Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 879
- 969
"Kuelewa, kufahamu na kuamua kutoelewa:
Ni ukweli usiopingika kuwa katika baadhi Ya maeneo nchini kumekuwa na upungufu wa mvua au kunyesha kinyume na hali yake ya kawaida (inconsistency). Hili wote wenye uelewa na ufahamu tunalijua.
Kutokana na upungufu au unyeshaji wa mvua usio wa Kawaida kama tulivyozoea kuna baadhi ya maeneo mazao yameathiriwa na jua hasa mvua inapokosekana mfululizo kwa wiki moja hadi mbili. Hili pia liko wazi.
Kuhusu uwepo wa njaa hapa ninaungana na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na wachache wenye uelewa na ufahamu kuwa Tanzania hakuna njaa. Hapa ninawaacha wasiotaka kuelewa au ambao wanaodhani kutangaza njaa ni sifa au keek yao ya kisiasa wabaki na ujinga au kutokuelewa kwao.
Kwa nini Tanzania hakuna njaa, Naomba nitoe sababu zangu kwa mujibu wa uelewa na tafsiri yangu na matokeo ya field. Naomba pia ieleweke majibu yangu ni kwa mujibu wangu
1. Tanzania inapokea mvua za aina mbili, kuna UNIMODAL na BIMODAL. bimodal ni maeneo yanayopokea mvua mara mbili kwa mwaka, yaani mvua za vuli kuanzia Oktoba hadi Januari na Machi hadi Mwishoni mwa Mei (Kwa mfano maeneo ya Dar es salaam na ukanda wa pwani na maeneo ya mwambao wa ziwa yaani interlacustrine regions) . Maeneo haya hupata mavuno yake kuanzia mwezi Februari hadi Juni. Maeneo yanayopokea mvua mara mbili yaani bimodal ni machache sana kulinganisha na yale yanayopokea mvua mara moja yaani unimodal.
2. Maeneo yanayopokea mvua mara moja (Unimodal) haya ndio mengi zaidi na hupokea mvua kipindi cha masika tu ambayo huanza Desemba hadi Mei maeneo haya hupata mazao yake kuanzia Aprili hadi Agosti.
Hivyo basi maeneo mengi yanayotegemea mvua mara mbili (bimodal) yamepata upungufu au mvua zisizo na uwiano mzuri kwa mvua za Oktoba-Januari lakini jambo lililopelekea baadhi ya watu na wanasiasa kushadadia uwepo wa njaa au ukame kitu kisicho na ukweli wowote.
3. Kwa kulinganisha maeneo yote mawili, lile linalopokea mvua mara mbili na lile linalopokea mvua mara moja na ukiachilia mbali maeneo yanayotegemea umwagiliaji, muda wa mavuno wa mazao ya kilimo kwa kawaida unaanza mwezi februari hadi Agosti. Na kwa wakati huu ama mvua zingekuwepo kama kawaida ama kama hali ilivyo bado muda wa mavuno haujafika hivyo ni dhambi kutangaza njaa wakati hata wakati wa mavuno haujafika.
4. Kwa kuwa bado muda wa mavuno haujafika, chakula kinachotumika ni kile kilicholimwa 2015/2016 ambacho kwa kumbukumbu sahihi kilikuwa kingi na mpaka wauzaji wa nafaka na baadhi ya wabunge walimuomba Rais aruhusu chakula kuuzwa nje ya nchi( hii ni miezi sita tu iliyopita). Hivyo wanaotaka kuelewa waelewe kuwa chakula kinachotumika ni cha msimu uliopita na sio kilichopo shambani na kwa kumbukumbu nchi ilikuwa na surplus na kwa sababu hiyo chakula bado kipo. Kwa wale wanaoelewa na waelewe.
5. Rais kukataza wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Baada ya kupatikana kwa mavuno mengi mwaka 2016 na mheshimiwa Rais Magufuli kupiga marufuku chakula kuuzwa nje ya nchi na kuwasisitiza wakulima kutunza chakula na kwamba mkono wake usingeizinisha kutoa msaada wa chakula kwa yeyote au sehemu yoyote ambayo ingepata tatizo la upungufu wa chakula ilhali kilikuwepo na watu walisisitizwa kutokuuza. Baadhi ya wakulima walishirikiana na wabunge kuhanikiza Rais atoe kibali na walanguzi wa chakula walianza kumchukia Rais kwa kitokutoa kibali cha nafaka kuuzwa nje (Hii ni miezi minne tu iliyopita)
6. Upungufu wowote wa chakula unaweza kurekodiwa endapo mvua hazitakuwa za kuridhisha hadi mwisho wa msimu huu yaani Mei 2017, na hivyo madai yoyote ya upungufu wa chakula yanaweza kurekodiwa kuanzia mwezi Novemba, 2017 kama hali ya mavuno haitakuwa nzuri kwa kipindi cha 2016/2017.
Kwa uelewa huu mdogo lazima tukubaliane kuwa kuna familia au watu hulala njaa hata kama msimu ni mzuri sio tu vijijini hata watani zangu wa Daslamu. Hivyo suala la mtu au familia kukosa chakula ni jambo la kawaida ambalo huchangiwa na sababu nyingi. (zinajulikana)
Kwa andiko hili nimshukuru na kumpongeza mheshimiwa Magufuli kwa maono yake ya kupiga marufuku chakula kuuzwa nje hata kama wakati ule mavuno yalikuwa mengi na wakulima walilazimika kuuza kwa bei chee.
Pia niwape Pole wale wanaotafuta picha ama za ukweli ama za mtandao kuonyesha mashamba ambayo mazao yamekauka na kuulazimisha umma kuamini kuwa hali iko hivyo nchi nzima. Njaa haisifiwi ndugu zangu.
Kwa andiko hili naomba anayetaka kubishana asome, aelewe na awe tayari kuelewa. Vinginevyo usichangie mjadala.
Kwa maaskofu, naomba waendelee kuombea mvua zinazoendelea kunyesha zinyeshe kama ambavyo hunyesha. Mavuno bado na bado kinatumika chakula cha 2016, wafanye tathmini kabla ya.....
Wakulima waendelee kuhifadhi chakula na ikibidi kuuza kwa ajili ya kujikimu, wauze kwa bei ya soko.