"Kutibia watu kwa kutumia majini" huu sio utaratibu wa Uislam.
Kwani Mtume Muhammad (pbuh) alishatuonya juu ya uongo wa majini, anaweza kukwambia neno moja la ukweli halafu 99 yakawa ni ya uongo.
Mbaya zaidi ni kuwa sisi hatuwaoni ila wao wanatuona. Kuwaona kwao ni mpaka wachukue maumbile (form) ya wanadamu, mnyama kama vile paka mweusi, mbwa mweusi,nyoka, ng'e n.k
Pia majini haswa mashetani wa kijini hawakufanyii kazi bure pasi na kuingia nao mkataba wa kulipana, na malipo yao mengi ni ya kumkufuru Mungu, mfano atataka unapochinja usimtaje Mungu ila uchinje kwa jina la huyo jini, akushurutishe kuvaa vito flani,uvae nguo flani, kukuwekea miiko ya kula vyakul flani, au ufanye rituals kama kuwachomea udi na ubani...na kadiri wanavyokufanyia kazi ndivyo masharti yanavyozidi kuongezeka mpk kupelekea kuua au kumwaga damu za familia yako.