Hakuna nishani ya ndoa, jipange kwanza na epuka presha za watu, wengi wanalia moyoni, ningejua!!

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
653
Nianze kwa kusema ndoa ni kitu chema na inapaswa kuwa sehemu ya amani na sio maradhi wala vita.

Kumekuwa na kitabia kinachokera sana, kila mtu akiona bao hujaoa au kuolewa utasikia unasubiri nini utazeeka, au sijui utaitwa babu au vinginevyo

Ndio sio kitu cha kukimbilia, kitu cha kuiga wala cha kuonyesha watu. usimshangae mtu ukikuta hajaolewa au kuoa kwa muda unaotaka wewe au unaodhani wewe ni sahihi. epuka kumpa mtu presha za ndoa kwa sababu wewe uko huko.

Wengi walio kwenye ndoa wanayajua sana sana waliokurupuka. siri ya wanachokipata wanayo wenyewe. usimshangae mtu akifika miaka 30 hajaoa, ana mipango yake.

Ndoa sio kitu cha kujaribu wa kuiga. ingia kwenye ndoa ukiwa na wito, utayari wa mwili na akili na pia utayariwa uchumi ikiwa kulea matumbo zaidi ya matano mwaka mzima bila kukosa kitu.

Hakuna nishani ya ndoa, kwamba ukikimbilia na kuwahikuoa mapema utapata. ndoa ni kitu cha maelewano ya watu wawili yaani mwanaume na mwanamke ambao wanaona wanaweza kuishi pamoja kwa kusaidia na kuheshimia na kukidhiana tamaa.

Tusipende kuishi kwa mikumbo na pia tusipende kuwalazimisha watu waishi kwa mitizamo yetu au experience zetu. usipende kuwauliza uliza watu kuoa.

Kama mwanaume yuko kamili hawezi kuuambiwa aoe muda fulani wakati yeye mwenyewe anajielewa.

Pia kwa wadada, ndoa inatakiwa kuwa sehemu ya maelewano na amani, usiolewa sababu ya umri umeenda, kama yupo wako atakuja tu.

Ukikurupuka kama unakufa kesho utapata jipu uchungu likusumbue mpaka upate kisukaru na mapresha alafu ufe taratibu kwa mateso makali.

Maisha ni jinsi unavyojipanga. Lazima ujipange na kitu cha muhimu kwenye maisha haya ni kifurahia kila siku ukiwa hai.

Usikubali kuishi kwa kunyanyasika sababu ya umri. ishi kwa furaha maana maisha ni mafupi na ukifa hamna maisha tena. Ishi kwa kufurahia kila siku Mungu anayokupa ili uishi vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Tumeyashika hayo mkuu,wengi wanaoa au kuolewa kisa agements wao tayari na wengine ni kwa pressure tu ya ndugu na wazazi.
ni kosa sana kuoa kwa ajili ya kumfuhisha mzazi wako. oa kwa ajili ya maisha yako. wazazi wamekwisha ishi maisha yao na ndo kwa kunaanza kuwa giza, lakini wewe ndio bado kabisaaa. huna haja ya kukimbilia sana
 
Tatizo wengi wetu tunajikuta umri umeshaenda si kwa sababu tuna mikakati saana, laa ila ni kwa sababu ya kutojitambua.

ANGALIA.

Kijana wa kiume anakula ujana kwanza,ujana unaliwa kweli kweli kuanzia lets say 23-33.....hana mikakati kwa ajiri ya hiyo familia yenyewe itakayokuja atakapoamu,ntajenga tu, nitafungua kitega uchumi nikioa, akiba ya nn huku sina mtoto,GHAFLA 30 hii hapa.hukuoa kwa hiyari kelele zinaanza kutoka kwa wazazi, ndugu na wadau wengine.
Mara unataka tusimuone mkwe wetu na wajukuu???, una matatizo gani wewe???angalia wakina jofrey wanavyopendeza na familia zao na ni wadogo zako!!!,utazeeka wewe watoto watalelewa na nani??? Halafu ukichunguza hamna jungu hata moja hapo ni ukweli mtupu.kidume ndio unakurupuka sasa na 120 unabeba lolote tu tia ndani.

