Hakuna cha bure bongo chako utauziwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna cha bure bongo chako utauziwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngekewa, Apr 25, 2009.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mbegu DECI sasa kung'olewa kwa malipo
  Friday, 24 April 2009 16:19
  Na Edmund Mihale

  KAMPUNI Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) imezua biashara nyingine ya kuuza kadi zenye namba maalumu kwa ajili ya kujiorodhesha ili kung'oa mbegu.
  Uchunguzi uliofanywa na Majira na kuthibitishwa na mmoja wa washiriki wa kampuni hiyo umebaini kuwa kadi hizo maalumu zilikuwa zikiuzwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa lengo la kuwawezesha wanachama hao kuwahi kuingia kwenye ofisi hizo ili kujiorodhesha kung'oa mbegu zao.

  Uchunguzi huo umebaini kuwa kadi iliyoanzia namba moja hadi 200 ziliuzwa kwa sh. 20,000 hadi 30,000 kwa kadi moja.

  Kadi iliyoanzia namba 201 hadi 1,000 ilikuwa ikiuzwa sh. 5,000 hadi sh 10,000 kwa kadi moja. Kadi iliyoanzia namba 1,001 hadi 2,000 iliuzwa kwa sh.2,000 hadi 3,000 huku kadi ilianzia namba 2,001 hadi 3,000 iliuzwa kwa sh. 1,000.

  Hata hivyo uchunguzi huo ulibaini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kadi hizo kuuzwa bei kubwa zaidi kutokana na washiriki waliowekeza fedha nyingi ambao ni wajiriwa katika kampuni, mashirika na idara mbalimbali za Serikali kushindwa kusubiri foleni ndefu.

  Mshiriki Bi. Anna Kassim ambaye alijitambulisha kuwa ni mfanyakazi serikalini, alisema kutokana kushindwa kupata muda wa kutoka ofisini na kupanga foleni yuko tayari kununa kadi hiyo kwa sh. 70,000.

  Bi. Anna, alisema amewekeza fedha nyingi katika kampuni hiyo, hivyo kiasi atakachotoa kwa ajili kununulia kadi, si kitu .

  "Kaka nimesikia mnazungumzia kuhusu kuuzwa kadi naomba nami mnioeshe nani anauza, niko tayari kununua hata kwa sh. 70,000 iwapo itaanzia namba moja hadi 100 kwani nimeshindwa kupanga foleni," alisema Bi Anna huku akionesha risiti alizopandia mbegu hizo.

  Mbali na kuuza kadi hizo, biashara nyingine iliyojitokeza ni kuuza sehemu ya foleni kwa watu waliowahi na kupanga foleni mapema. Nafasi hiyo inauzwa sh. 500 hadi sh 2,000 kutokana na umbali kutoka msimamizi anayetoa kadi zenye namba.

  Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Kamati ya dharura ya washiriki wa DECI Mchungaji Isaack Kalenge, alisema leo ameitisha mkutano mkubwa katika viwanja vya Jangwani kwa ajili ya kujadili hatima ya fedha zo katika Kampuni ya DECI.

  Akizungumza na Majira kwa njia ya simu, Mchungaji Kalenge alisema lengo la mkutano huo ni kuitaka Serikali kuichia kampuni hiyo iendelee na huduma zake kama kawaida kwa kuwa hadi sasa hakuna madhara yoyote yaliyojitokeza.

  Alisema moja ya agenda ni kujadili kauli ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, aliyoitoa katika Kikao cha Bunge wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo kuwa kampuni hiyo ni ya kidini kwani hakutenda haki juu ya kampuni hiyo kwani imekuwa ikifaidisha watu wote bila kujali dini wala kabila.

  Alisema katika mkutano huo wamewalika viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa, wanasheria na wachumi.
   
Loading...