikiliwa kwenye mpaka huu kabla ya kuingia nchini Kenya kutokana na kutokidhi matakwa ya sheria ya forodha ya Afrika Mashariki ambapo serikali ya Kenya inaitekeleza kisawasawa.
Hata hivyo,baada ya kukidhi matakwa hayo,malori yote 15 yaliruhusiwa kuingia na kusambaza bidhaa zake kwenye masoko ya Kenya.

(II). MCHELE KUINGIZWA KENYA KUPITIA MPAKA WA ISEBANI/SIRARI.

Ikumbukwe kuwa,kwenye mpaka huu hakuna vigezo vya kupima ubora wa Mchele kabla ya kuingia Kenya kutokana na kuwa tayari mamlaka za ubora za Afrika Mashariki zilikwishathibitishwa kuwa,Mchele kutoka Tanzania una ubora unaokidhi matakwa ya matumizi kwa binadamu.

Kutokana na Mchele huo kutowekwa kwenye vifungashio na kuandikwa uasili wake kama inavyotakiwa na sheria ya ubora ya Afrika Mashariki,wasafirishaji na waingiza walishauriwa kukidhi kwanza matakwa hayo ya kisheria ambapo baada ya kukidha mahitaji hayo,bidhaa ziliruhusiwa kuingia na kutawanywa kwenye masoko ya Kenya,hivyo wananchi kufurahia bidhaa hizo.

Tofauti na upotoshaji huo wa mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari,Mchele na NGANO kutoka Tanzania unaingia kwa kutumia sheria ya soko la pamoja la forodha kadhalika na mkataba wake.

Ubalozi unahitimisha taarifa hii kwa kusema,
HAKUNA VITA YA KIBIASHARA BAINA YA KENYA NA TANZANIA na tu naomba vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kujiridhisha na taarifa zako wanazozirusha ili kutoharibu mahusiano mwema BAINA ya Kenya na Tanzania.

Ifahamike.kuwa,lengo kuu la Ubalozi wa Kenya nchini Tanzania ni kuhakikisha tunakuza mwingiliano wa KIBIASHARA mara mbili zaidi kwa lengo la kukuza vipato vya mataifa haya kufikia uchimi wa kati.

Imetolewa na ofisi ya Balozi wa Kenya nchini Tanzania
27/9/2018.

Mungu ibariki Kenya,Tanzania na Afrika kwa ujumla.




IMG_20180927_090536.jpeg
IMG_20180927_090551.jpeg
IMG_20180926_224308.jpeg
 
Basi kuna chuki, mko ofisini mnatoa matamko, mitaani watu wanakomoana!
 
Basi kuna chuki, mko ofisini mnatoa matamko, mitaani watu wanakomoana!
Ungefafanua ili hatua zichukuliwe na serikali zote mbili kuliko kulalamika tu maana pasipo utafiti hata haki ya kuzungumza inafungwa.!
 
Ungefafanua ili hatua zichukuliwe na serikali zote mbili kuliko kulalamika tu maana pasipo utafiti hata haki ya kuzungumza inafungwa.!
Watoke maofisini na wawatembelee wananchi waongee nao!
 
Back
Top Bottom