Mdada-yeye huyu anakwambia ndoa stress tupu.wakati huo yupo between 20-27 hapo.anaendelea kutest radha mbali mbali za kiulimwengu na kujiaminisha hawezi chungwa kama jirani mama flan.good enough wadau wanaisugua mpaka inakuwa nyeusi na injini kazaa zinateremshwa.about 28 pale huku umeanza kuwa mkali kwa wadogo zako kwa makosa za kawaida tu.unaanza kuulizwa mwenzetu kulikoni mbona kimya kingi.umemuona shemeji yako kwa mdogo wako suzi??? Wewe lini??? Utajifanya kauzu kujibu mi sihitaji, usingizi utakatika usiku wa manane unaanza kutafakari upya.mara unaanza kuhudhulia kanisani kwa kasi na maombi kwa wingi.mara umekuja na shemeji yetu mtarajiwa kumbe kaacha mke na watoto kyela huko sjui.
KWANINI UFIKIE HUKU??????.

Kuweni makini bana.
 
Mi nashangaa watu kumkomalia mtu ataoa/olewa lini.
Muwaache watu na maisha yao.
Yani kuna watu wanaishi maisha magumu kwa sababu ya mashinikizo.
Asipofanya hili anasakamwa wakati hakua na mpango wa kulifanya.
Akilifanya hana furaha nalo.
Kero tu.
 
nianze kwa kusema ndoa ni kitu chema na inapaswa kuwa sehemu ya amani na sio maradhi wala vita

kumekuwa na kitabia kinachokera sana, kila mtu akiona bao hujaoa au kuolewa utasikia unasubiri nini utazeeka, au sijui utaitwa babu au vinginevyo

ndo sio kitu cha kukimbilia, kitu cha kuiga wala cha kuonyesha watu. usimshangae mtu ukikuta hajaolewa au kuoa kwa muda unaotaka wewe au unaodhani wewe ni sahihi. epuka kumpa mtu presha za ndoa kwa sababu wewe uko huko
wengi walio kwenye ndoa wanayajua sana sana waliokurupuka. siri ya wanachokipata wanayo wenyewe. usimshangae mtu akifika miaka 30 hajaoa, ana mipango yake

ndoa sio kitu cha kujaribu wa kuiga. ingia kwenye ndoa ukiwa na wito, utayari wa mwili na akili na pia utayariwa uchumi ikiwa kulea matumbo zaidi ya matano mwaka mzima bila kukosa kitu.
hakuna nishani ya ndoa, kwamba ukikimbilia na kuwahikuoa mapema utapata. ndoa ni kitu cha maelewano ya watu wawili yaani mwanaume na mwanamke ambao wanaona wanaweza kuishi pamoja kwa kusaidia na kuheshimia na kukidhiana tamaa.
tusipende kuishi kwa mikumbo na pia tusipende kuwalazimisha watu waishi kwa mitizamo yetu au experience zetu. usipende kuwauliza uliza watu kuoa. kama mwanaume yuko kamili hawezi kuuambiwa aoe muda fulani wakati yeye mwenyewe anajielewa.

pia kwa wadada, ndoa inatakiwa kuwa sehemu ya maelewano na amani, usiolewa sababu ya umri umeenda, kama yupo wako atakuja tu. ukikurupuka kama unakufa kesho utapata jipu uchungu likusumbue mpaka upate kisukaru na mapresha alafu ufe taratibu kwa mateso makali. maisha ni jinsi unavyojipanga. lazima ujipange na kitu cha muhimu kwenye maisha haya ni kifurahia kila siku ukiwa hai
usikubali kuishi kwa kunyanyasika sababu ya umri. ishi kwa furaha maana maisha ni mafupi na ukifa hamna maisha tena. ishi kwa kufurahia kila siku Mungu anayokupa ili uishi vizuri
Nilivutiwa sana na title ya thread nikijua thread ina real life experience, kumbe blah blah tu! Unajutia nini sasa?
 
