Hakika Maisha ya Binadamu Hayana Maana na Hakukuwa na Sababu ya Kuwepo Ulimwenguni

Hakika Maisha ya Binadamu Hayana Maana na Hakukuwa na Sababu ya Kuwepo Ulimwenguni

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
2,603
Reaction score
4,028
Katika historia yote ya mwanadamu, swali kuu limekuwa Kwa nini tupo hapa Ulimwenguni? Je, kuna maana yoyote ya maisha haya, au ni mwendelezo tu wa mzunguko wa kuzaliwa na kufa?

Kwa macho ya kawaida tu ni rahisi kusema kuwa maendeleo yote ya binadamu, teknolojia zote, elimu na falsafa zote, bado haziwezi kubadili ukweli wa msingi wa mwanadamu kwamba anazaliwa, anaishi kwa muda mfupi, kisha anapotea.

Mwanadamu Pamoja na "Maendeleo" Lakini Bado Mwisho ni Ule ule

Kila kizazi cha binadamu kimekuwa kikijitahidi kuondoa ukomo wa maisha. Wengine walitegemea dawa, wengine sayansi, wengine dini, na wengine teknolojia. Lakini licha ya jitihada zote, hakuna aliyewahi kuikwepa hatma.

Mwanadamu wa kale aliyeishi katika mapango alikufa. Mwanadamu wa sasa mwenye smartphone ya gharama na intaneti ya kasi naye atakufa. Na hata yule wa baadaye atakayemiliki akili bandia na safari za nyota bado hatamkwepa ndugu kifo.

Hii inadhihirisha kuwa maendeleo yote tunayojivunia, maandiko, miji mikubwa, na hiyo teknolijiaaaa ni kivuli cha muda tu. Hayabadili ukweli kuwa mwisho wa maisha ya ni kifo, kama alivyosema The Legend Himself Ramadhani Mtoro Ongala. Kwa hiyo, mtu akijaribu kutafuta maana ya maisha kupitia maendeleo haya, mwisho atabaki na shaka na utupu.

Teknolojia ni Mwanga wa Uongo

Teknolojia mara nyingi huchukuliwa kama suluhisho la changamoto za binadamu. Inatuahidi maisha bora, afya bora, na urefu wa maisha. Lakini tukifikiria kwa undani, teknolojia si kinga ya maana ya maisha. Ni chombo cha muda tu kinachoficha ukweli wa uhalisia. Ni biashara za wale wenye kutaka kunafaika na hofu za wenzao.

Mfano leo tuna simu zinazoweza kutuunganisha na ulimwengu mzima, lakini bado tunabaki peke yetu tukilala kitandani tukijua kwamba siku moja pumzi itakata. Tunaweza kwenda kwenye mwezi au sayari nyingine, lakini bado hatuwezi kutoroka kifo. Tunaweza kuunda mashine zenye akili kuliko zetu, lakini bado akili zetu hazijibu swali kuu kuwa kwa nini tupo Duniani?

Hivyo basi, maendeleo ya teknolojia ni kama kivuli cha taa kinachotuonyesha mwangaza wa muda mfupi, lakini nyuma ya mwangaza huo bado kuna giza lisilo na mwisho. Ni danganyatoo ya wachache wenye kutaka kuneemeka kwa yasiyo na faida kwa binadamu zaidi ya kumfanya mtumwa.

Kuzaliwa na Kufa ni Mzunguko Usio na Sababu

Hakuna mwanadamu aliyechagua kuzaliwa. Kila mmoja wetu alijikuta tu duniani, bila ridhaa, bila kupewa sababu. Kisha tunakulia katika dunia yenye matatizo, furaha, huzuni, na mamilioni ya vikwazo. Mwisho wa yote, bila kujali mtu alikuwa tajiri au maskini, msomi au mjinga, mwenye hadhi au mtumwa, wote huishia kwenye kaburi.

Ikiwa kweli maisha yana maana, basi angalau kufikia karne ya sasa, binadamu angekuwa amepata jibu jingine zaidi ya huu mzunguko. Lakini historia yote imetufundisha kitu kimoja tu: tumezaliwa ili kufa.

