Haki za mteja endapo benki itafilisika

Haki za mteja endapo benki itafilisika

*anaandika mtaalamu wa masuala ya Benki na sheria.*

Benki inapokua inafilisiwa, *Deposit Insurance Board* (DIB) ambayo ipo kwa mujibu wa *kifungu cha 36* na *37* cha *Sheria Na. 5* ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya *mwaka 2006*, hufanya utaratibu wa kuwalipa wateja amana zao.

Members wa bodi hiyo ni Gavana wa BOT (chairman), Makatibu Wakuu wa Hazina wa Tanzania Bara na Visiwani, na Wajumbe wengine watatu ambao huteuliwa na Waziri wa fedha ambao ni wajuzi na wabobezi ktk masuala ya kibiashara, utaalamu au taaluma na wenye tabia na mwenendo mzuri na uzoefu ktk sekta ya zinazohusiana.

Bodi hutoa malipo ya awali kwa wateja wote ambayo kiwango cha kuanzia huwa Tsh milioni moja na nusu. Hii ni kwa mujibu wa *tangazo la serikali Na. 198 la mwaka 2010*.

Kwa wateja ambao kiwango cha amana zao wakati wa ufilisi ni chini ya na *hakizidi 1.5m* hao watalipwa amana zao zote kulingana na kiasi walichokuwa wameweka.
Kwa wateja ambao kiwango cha *amana zao kitakuwa kimezidi 1.5m* hawa kwanza *watapokea hiyo 1.5m kama malipo ya awali* kisha kiasi kilichobakia watalipwa baada ya mali zote za benki kuthaminishwa na kufilisiwa. Ni wajibu wa yeyote anayeidai benki inayofilisika kuwasilisha *maombi ya madai ukiambatanisha ushahidi wa nyaraka* kwa hiyo bodi
ili fedha ziweze kulipwa kutoka kwenye *"protected deposit"* ya bodi ambayo vyanzo vyake vya fedha hutokana na michango ya kila mwaka kutoka kwenye hayo mabenki nk.

Ikifikia hatua ya liquidation na kuteuliwa kwa mfilisi bodi itachukua au kupokea kiwango kilichozidi kutoka kny assets za benki kilichofidiwa kwa depositors. Hii kiutaalamu tunaiita *"subrogation right"*.


*#* Hivyo kiwango cha 1.5m ni kiwango cha awali na *sio* kiwango cha mwisho,baada ya kulipwa 1.5m ,unaandika maombi ya madai ukiambatanisha nyaraka zote kwa board ambapo utalipwa pesa zako zote kupitia *protected deposits*.
 
Mm natunza ndani Naogopa kuweka bank maana wanadhulumu
 
Kuna wasiwasi nikaanza kufukia amana zangu kidogo kidogo huu utaratibu sio mzuri kabisa....1.5m wakati nina 10m hapanaa asee
 
Kumekuwa na taarifa zisizo rasmi kwamba hali ya taasisi zetu za kifedha sio nzuri, nakuchangia baadhi ya taasisi zisizo fanya vizuri kufungwa na serikali bila kutoa maelezo ya kina juu ya fedha za wananchi zilizowekwa kwenye taasisi hizo. Hofu yangu ni kuhusu usalama wa fedha zetu kwenye benki hizi zingine, Je uko salama? Itakuwaje siku ukisikia benki nyingine zimefungiwa?

Kuweni makini msitegemee sana hizi taasisi, siku utakuja lia, mimi kwasasa siweki tena fedha benki mpaka awamu hii ya tano itakapotoka madarakani.
 
Mkuu vipi ulikuwa na akiba ya fedha Ephata benki?
 
Zile hazikifikisha huo mtaji wa bilioni 5 ndiocmaana zilifungwa, si kwamba zilifilisika.
 
Kumekuwa na taarifa zisizo rasmi kwamba hali ya taasisi zetu za kifedha sio nzuri, nakuchangia baadhi ya taasisi zisizo fanya vizuri kufungwa na serikali bila kutoa maelezo ya kina juu ya fedha za wananchi zilizowekwa kwenye taasisi hizo. Hofu yangu ni kuhusu usalama wa fedha zetu kwenye benki hizi zingine, Je uko salama? Itakuwaje siku ukisikia benki nyingine zimefungiwa?

Kuweni makini msitegemee sana hizi taasisi, siku utakuja lia, mimi kwasasa siweki tena fedha benki mpaka awamu hii ya tano itakapotoka madarakani.
Bank za nje kama KCB,Exim,Nk ziko Salama wakifilisika unaenda main branch kwenye nchi zao unachukua hela yako hizi Saccoss bank ikifilisika ndo mazima kilio.
 
Hata siye tulio na pesa benki ya HBC tujiangalie , jamaa kama vile hawana mzigo.
 
Kwa nini waliruhusiwa kufanya biashara ilhali hawana mtaji unaotakiwa na BOT? Wanacheza na pesa za watanzania.
Sheria ilikuja kubadilika wakati benki zimeshapewa kibali, mwanzo ilikuwa 200mil, baadae wakabadili hadi billion 5, na wakapewa miaka mi5 kukuza mtaji hadi bil5 lakini wakashindwa
 
Kama hawakufirisika mbona gavana wa Bank kuu aliwambia wenye amana zaidi ya 1.5m watalipwa kiwango kisichozidi 1.5m?
Bank huwa hawakai tu na pesa kama mayai, huwa wanazikopesha, sasa unapoifungia ghafla inabidi kwanza ulipwe 1.5m then madeni yakiiva na kukusanywa mnalipwa zilizobaki.
 
Hujatuambia kama Bank haina chakupigwa mnada labda benki kama hizo za vijijin ambazo hazina mali nini kitauzwa
 
Back
Top Bottom