Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,196
- 7,532
Hivi hakuna maandamano yeyote yaliyopangwa kufanyika mwezi ujao ili tuhudhurie maana naona mwezi huu kimyaaa! Any way natania tu wakubwa.
Leo tutafakari kidogo haki ya maandamano.
Ninavyofahamu mimi ni kuwa; haki yeyote ile ya mtu, huishia pale haki ya mtu mwingine inapoanzia. Unaweza kukosoa au kutukana hapa ukipenda.
Sasa hebu fikiria "Scenerios" zifuatazo:
1.Unarudi kazini usiku saa mbili umechokaaaa! karibu na nyumba yako kuna mtu anauza pombe, kafungulia mziki kwa sauti kubwaaaaa, halafu ukimwambia apunguze au audhibiti usisambae ili uweze kulala, anakuambia anachokifanya ni haki yake, halafu anaendelea mpaka saa nane usiku.Unajisikia je? je! unadhhani ni sawa? unajifunza nini kwa haraka?
2. Mwanao anaumwa sana, anaonekana anashindwa kupumua, umeshauriwa kumuwahisha hospitali maeneo ya mjini, umekopa hela umekodi taxi kumkimbiza, unafika njiani unakuta njia haipitiki, unauliza kuna shida ganilunaambiwa mbele kuna maandamano, mwanao anapoteza maisha.Unajisikia je! unatafsiri je dhana ya haki za watu?
3. Umechukua ka-mkopo benki baada ya kuomba ajira kwa miaka mitano bila mafanikio.Umeanza kuuza vinjwaji barabarani.siku moja watu wanavamia kakibanda kako wanakunywa vinjwaji vyote kwa hoja ya kuwa yalikuwa ni maandamano. Utatafsirije kinachoitwa haki ya kuandamana?
Nadhani kwa scenerio hizi chache sasa naweza kuuliza swali la msingi.Hivi ikiwa lengo la maandamano ni kufikisha ujumbe kwa watu fulani, hakuna njia nyingine inayoweza kutumika na ikafikisha ujumbe bila kuleta madhara kwa watu wengine ili haki ya mtu mmoja isiwe kizuizi na kikwazo kwa haki za wengine, au haki za kundi fulani zisiwe kikwazo cha haki za wengine?

KARIBUNI;