Hakika Lowassa ni Liability CHADEMA!!

Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,854
1,776
Watu wenye upeo mdogo wanaangalia vihesabu vya nyongeza ya Wabunge na Madiwani CDM katika Uchaguzi wa Mwaka 2015. Wanasahau kwamba kutokana na upepo wa Kisiasa ulivyokuwa watu walitaka mabadiliko hata kama angesimama DR. SLAA wangepata viti vingi zaidi. Tena vingi zaidi kwa sabau CCM wasingepunguza kura za CDM kwa ajenda ya UFISADI ambayo kwa DR. SLAA isingetajwa.

Ukiangalia upande wa pili, matokeo ya Uchaguzi mwaka 2015 ni muunganiko wa nguvu za vyama vinne sio kimoja kama ilivyokuwa mwaka 2010. CDM ilipata kura za CUF, NLD na NCCR na siyo CDM pekee na hili halina ubishi.

Ukitoa kura za CUF, NLD, na NCCR say 1,000,000 utapata hesabu ya kura 2,400,000ndizo kura alizoongeza LOWASSA kwa kunufaika na Muungano wa UKAWA wakati CCM imeongeza kura 3,000,000 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2010.

Naweza kusema bila woga kwamba kilichosaidia wapinzani kupata kura nyingi ni vijana kuichukia CCM na wangeweza kumpigia yeyote hata kama angesimamishwa DR SLAA na tena huyo ndio angepata kura nyingi zaidi kuliko inavyodhaniwa. HIVYO ASIJIDANGANYE MTU KUSEMA LOWASSA NI ASSET. HAKUNA. NI LIABILITY PERIOD!!!
 
Asset ni DR SLAA ambaye Mbowe amemtosa kwa tamaa yake. Mtamkumbuka sana na matokeo ya SM 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 mtajuta sana!!
 
pamoja na kura kuchakachuliwa lowassa alikuwa na kura zaidi ya mil 6 ,,,mnataka nini zaidi.

najua umeongea kwa kuongozwa na mihemko bla kujali uhalisia.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom