Hakimu apandishwa kizimbani kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakimu apandishwa kizimbani kwa rushwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by thatha, Sep 25, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ilala: Hakimu apandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumwomba mteja rushwa

  25/09/2012

  0 Comments




  Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala Pamela Kalala (kushoto),akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana,baada ya kusomewa shitaka la kuomba rushwa ya Shilingi milioni tatu. (Picha: Michael Matemanga/MWANANCHI)

  HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Pamela Kalala amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, kujibu mashitaka ya kuomba rushwa Sh milioni 3 na kupokea Sh 900,000.

  Kalala alipandishwa kizimbani jana mbele ya Hakimu Aloyce Katemana na kusomewa mashitaka yanayomkabili. Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Allen Kasamala alidai kuwa mshitakiwa anakabiliwa na mashitaka matatu.

  Kwa mujibu wa Kasamala katika tarehe tofauti Februari mwaka huu mshitakiwa akiwa katika Manispaa ya Ilala aliomba rushwa ya Sh milioni 3 kutoka kwa Josephine Wage. Wage ni mke wa mshitakiwa katika kesi namba 703 ya mwaka 2008, dhidi ya Aboubakar Hamis na wenzake, na alitaka kumshawishi ili atoe uamuzi wa kumpendelea mumewe katika kesi inayomkabili.

  Katika mashitaka la pili, Kalala anatuhumiwa kupokea rushwa ya Sh 800,000 kutoka kwa Wage, ikiwa ni ushawishi wa kutoa uamuzi wa kumpendelea mume wake huyo.

  Hata hivyo, Kasamala alidai kuwa katika mashitaka ya tatu, hakimu huyo anatuhumiwa kupokea rushwa ya Sh 100,000 kutoka kwa Wage Februari 6, ukiwa ni ushawishi wa kutoa uamuzi wa upendeleo.

  Mshitakiwa alikana mashitaka yote na Kasamala kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na upande wa Jamhuri hauna pingamizi juu ya dhamana.

  Katemana alisema ili mshitakiwa aweze kuwa nje kwa dhamana, anatakiwa asaini hati ya dhamana ya Sh milioni moja na mdhamini mmoja wa kuaminika atakayesaini hati ya dhamana ya kiasi hicho cha fedha.

  Mshitakiwa alikidhi masharti ya dhamana na kuwa nje hadi Oktoba 23 kesi hiyo itakapotajwa.

  Baada ya kutimiza mashati hayo, Kalala akifuatana na mtu anayedaiwa kuwa mumewe, walitoka mahakamani hapo kwa kupitia mlango wa nyuma kwa lengo la kukwepa wapigapicha waliokuwa wakisubiri picha yake. Hata hivyo, wapigapicha hao walimwona na kumkimbilia ili kumpiga picha, hata hivyo waliendelea kupata ugumu baada ya mumewe kumkumbatia huku akicheka kwa dharau na kuwataka wapige picha kadri wawezavyo.
   
 2. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hako ni dagaa tu. Wanaopiga fedha nzito zenye athari kwa maendeleo ya taifa wako mtaani. Hosea naye kuhusu suala la rushwa amekuwa mwanasiasa.
   
 3. Kitaeleweka

  Kitaeleweka JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 393
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  C liwalo na liwe bado hakijaeleweka tu?

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
Loading...