Hakuna kiongozi ‘spesho’ wote wanaweza

Hakuna kiongozi ‘spesho’ wote wanaweza

Richcountrytz

Member
Joined
Dec 17, 2014
Posts
9
Reaction score
2
Na Mwandishi wetu.

Yapo madai kuwa, baadhi ya viongozi ni ‘wateule’ au ‘majembe’ na hawawezi kuondoka madarakani hata wakiwa na madoa. Lakini ukweli unabaki kuwa kila mmoja akipewa nafasi anaweza, hivyo si muda wakujisifia wala kuwa king’ang’anizi madarakani.
Mchambuzi wa masuala ya Uongozi anaangalia dhana hiyo kwa kutizama wizara ya nishati na madini kuwa hivi kiongozi hawezi kung’atuka kwa madai eti ni ‘spesho’ Je, waliotangulia waliacha alama gani?
Sekta ya Nishati hasa mafuta kwa miaka mingi tangu kupatikana kwa uhuru miaka 53 iliyopita haijatoa mchango stahiki kwa maendeleo ya uchumi na pato la taifa kwa ujumla.
Sababu za kutokutoa mchango huo ni nyingi moja na uwekezaji duni, usimamizi unaolegalega na uingizaji holela wa mafuta yasiyokidhi viwango vya matumizi mbalimbali.
Mafuta yameingizwa nchini kwa mfumo usio rasmi na kwa miongo mingi watanzania walikuwa wakitumia nishati hiyo chafu na mengine yaliyochanganywa na mafuta ya taa au dizeli na kusababisha uharibifu wa mitambo.
Matokeo ya kuingizwa holela na hata wafanyabiashara kutumia mwanya wa soko huria kulisababisha malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwa wanauziwa mafuta machafu.
Hatua hiyo iliilazimu Wizara ya Nishati na Madini kuingilia kati na kufanya ukaguzi kwenye vituo vya mafuta na kubaini kasoro nyingi katika baadhi ya vituo ambapo kulikuwa na mafuta machafu.

Baadhi ya vituo vilibainika kuuza mafuta ya petrol yaliyokuwa yamechanganywa na mafuta ya taa. Lengo la kufanya hivyo ni wafanyabiashara kupata faida kubwa. Matokeo yake, baadhi ya vituo vilifungiwa au kutozwa faini kutokana na mchezo huo wa kuchakachua.

WILLIAM NGELEJA wakati huo akiwa Wizara ya nishati na madini, Wizara ilianzisha utaratibu wa kuagiza mafuta kwa pamoja uliojulikana kama ‘bulk procurement system’( BPS) uliofanywa na mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati za maji (EWURA).

Mfumo huo uliondoa ule wa awali uliokuwa umetoa mwanya kwa kila kampuni ya mafuta kuagiza mafuta kwa utaratibu wake, jambo lililosababbisha kuwepo kwa mafuta machafu vituoni pamoja na udanganyifu mkubwa katika ukusanyaji ushuru wa serikali.

Wakati mwingine, baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wakiagiza mafuta kwa kisingizio kuwa yanapelekwa nchi jirani za Zambia ,Congo, Rwanda lakini yalikuwa yakiishia katika mikoa ya Morogoro na Dodoma.
Licha ya udanganyifu huo, pia beinza mafuta zilikuwa zikipangwa kiholela ambapo kila kampuni ilikuwa ikijiwekea bei inavyotaka au wafanyabiashara hao kupitia umoja wao kuamua kuuza mafuta kwa kiwango ambacho wanapata faida bila kujali maslahi ya taifa.
Hata serikali ilipokuwa ikiingilia na wakati mwingine kushusha bei, wafanyabiashara hao walikuwa wakigoma na kusababisha adha kubwa kwa wananchi,
Kuanzishwa kwa mfumo huo, kulisaidia kudhibiti uwapo mafuta machafu kwenye vituo na hivi sasa hakuna malalamiko kama ilivyokuwa zamani.

Licha ya kusababisha usumbufu mwingi kuchakachua kunasababisha injini za magari kuharibika na mifumo ya mipira inayohusika na kusafirisha mafuta nayo kuharibika. Si hivyo tuu kuchanganya mafuta ya taa na petroli au dizeli kwa matumizi ya majumbani kunasababisha majiko kulipuka na ajali za moto.
Kubwa zaidi, bei ya mafuta imekuwa ikishuka kila uchao kutokana na ukweli kwamba hakuna udanganyifu na pia mfumo huo umesaidia serikali zaidi y ash. bilioni 500.
Pia usumbufu uliokuwa ukifanywa na kamopuni za mafuta kabala ya kuanza kwa mfumo huo, haupo tena. Ili utaratibu huo uweze kuwa endelevu na kuboreshwa kwa nidhamu katika biashara ya mafuta, Waziri NGELEJA wakati huo alisimamia kutungwa kwa sheria ya mafuta ya mwaka 2008 ambayo iliweka utaratibu wa ununuzi wa mafuta kwa pamoja BPS.

Mbali na sheria hiyo kuweka miongozo na taratibu za uagizaji wa mafuta kwa pamoja badala ya ule wa kila kampuni kufanya ilivyotaka, Pia inapendekeza kuanzishwa kwa akiba ya taifa ya mafuta.
Katika kuhakikisha pia upatikanaji wa mafuta unakuwa wa uhakika mwaka 2011 Wizara ya Nishati na madini ilisimamia kufufua kampuni ya mafuta ya serikali ya Commercial Petroleum Company of Tanzania (COPEC) ambayo inaendeshwa na shirika la maendeleo ya petrol la taifa (TPDC). Kampuni hii ilikuwa imekwama tangu mwaka 2000.

Jambo linguine ambalo lilisimamiwa na NGELEJA wakati huo ni uendelezaji wa nishati na ugunduzi wa gesi asilia unaoendelea sasa hivi katiak maeneo mbalimbali nchini hasa ukanda wa pwani wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Kazi hiyo imesababisha kuwapo kwa kampuni nyingi za kutafuta na kuchimba gesi na mafuta ambayo iwapo yatapatikana yatasaidia kuchochea kukuza kasi ya uchumi wa taifa na kupunguza umasikini milngoni mwa watanzania.
Ugunduzi huo na kuanza kupatikana kwa gesi asilia kumewezeshakupunguza hata matatizo ya umeme yaliyokuwa yaameikabili nchi kwa kipindi kirefu.
Tayari hivi sasa swala la gesi limekuwa gumzo kwa wananchi ambao wameshuhudia kukamilika kwa bomba kubwa la gesi kutoka mtwara hadi dar es salaam.

Baadhi ya taasisi vikiwamo viwanda vimeanza kutumia gesi hiyo kwa matumizi mbalimbali. Mbali na matumizi hayo, gesi hiyo inatarajia kufanikisha upatikanaji wa umeme kma vile vituo vya kupokea nishati hiyo vya Kinyerezi mkoani Dar es salaam.

Lakini TPDC isingekuwa hivy ilivyo kwani ni kipindi hicho NGELEJA na timu ya wataalamu wa Wizara hiyo walicgukua uamuzi mgumu wa kuliboresha shirika hilo ili liende na mabadiliko ya maendeleo ya nishati nchini.

Miongoni mwa mabadiliko hayo ni kuliwezesha shirika hilo kuwa msimamizi mkuu wa masuala ya utafiti, ugunduzi na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia nchini.
Hivi sasa, kutokana na mabadiliko hyo, TPDC imekuwa imara tofauti na ilivyokuwa mwanzo kwa sababu imepewa nguvu na mamlaka makubwa katika usimamizi wa sekta ya nishati hususani mafuta na gesi.
Kwa mambo hayo yaliyofanyika kipindi hicho cha NGELEJA, mabadiliko makubwa yataendelea kuwa alama ya ukumbusho katika maendeleo ya sekta ya nishati nchini. Na chachu ya sekta hiyo hivyo kuwa mmoja miongoni mwa viongozi wenye kuthubutu katika maendeleo na mambo yanayowagusa wananchi.

Wakati huo ndipo jitihda za kulifufua shirika la madini la Taifa (STAMICO) zilipofanyika na sasa linaanza uwekezaji huko Buhemba na Arusha kwenye migodi ya Tanzanite kwa hiyo si kwamba kuna jembe kwenye kazi za umma, kila mmoja akipewa nafasi anaweza kuonyesha maajabu.


By:
Mtanzania Safi
 
Back
Top Bottom