Sijui kuna mahusiano gani bhana kati ya mvua na sikukuu za kidini..waumini watasema ni Neema hiyo.
Huku wenye imani haba utasikia wachawi wanaleta mvua ili kuharibu sikukuu sababu wao hawako vizuri kiuchumi.
Basi sisi wenye masikio yetu tunayapandisha juu kidogo ili tusikie wana sayansi nao watasemaje,sisi raha yetu ni kusikiliza tu basi.