Hakuna sababu za kuhoji PhD ya Magufuli

Hakuna sababu za kuhoji PhD ya Magufuli

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
1,056
Reaction score
1,086
TANGAZO la muswada wa sheria ya uhalifu wa kimtandao (Cybercrime Bill) lililowekwa hadharani na serikali katikati ya mwaka jana liliniweka katika kipindi kigumu. Kwa upande, kama mmoja wa watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii sambamba na kuwa miongoni mwa mabloga wa kwanza kabisa wa Kitanzania, ni muumini mkubwa wa uhuru wa habari.

Ninaamini kwa dhati kuwa uhuru wa habari ni haki ya msingi ya kila binadamu, iwe kueleza habari, kupata au kupatiwa habari.

Kwa hiyo kutetea muswada huo ambao baadaye ulipitishwa na kuwa sheria lilikuwa suala gumu kwangu. Nilitambua bayana kuwa muswada huo ukiwa sheria, ungeweza kutumiwa vibaya na vyombo vya dola kuwanyima wananchi uhuru wao kwenye habari na maoni.

Hata hivyo, nilikwishawahi kuwa mwathirika wa makosa ya kimtandao. Wakati fulani nilifikia hatua ya kutaka kujiondoa kwenye mtandao mmoja wa kijamii baada ya kuandamwa mfululizo pasipo sababu yoyote ile. Kwa hiyo, licha ya hofu kuwa muswada huo ungeweza kuzaa sheria yenye athari kwa uhuru wa habari na maoni, kwa kuzingatia uzoefu wangu mwenyewe nilivyonyanyaswa mtandaoni, ikanibidi tu niuunge mkono muswada huo.

Lakini pamoja na kuunga mkono hadi ulipopitishwa na kuwa sheria (Cybercrime Act), sijaridhishwa na ufanisi wake, ambapo sheria hiyo imeonekana kwa kiwango kikubwa kuwa na nguvu dhidi ya wanaofanya makosa ya kimtandao dhidi ya viongozi na sio dhidi ya wananchi wa kawaida.

Naendelea kuamini kuwa tatizo sio sheria hiyo bali utekelezaji wake. Na hilo ni tatizo letu takriban kwenye kila sheria. Laiti ikitumika vyema bila kubagua kati ya viongozi na wananchi basi kwa hakika itasaidia kufanya maisha yetu mitandaoni kuwa ya amani.

Nimekumbuka harakati za kuutetea muswada huo na baadaye sheria husika baada ya kubughudhiwa mno na jitihada zinazofanywa na kada mmoja maarufu wa chama kimoja cha upinzani huko nyumbani, ambaye kwa wiki kadhaa sasa amekuwa akifanya kila jitihada kutuaminisha umma kuwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Rais Dk. John Magufuli ni feki.

Miongoni mwa misingi ya hoja yake hiyo ni madai kuwa hajaona machapisho ya kitaaluma ya Dk Magufuli, kitu ambacho licha ya kuelezwa amegoma kukikubali ni kwamba uamuzi wa kuandika na kuchapishwa maandiko ya kitaaluma ni uamuzi binafsi, isipokuwa tu kwa wahitimu wanaobaki vyuoni kama wahadhiri.

Hiyo haimaanishi kwamba mtu aliyehitimu shahada iwe hiyo ya uzamifu, uzamili au ya kwanza, hapaswi kutoa machapisho ya kitaaluma kwa vile tu hatarajii kuwa mhadhiri. Tofauti kubwa ni kwamba wakati ni muhimu kwa ‘wasomi’ waliopo vyuoni kama wahadhiri kutoa machapisho ya kitaaluma, wanafunzi au wahitimu wa shahada hawalazimiki kufanya hivyo isipokuwa kwenye dissertation au thesis zao.

Lakini huyo kada wa upinzani hajaishia kwenye madai hayo tu bali amekwenda mbali na kudai kuwa rais aliandikiwa PhD yake. Kadhalika, amehusisha hoja yake hiyo na uteuzi wa msomi mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuwa mwenyekiti wa bodi moja ya taasisi ya umma, kama fadhila ya Dk Magufuli kwa Profesa aliyekuwa msimamizi wa PhD yake (na aliyemwandikia PhD hiyo).

Kijana huyo anadai kuwa kabla Serikali ya Dk Magufuli haijaanza uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, aanze yeye kuhakikiwa PhD yake. Asichosema ni kuwa uhakiki huo wa PhD ya Dk Magufuli ufanyike vipi, Rais akiombe Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufanya uhakiki? Aiombe wizara kumhakiki? Au amwite kijana huyo athibitishe yeye mwenyewe? Na athibitishe nini kati ya chapisho la mwisho wa PhD (thesis) au cheti cha shahada ya uzamivu?

Kama mtu ninayefahamu vema kibarua cha kusaka shahada ya uzamivu, nilijaribu kumuelimisha kada huyo lakini akanigeuzia kibao kwa hoja zisizo na mashiko.

Kasoro kuu katika hoja ya kada huyo ni kutoa hukumu kabla ya kuweka hadharani uthibitisho wa hoja yake. Kwa kuwa yeye ndiye mwenye tuhuma, basi jukumu la kuzithibitha (burden of proof) kuwa PhD ya Dk Magufuli ni feki lipo mikononi mwake na sio kwa rais wetu.

