Haki ya kuchagua na kuchaguliwa

Banner

Member
Oct 6, 2011
5
2
Nijuavyo mimi kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya mungano wa Tanzania,ni haki ya msingi ya MTANZANI ailefikisha miaka 18 kushiriki katika chaguzi za udiwani na ubunge,kugombea,kuchagua au kuchaguliwa.

Hilo hata baba wa TAIFA MWL JK NYERERE aliliona na aliwahi litolea tamko katika sherehe za may mosi zilizo fanyika kitaifa mkoa wa Mbeya mwaka 1995 yeye akiwa mwalikwa kama mgeni wa heshima na mie pia nakumbuka nilikua mmojawapo kati ya WATANZANIA tuliohudhulia sherehe hizo.Na alitoa mfano wa jinsi gani mgombea binafsi anavyokua na nguvu ya uma alipokwenda kumnadi chifu waliomteua chama(TANU) na chama kikiwa na uhakika walie mteua ni msafi lakini akajitokeza kijana ambaye pia alikua mwana chama wa TANU akagombea kama mgombea binafsi na AKAWASHINDA,pamoja na MWL JK NYERERE kwenda kushawishi wananchi wamchague chiefu na hasa ukitilia maanani mzee wetu wote twa mjua katika swala la ushawishi mwenyezi mungu alimjalia,Dunia nzima walimjua kwamba yupo juu katika ushawishi hata mataifa tunayosema ni makubwa kwa BABA WA TAIFA alikua kiboko yao.Lakini alikwama kuwashawishi wananchi wamchague chifu badala yake walimkataa chifu na wakamchagua kijana aliegombea kama mgombea binafsi.

Yasemekana katika uchaguzi uliofanyika nchini ZAMBIA viti vingi vimenyakuliwa na wagombea binafsi hii ni kuashiria watu wamechoshwa na mambo ya vyama maana ndani ya chama nilazima ukubaliane na sela za chama hata kama zinakasolo ukipinga utaishia kufukuzwa chama na kiti ulicho gombea ukakipoteza au wakati wa kura zamaoni jina lako wakalichinjia baharini mfano hiyo ni mingi na tumeishudia si kwa cha kimoja ni vingi.

Sasa katika kumuenzi BABA YETU WA TAIFA na miaka 50 ya UHURU ninani anaetumia nguvu nyingi kutunyima haki hii ya kua na mgombea binafsi bila ya hata woga wa mzee wetu na kwa sababu zipi na akiwa na maana gani?au akiwa na kusudio gani katika Nchi yetu?

Wadau naomba mniambie labda kunasababu zimejificha mie sizielewi na ni nzito labda zina msingi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom