VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Ukimtazama na kumsikiliza Edward Ngoyai Lowassa unaweza kunibishia. Ukimtazama na kumsikiliza tena Lowassa utaniamini. Ukimtazama na kumsikiliza Lowassa kwa mara ya tatu, hutatamani kumtazama na hata kumsikiliza mara nyingine. Ni msanii kwelikweli. Lowassa anajipambanua kama dawa ya umaskini wa Tanzania. Ameshindwa vibaya kuuondoa umaskini wa Monduli tu aliyoiongoza kwa miaka 25 kama Mbunge.
Lowassa anapokaririwa akisema kuwa ndani ya CC na NEC hakuna wa kukata jina lake unaweza kumuamini. Anajichora kama mpambanaji na shujaa hasa. Anajichora kama mwenye misuli imara chamani na asiyezuilika. Mtazame tena Lowassa na utabadili mtazamo wako. Lowassa amejaa woga na kutojiamini. Ndiyo maana anashtukiashtukia. Anacheza filamu ya takwimu wakati wenzake wamesharejesha fomu na fomu zimeanza kuchambuliwa! Ameshindwa mapema.
Kulipokuwa na fukuto la ufisadi katika Jengo jipya la UVCCM, Lowassa aliingia kwenye mpambano na Nape Nnauye. Lowassa akiwa Waziri Mwandamizi Serikalini na mmoja wa wanabodi ya Udhamini ya UVCCM,Nape alikuwa kijana mdogo na mchanga ndani ya UVCCM. Nape alimpeleka puta Lowassa na kumlaza macho. Lowassa, kwa sisi wachambuzi,alishindwa na Nape.
Mwaka 2008, Lowassa aliingia tena ulingoni kupambana na Dr.Harrison Mwakyembe akiwa na Kamati yake teule ya Richmond. Hapa Lowassa alipigwa KO na kuishia kulalama na kulialia kutafuta huruma. Akasingizia kuwa Uwaziri Mkuu ndiyo uliolengwa. Angekuwa mpambanaji angepambana. Hata PM Pinda anamzidi. Pinda amebaki imara pamoja na Operesheni Tokomeza, Operesheni Kimbunga na Escrow.
Kwenye uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki (baada ya kifo cha Hayati Jeremiah Sumari), Lowassa alipanda tena ulingoni. Safari hii alikuwa kichama zaidi. Aliongoza kampeni za mgombea wa CCM na pia ni mkwewe, Sioyi Sumari. Akiwa katika uwanja wa nyumbani-karibu kabisa na Monduli, Lowassa aligaragazwa na kijana wa miaka 25 toka CHADEMA,Joshua Nassari aka Dogo Janja.
Sitaki kutaja kushindwa kwake kununua mvua za kutengeneza Thailand na hata Shule za Kata. Nataka mumtazame na kumsikiliza tena Lowassa halafu mshuhudie usanii wa mtangaza nia huyu. Chamani, Lowassa ni mwepesi na ameshazoea kushindwa. Hana upekee wowote na atayapokea matokeo yoyote Julai 12.
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.
Hakika una tatizo la kimsingi.
Your principles in life and society are way below admirable standards.
Kuna uzi humu kuwa EL amefisadi hadi kanisani.
Mtu mwizi, fisadi, mwongo hawezi kuwa nguzo mahali popote katka jamii zilizostaarabika.
Pengine huko kwenu kwenye jamii ya wezi.
Hakika una tatizo la kimsingi.
Your principles in life and society are way below admirable standards.
Kuna uzi humu kuwa EL amefisadi hadi kanisani.
Mtu mwizi, fisadi, mwongo hawezi kuwa nguzo mahali popote katka jamii zilizostaarabika.
Pengine huko kwenu kwenye jamii ya wezi.
Ukiwa muongo usiwe msahaulifu. Hapa ulisema nini?
Wewe jamaa ni laghai sana.
Hivi hapo kwenye ofisi za bavicha hamchoki kulaghai wananchi?
Mkuu huyu atoona na lile la pili litapata chongo awe kipofu jumla maana ni mgumu kuamini kumpita Tomaso .Wewe huenda ukawa ni kama yule askari aliyekuwa na chongo aliyemuchoma.Masii mkuki ubavuni maji na damu vikatoka,ndipo maji yakaruka mpaka kwenye jicho lile lenye chongo akapata kuona tena ndipo akakiri kuwa hakika huyu ni mwana wa Mungu.
Nitajie malaika aliyekuwa akakubalika. Pamoja na changamoto zote mitume na manabii walipata misukosuko hasa ya kukataliwa. Lowasa kakatwa na CCM. Lakini hajakataliwa na wapiga kura
Mwizi, fisadi na mwongo hajatubu na kurudisha mali kwa masikini.Wewe huenda ukawa ni kama yule askari aliyekuwa na chongo aliyemuchoma.Masii mkuki ubavuni maji na damu vikatoka,ndipo maji yakaruka mpaka kwenye jicho lile lenye chongo akapata kuona tena ndipo akakiri kuwa hakika huyu ni mwana wa Mungu.
Ingawa sisomisomi biblia kila mara,nina mistari naijua. Najua kuna mistari inayosimulia jinsi wayaudi walivyokuwa hawamkubali Yesu na kumuona wa kawaida,tapeli na mbabaishaji. Wapo ambao hawakumkubali kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Hata siku Yesu,saa saba mchana,alipokufa msalabani,askari waliokuwa lindo kwenye misalaba walikosulubiwa Yesu na majambazi wawili walikiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Walisema: hakika huyu alikuwa ni Mwana wa Mungu!
Hapo ni baada ya giza kuifunika nchi na hata pazia la hekalu kuraruka katikati wakati Yesu akikata roho msalabani. Ndicho kinachotokea kwa mwanasiasa Edward Lowassa. Lowassa anaivuruga CCM. Anaichachafya. Haili na kulala kwa raha.
Kwa matendo na maneno yake pamoja na fukuto linaloendelea ndani ya CCM,Lowassa alikuwa nguzo chamani. Alikuwa ni mwenye ushawishi na kukubalika. Ameshajihakikishia kura kwa maelfu toka kwa makada wa CCM ambao wanamkubali. Wale walio CCM kimwili tu. Wengi tu.
Lakini,CCM itapambana naye hadi mwisho wa uchaguzi huu. Mpira ni dakika 90!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Mtu tangu awe bungeni hajawahi kutoa mchango hata mmoja zaidi ya kuvizia kuiba kwa ufisadi wake halafu unasema alikuwa nguzo kama kwa ufisadi hapo nakubali.Well. Umelink vema sana. Hongera hakika lowassa ndio rais ajaye
Kwisha habari yake akafanye kazi zake za ufisadi tu.Jiwe la kujengea Tanzania mpya walilolikataa ccm sasa wameanza kuona thamani yake likiwa kwenye msingi wa mabadiliko :A S 41:
Mwizi, fisadi na mwongo hajatubu na kurudisha mali kwa masikini.
Lowasa wenzake ni mafisadi wenzake hakuna mpiga kura ambaye yupo na fisadi Lowasa.Nitajie malaika aliyekuwa akakubalika. Pamoja na changamoto zote mitume na manabii walipata misukosuko hasa ya kukataliwa. Lowasa kakatwa na CCM. Lakini hajakataliwa na wapiga kura
Lowasa ndiyo alikuwa fisadi nadani ya ccm pamoja na wenzake aliotoka nao kwenda kwa majambazi wenzake.NA CCM mbona haijatubu wizi ufisadi na uongo. Kelele zote ni hofu ya kuumbuliwa mazongezonge yenu ya kutawala kwa hila .