Haki ya mpiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki ya mpiga kura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chovek, Apr 13, 2012.

 1. c

  chovek New Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wa uchaguzi, mpiga kura anapewa karatasi ya kupiga kura yenye majina na picha za wagombea kadhaa. Mpiga kura anatakiwa aweke alama ya vyema (√) chini ya picha ya mgombea anayempenda.
  Swali langu: Ikiwa mimi sijaridhika na mgombea yeyote kati yao, nifanyeje? Naamini pia nina haki ya kutomchagua mgombea yeyote. ZEC na NEC haitoi haki kwa mpiga kura katika uchaguzi kujieleza haki yake ya kuwakataa wagombea wote.

  Napendekeza kuwepo kwa kisanduku katika karatasi ya uchaguzi bila picha wala jina la mtu yeyote ili niweze kuiwekea alama ya vyema. Yaani, kuwe na “kivuli” kama wakati wa mfumo wa chama kimoja.

  Ikiwa “Kivuli” kitashinda, basi uchaguzi urudiwe na wagombea wote wawe wengine wapya. Au

  1. mgombea atakayeshinda ashike nafasi aliyogombea kwa kipindi cha chini ya miaka mitano. Baadaye, uchaguzi mwengine wa uitishwe na mshindi atashika nafasi hiyo kwa miaka mitano bila kujali uchaguzi mkuu wa taifa.
  2. nafasi hiyo ishikwe na wagombea wawili, i.e mshindi wa kwanza na wa pili, kwa vipindi viwili tofauti, kila urefu wa kipindi kwa mujibu wa asilimia alizoshinda.
  3. wagombea binafsi waruhusiwe.
   
Loading...