Hakuna Suluhisho la Hali ya Mwanadamu

Watu wengine hutafuta maana kupitia dini. Lakini dini zenyewe zimetofautiana sana kiasi cha kuibua mashaka badala ya majibu thabiti. Wengine hutafuta kupitia falsafa na tafakari, lakini falsafa zimebaki kuwa maneno matupu yasiyoweza kubadili ukweli wa kufa. Wengine hutafuta kupitia sayansi, lakini sayansi huonyesha zaidi jinsi tulivyo wadogo katika ulimwengu mpana kuliko kutoa maana ya kiuwepo chetu.

Kila njia ya mwanadamu ya kutafuta majibu huishia kwenye ukuta ule ule kwamba maisha hayana maana ya kudumu. Ni safari ya muda mfupi inayokoma ghafla, na hakuna anayejua "kwa nini."

Kwa mtazamo wa ukweli wa maisha, ni sahihi kusema kuwa Hakika maisha ya binadamu hayana maana na hakukuwa na sababu ya kuwepo ulimwenguni. Hatima yetu inabaki ile ile tangu mwanzo hadi leo kuwa siye ni wa kuzaliwa na kufa.

Maendeleo yote, teknolojia zote, maarifa yote, bado hayajatupeleka mbali zaidi ya hapo. Tunabaki katika fumbo lisilo na jibu, na hivyo basi, maisha ya binadamu hubaki kama kivuli cha ndoto isiyo na maana, inayotoweka kabla hatujaielewa.
 
Maana ya maisha binadamu anaitengeneza peke yake .
 
Mkuu hebu nisaidie kujibu swali hili unadhani maisha yangekua vp ndio yangekua na maana kwa binadamu
 
Niliwahi kusema humu kwamba tatizo letu binadamu tunajipa umuhimu ambao hatuna.

Binadamu sisi ni wanyama kama wanyama wengine waliopo hapa duniani. Tupo hapa kuishi, kuzaliana na kufa, full stop. Hivi viakili kidogo tulivyopewa ni vya kutusaidia saidia tuweze ku survive hasa ukizingatia sisi hatuna protection yoyote against nature kama wanyama wengine.
 
Kuzaliwa na kufa ndiyo mfumo mzima wa maisha.ingekuwa ni kuishi MILELE ingekuwa Dunia imejaa na hakuna pa kukanyaga.
 
Ndio maana kuna mwanajeshi mmoja kule marekani aliandika kitabu kinaitwa "MAN SEARCH FOR MEANING "
 
1. Mitazamo ya Ujamaa na Dini

Dini nyingi huona kuwa maisha yana maana kwa sababu tumeumbwa kwa kusudi—kama kumwabudu Mungu, kueneza mema, au kufuata maagizo ya kiroho.

Wengine huamini maisha ni zawadi na kila mmoja anatakiwa kuitumia kuleta mwanga kwa wengine.



2. Mitazamo ya Falsafa (Utafsiri wa Kibinadamu)

Existentialists (kama Jean-Paul Sartre na Albert Camus) husema kuwa maisha kiasili hayana maana iliyojengwa ndani yake, lakini binadamu ana uhuru wa kuipa maana kupitia matendo, uhusiano, na maamuzi yake.

Camus aliita hili “absurd”—ukweli kuwa tunatafuta maana katika ulimwengu usio na maana ya kiasili—lakini bado alisisitiza kuishi na kuunda maana yetu wenyewe.



3. Mitazamo ya Kisayansi

Kihalisia, kimaumbile, sisi ni matokeo ya mageuzi na michakato ya kiasili bila “sababu” iliyoamuliwa mapema.

Lakini ndani ya huo muktadha, binadamu huunda sababu ya kuishi kupitia uhusiano, upendo, ugunduzi, na ubunifu.



4. Maisha ya Kila Siku

Hata kama hakuna “sababu kuu ya ulimwengu,” tunapata maana kupitia familia, marafiki, ndoto, kazi, au hata furaha ndogo ndogo (kama muziki, sanaa, au kusaidia wengine).




Kwa hiyo, ni kweli unaweza kuona maisha hayana maana ya asili. Lakini bado tuna nguvu ya kuyapa maana kupitia jinsi tunavyoishi
 
Back
Top Bottom