Tatizo wengi wetu tunajikuta umri umeshaenda si kwa sababu tuna mikakati saana, laa ila ni kwa sababu ya kutojitambua.

ANGALIA.

Kijana wa kiume anakula ujana kwanza,ujana unaliwa kweli kweli kuanzia lets say 23-33.....hana mikakati kwa ajiri ya hiyo familia yenyewe itakayokuja atakapoamu,ntajenga tu, nitafungua kitega uchumi nikioa, akiba ya nn huku sina mtoto,GHAFLA 30 hii hapa.hukuoa kwa hiyari kelele zinaanza kutoka kwa wazazi, ndugu na wadau wengine.
Mara unataka tusimuone mkwe wetu na wajukuu???, una matatizo gani wewe???angalia wakina jofrey wanavyopendeza na familia zao na ni wadogo zako!!!,utazeeka wewe watoto watalelewa na nani??? Halafu ukichunguza hamna jungu hata moja hapo ni ukweli mtupu.kidume ndio unakurupuka sasa na 120 unabeba lolote tu tia ndani.

Mdada-yeye huyu anakwambia ndoa stress tupu.wakati huo yupo between 20-27 hapo.anaendelea kutest radha mbali mbali za kiulimwengu na kujiaminisha hawezi chungwa kama jirani mama flan.good enough wadau wanaisugua mpaka inakuwa nyeusi na injini kazaa zinateremshwa.about 28 pale huku umeanza kuwa mkali kwa wadogo zako kwa makosa za kawaida tu.unaanza kuulizwa mwenzetu kulikoni mbona kimya kingi.umemuona shemeji yako kwa mdogo wako suzi??? Wewe lini??? Utajifanya kauzu kujibu mi sihitaji, usingizi utakatika usiku wa manane unaanza kutafakari upya.mara unaanza kuhudhulia kanisani kwa kasi na maombi kwa wingi.mara umekuja na shemeji yetu mtarajiwa kumbe kaacha mke na watoto kyela huko sjui.
KWANINI UFIKIE HUKU??????.

Kuweni makini bana.
Umemaliza kila kitu
 
Nakubaliana na wewe lakini ni muhimu kila kitu kuwa na deadline kwa sababu mimi naamini ili kila kitu kikamilike kinahitaji timeframe hii husaidia kupanga vizuri na kutia juhudi kuyafikia malengo uliyojiwekea, kinyume cha hayo utakuwa na meli iliyotelekezwa baharini. Maisha ya binadamu kibaiolojia hayana tofauti na viumbe wengine,

jifunzeni kwa mimea mhindi mathalani, ukishaupanda ukamea mvua ikija utachanua na kuzaa baada ya hapo hukomaa na baada ya hapo huanza kunyauka hata kama mvua ikiendelea kunyesha hunyauka na kukauka kabisa baadaye ndivyo hata maisha yetu yalivyo

Watu wengi jukumu lao hapa dunianı, from ecological point of view, kiumbe kina majukumu shughuli kuu 2,ni kula na kuzaliana shughuli hizi ndizo viumbe vyote hapa dunianı hupambana kuzitimiza zingine ni mbwembwe tu.

Wanabaiolojia wanaamini kwamba organism that fails to pass on its generation is genetically distinct

Hii ndio sababu wanyama kama simba pundamilia n.k humtia msukosuko mate akiwa pregnant au anaponyonyesha aidha kwa kuwaua watoto (simba) au kumpiga mateke (punda mwenye mimba ili ku abort) na kuzaa naye au hata sisi wanaume kutopenda kulea watoto wasiokuwa ni muendelezo huohuo

Mmewahi kujiuliza kwamba hasara za kupata watoto in late? Unategemea nani atakulelea,unamwamini?life span yenyewe 70yrs umejitahidi sana! Kaa chini utafakari
 
