Hakikisheni wanarudi "lecole"

Hakikisheni wanarudi "lecole"

Mbaga Lazaro

Senior Member
Joined
Aug 9, 2020
Posts
132
Reaction score
109
Naibu katibu mkuu wizara ya elimu Prof Carolyne Nombo ameagiza watoto walioacha shule kurudi kwenye masomo na kuwataka maofisa elimu na walimu wakuu kuhakikisha wanasimamia wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali wanarejea mashuleni pindi shule zinapofunguliwa.la source ITV


Ikumbukwe kwamba serikali ya tanzania hivi karibuni imeruhusu wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na wale waliopata ujauzito kurudi shule jambo ambalo lilizua mjadala hasa kwenye mitandao ya kijamii wengine wakionekana kuunga mkono (ikiwa ni pamoja na wadau wa ndani ya nchi na nje ya nchi kama vile benki ya dunia na wadau wengine) na wengine kuonekana kutokukubaliana na msimamo huo.
 
Back
Top Bottom