Na jaribio lake la kujitetea kuwa anatumia haki ya kutoa maoni halina mashiko kwa sababu haki huendana na wajibu. Pasipo uthibitisho wa madai yake, anachokifanya kada huyo ni uzandiki, na hilo ni kosa kubwa linaloangukia kwenye uzito wa makosa ya ugaidi, uhujumu wa uchumi na hujuma (shughuli kuu nne za adui kwa mujibu taaluma ya usalama wa taifa)

Raia Mwema
 
unasemaje???

na yenyewe ihakikiwe??

eti ni feki?
sasa mnataka kunijaribu,kwa taarifa yenu mimi sijaribiwi
 
TANGAZO la muswada wa iwa


Na jaribio lake la kujitetea kuwa anatumia haki ya kutoa maoni halina mashiko kwa sababu haki huendana na wajibu. Pasipo uthibitisho wa madai yake, anachokifanya kada huyo ni uzandiki, na hilo ni kosa kubwa linaloangukia kwenye uzito wa makosa ya ugaidi, uhujumu wa uchumi na hujuma (shughuli kuu nne za adui kwa mujibu taaluma ya usalama wa taifa)

Raia Mwema
mbona anahukumu kama yeye anajua kuwa Phd ni halali mbona hajaleta uthibitisho??

anatetea yeye kama nani?aleta uthibitisho wa utetezi wake aache kujipendekeza.
 
Umeulizwa na Ben Saanane ilikuwaje JeiPiemU apate Ph.D kwa miaka mitatu wakati hakuwa Full Time? Anza kujibu hapo kwanza.
 
images.jpeg


swissme
 
Swali la kujiuliza, kabla hujaenda mbali, ni kwanini huyu kijana anatilia shaka Phd ya bwana mkubwa? Inawezekana hoja yake ikahusishwa na matamko ya bwana mkubwa kwamba yanaonyesha kiwango cha chini cha weledi? uwezo wake wa kufikiri na kujenga hoja unatia shaka? kutoonekana kwa basic justifications za kuwa na Phd?
Je ni kweli bwana mkubwa yuko hivyo? Mimi sina jibu.
 
Ya kawaida sana hilo mkuu, Kwa nini hasiakikiwe ilihali nae ni mtumishi wa Serikali???

Mbona watumishi wengine wanahakikiwa?? Kwa kutuonyesha mfano anapaswa kufanya hivyo ili wa chini wake wasiweze kukwepa.

Mbona alikuwa wa kwanza kuhakikiwa Bastola yake mbele ya Mkuu wa Mkoa pale Dsm na huku kwa nini Ikulu isiwe ofisi ya kwanza kuanza swala la uhakiki wa vyeti.

Hili swala haliitaji Upinzani wala Chama tawala, Vihiyo wote watoke Serikalini.

Aibu gani hii ndo maana waliotutangulia kuliona jua wamewahi kutuonya kwa kusema tunakwenda kama Gari Bovu.
 
We unaye hoji hivyo umefikia level ipi ya elimu? Usikute ni mmoja wa wale mnaohaha kutafuta Loss report na kwenda gazetini kutoa taarifa nimepoteza cheti. Ukiona hivyo imekugusa kwa namna flani. Msema kweli sikuzote ni mpenzi wa Mungu.
 
Nidhamu lazima irudi maofisini. Zile mbwembwe na manyanyaso wakati mtu kaishia darasa la sita halafu anaringia masters yake, ni lazima zife.

Ni aina fulani ya kujifariji, mtu anapohoji PHD ya mkuu kabisa, wanachosahau watu wa aina hii ni ule ukweli kwamba mkuu kabisa kashika mpini na wao wameshika makali. Kama vyeti vyao ni feki imekula kwao mazima, wawapishe wenye vile vyeti original.

Tuiokoe nchi ili isiendelee kuwa na maisha ya ujanja ujanja, ili vizazi vya kesho na keshokutwa visiwe na umbumbumbu mwingi kwenye mambo ya msingi maishani.

Tunashindwa kwenye kila sekta kimataifa, mara ya mwisho Taifa Stars imeshiriki AFCON mwaka 1980. Miaka 36 iliyopita. Tunazo kila aina ya rasilimali ambazo majirani zetu wengi hawana, lakini kuna tatizo katika kuzitangaza.


Na kushindwa kwetu kunachangiwa na maisha ya ubabaishaji wa wasomi ambao baadhi yao hawastahili kuwa katika nafasi za kazi walizonazo.

Iwe PHD ya mheshimiwa ni original au feki, ujumbe wa kuwaondoa waliofoji vyeti kutoka katika nafasi wanazozishikiria, ni muhimu sana sio kwa kizazi cha leo tu, mpaka vizazi vingi vijavyo.
 
Mhakiki mkuu anapogoma kuhakikiwa, na badala yake wapenda vyeo wanajitokeza kifua mbele kumjibia, viongozi wanatakiwa wawe mfano kwa wanaowaongoza afanye kama alivyofanya kwenye swala la silaha
 
Mi naona ahakikiwe,kama aliweza kujitokeza kuhakikiwa bunduki zake,nadhani hata kwa vyeti vyake apeleke tu vikahakikiwe
 
Swali ni kwamba Thesis ya Mkuu ni halali? Je, haikuwahi kufanyika popote duniani? Tuanze kwa kujiuliza kama kabla ya 2008 haikuwa imewahi kufahamika kuwa maganda ya korosho yana vitu vinavyoweza kuzuia kutu na jinsi ya kuvi-extract.
 
Back
Top Bottom