Mi nashangaa watu kumkomalia mtu ataoa/olewa lini.
Muwaache watu na maisha yao.
Yani kuna watu wanaishi maisha magumu kwa sababu ya mashinikizo.
Asipofanya hili anasakamwa wakati hakua na mpango wa kulifanya.
Akilifanya hana furaha nalo.
Kero tu.
hao watu wanaokulazimisha na kukushawishi sana kuolewa au kuoa ukioa alafu ukaomba wakupe hata kamtaji kadogo utasikia komaa bwana. maisha ni yako so mwenye kufurahiau kuumia ni wewe,ni vyema kujipanga sawa sawa
 
Nakubaliana na wewe lakini ni muhimu kila kitu kuwa na deadline kwa sababu mimi naamini ili kila kitu kikamilike kinahitaji timeframe hii husaidia kupanga vizuri na kutia juhudi kuyafikia malengo uliyojiwekea, kinyume cha hayo utakuwa na meli iliyotelekezwa baharini. Maisha ya binadamu kibaiolojia hayana tofauti na viumbe wengine,

jifunzeni kwa mimea mhindi mathalani, ukishaupanda ukamea mvua ikija utachanua na kuzaa baada ya hapo hukomaa na baada ya hapo huanza kunyauka hata kama mvua ikiendelea kunyesha hunyauka na kukauka kabisa baadaye ndivyo hata maisha yetu yalivyo

Watu wengi jukumu lao hapa dunianı, from ecological point of view, kiumbe kina majukumu shughuli kuu 2,ni kula na kuzaliana shughuli hizi ndizo viumbe vyote hapa dunianı hupambana kuzitimiza zingine ni mbwembwe tu.

Wanabaiolojia wanaamini kwamba organism that fails to pass on its generation is genetically distinct

Hii ndio sababu wanyama kama simba pundamilia n.k humtia msukosuko mate akiwa pregnant au anaponyonyesha aidha kwa kuwaua watoto (simba) au kumpiga mateke (punda mwenye mimba ili ku abort) na kuzaa naye au hata sisi wanaume kutopenda kulea watoto wasiokuwa ni muendelezo huohuo

Mmewahi kujiuliza kwamba hasara za kupata watoto in late? Unategemea nani atakulelea,unamwamini?life span yenyewe 70yrs umejitahidi sana! Kaa chini utafakari
nakubalaiana na wwewe kwa maana ya timeline. lakini timeline ispoangalia uhaliasia wa hali inakuwa mateso kwa watoto.
nataka kukwambia kitu kuwa it is not absolutely necessary for you to your genetic information bila kuwa sure kwamba those genetic information zitakuwa safe vipi. kuwa genetic extinct au genetically available should take into consideration the point of mutation molecularly which might end up changing the fate of basic genome of the organism.kama weweukishindwa kurithisha genetic infomation wapo ndugu zako ambao kwa asilimia 98 mko genetically similar, let them do that for you.
point yangu hapani kwamba genetic information should take also consider environmental factors. kama environmental factors zitakuwa sio nsuri kuna hatari ya kupoteza hizo genetic information
swala siokuingia tu kwenye ndoa na kuzaa swla hapa ni je mtoto anazaliwa kwenye mazingira gani na analelewaje? yakobo alipewa ngombe ndio akaoa na mussa baada ya kuchunga mifugo miaka arobaini ndio akapewa mke na share yake. hii inamaanisha nikosa kuoa kama hujajiandaa kwa familia
 
Ndoa sio wajibu ni hiari ya mtu akiwa tayari ukiifanya kuwa wajibu ndo utakimbilia kuoa wakati haujajipanga ila unaoa sababu umeona umri unaenda marafiki wanaoa na kuolewa na wew unasema Mbna yule kaoa au kaolewa why not me unakurupuka miezi 2 mnakutana serikali ya mtaa mmetiana ngumi
 
Mnaweza kuwa genetically sawa lakini mkatofautiana tabia ambazo mara nyingi huathiriwa na mazingira na tabia hizi ndizo zinazoweza kutambua mwelekeo wa mtu why can't you strive to achieve yours do you leave your gene at the mess of your brother or sister?
 
Back
Top Bottom