Hakuna record label ninayoweza kukubali inisainishe, watanipa nini ambacho sijafanya! – Diamond

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Diamond Platnumz hana mpango wa kuwa chini na record label yoyote duniani. Infact hitmaker huyo amedai kuwa makampuni kibao yamewahi kummendea yakitaka awe chini yake lakini akayapiga kibuti.

“Mimi nimeshaapprochiwa na makampuni mengi sana kutaka kunisaini, mengi sana, mengi hata wanayoyasikia, mengine wanayasikia,” Diamond ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Lakini nafikiria kwamba unapotaka kunisaini mimi unataka kunifanyia nini? Una kitu gani cha kunioffer cha kuona mimi unisaini? Video? Mimi naweza kufanya video zangu hadi za wasanii wangu. Collabo? Collabo mimi naombwa napigiwa simu, msanii wa Marekani wa Tanzania, yeyote nikitaka kufanya chochote naweza kufanya naye,” ameongeza.

“At the end of the day is all about money, nina capital, nina network, ndio maana nikasema kwa nilipofikia sio nibaki mimi tu, niwe na record label yangu. So sifikirii kusainishwa, nafikiria kusaini watu ili kuweza kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.”

“Kwa mfano unataka kunisaini, unataka kunifanyia nini? Nikaperform mbinguni? Tuzo zote ambazo mwaafrika anatakani kuziwin.. sijawahi kupata BET na Grammy tu, nataka nipige na Grammy nioneshe kabisa napiga na Grammy. Ukiniambia nasainiwa it doesn’t make sense. Naamini management yangu ni kubwa kuliko mtu yeyote akinisaini, akisema anifanyie promotion hatoweza kufanya promotion ninayoifanya mimi,” amesisitiza.

Diamond aliyeanzisha record label yake, WCB tayari amewasaini Harmonize na Raymond huku kukiwa na uwezekano kuwa amemshamsaini Rich Mavoko.
 
kuna uhusiano wa moja kwa moja wa uswahili na utandale yeye ni nani mbona wakina chris brown lil wayne kanye jay z nk wapo chini ya record lebel yan huyu ni ili mradi tu aonekane hamkubali kiba ila akubali akatae ishamuingia haina namna atulie na kiki zake #aje
 
Aiseee
Michael Jackson
Adele
Drake
Nick Minaj
Hawa wote walipata au wanapata hela nyingi kuliko yeye
Hawa wana fan base kubwa kuliko yeye
Hawa wote walikuwa au wako kwenye label

Ni maoni yangu tu msinipige mawe maana hamchelewi
 
Huyu kijana inabidi apunguze majigambo kwa jinsi wasanii wakubwa wa nje wanavyohitaji au wanavyopenda kuwa chini ya lebo yeye anaponda hata sijamuelewa.Wakati mwenzie alipohojiwa hakuonesha dharau wala kinyongo kama kama yeye.Kweli jamaa bado ana asili yake ya ule uswazi wa Tandale.
 
Sio lazima afanye kama wasanii wengine wanavyaofanyaa kwann awape faida au kutajirisha watu wengine misina Team ila kunapoint kaongeaa sio kisa wasanii wambelee wenye majina makubwaa wapo kwenye record lebel na nassibu nae lazima awe kwenye hizo system hizo kampuni zinafaidika sanaaa wanapata zaidii ya kile wanachopata wasanii
 
Mkuu
Huyu kijana inabidi apunguze majigambo kwa jinsi wasanii wakubwa wa nje wanavyohitaji au wanavyopenda kuwa chini ya lebo yeye anaponda hata sijamuelewa.Wakati mwenzie alipohojiwa hakuonesha dharau wala kinyongo kama kama yeye.Kweli jamaa bado ana asili yake ya ule uswazi wa Tandale.
hayo si majigambo kijana kaongea reality ... si kwamba ameongea kwa dharau bali ameongea kwa kujivunia kabisa na kimsingi ana haki kbsa ya kujivunia ila kwakuwa wewe mtazamo wako bado ni ule ule ni haki yako kbsa kuuona huo ujumbe kwa mtazamo wa dharau lakini ki ukweli msanii unatakiwa uwe hivyo ... with CAPITAL and NETWORK.
 
Ila wasanii wengi wa Africa naona hizi Lebo za nje hawazifagili mmoja wapo wizkid naona sasa hivi anakazania lebo yake ya starboy worldwide, olamide YBNL na hata ice prince ambaye yupo chini ya legendary MI chocolate city mkataba wake unaisha na anaanzisha lebo yake. Hao wote ni wasanii wakubwa Africa, nahisi lebo za nje bado hawaja ujua mziki wa Africa na soko Lake,kwa mimi hapa Africa lebo kubwa naiona mavins ya Don jazy. Kwa diamond naona nae anaamini kama hao wasanii wa Nigeria, ila mwisho wa siku kila mtu achwe afanye anachokitaka as long anaona kitamfikisha ktk target zake.
 
Mkuu

hayo si majigambo kijana kaongea reality ... si kwamba ameongea kwa dharau bali ameongea kwa kujivunia kabisa na kimsingi ana haki kbsa ya kujivunia ila kwakuwa wewe mtazamo wako bado ni ule ule ni haki yako kbsa kuuona huo ujumbe kwa mtazamo wa dharau lakini ki ukweli msanii unatakiwa uwe hivyo ... with CAPITAL and NETWORK.
Sawa mkuu sijakataa swala la capital na network ni zuri kwa kila mfanya biashara.Ila unaamini kuwa kwa mafanikio ya Diamond anamzidi Nick Minaj au P Didy???
Hayo ni mambo ya kitoto kuponda mafanikio ya wengine so haoni kuwa wale waliochini yake pia wanajihisi inferiority kwa hizo kauli zake.
 
Mkuu sijaona kama kamtaja mtu au kuna jiwe lilirushwa gizani?
 
ingetosha tu kusema haitaji kuwa chini ya label ya mtu bali yake mwenyewe, hayo mengine aliyoongea ni pumba tupu . Kwa hizo show za kitchen party huko ulaya na marekani ndo kashamliza show za hapa duniani?
 
Naamini kila mtu ana njia yake au anatumia njia yake kufikia mafanikio..
Siyo lazima kwa sababu flani kafanya hivi na mimi nifanye hivi..
Kama yeye kaona njia anayoitumia inamnufaisha basi haina haja ya yeye kuwa na management.
Keep the fire burning SIMBAAAAAAAAAAA
 
huyu kijana anatudhihirishia kushuka sana, na kwenye mziko hakuna anachokifahamu, sasa asubiri hao madogo wake wampge chini ndo atajua
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom