Mara nyingi napenda kusoma vichwa vya habari vya magazeti mbalimbali kutoka Tanzania. Leo nimepitia mitandao mingi lakini sijaona vichwa vya habari au picha za kurasa za mbele za magazeti. Je ni mimi tu ndio sikuyaona au kuna mengine?
Asante nimeyaona, lakini kwa kawaida kuna sites nyingi sana kama facebook, Michuzi, Mjengwa n.k. ambazo pia huweka magazeti hayo. Cha kushangaza kote huko leo hakuna kitu!!
Hata mimi nimehisi hivyo kwa maana sehemu zote zile ambazo nimezoea kusoma hayo magazeti sikuona habari yoyote, si Michuzi wala Mjengwa wala facebook Magazeti ya Tanzania!!
Hii ndio Tanzania na waandishi wetu wa habari.Yapo Mengi sana yakuandika nakuuza.
Ndio maana huwa nasema acha hata waandishi wahabari wasiandike mema ya Serikali ili wapate Habari ya kuboost kisiasa zaidi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.