Haji Manara vs Shafii Dauda Nyuma ya Pazia

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
16,513
2,000
Manara: Umeonaje ila formula niliyokwambia, si unaiona imetiki, Instagram yote tunazungumziwa sisi tu.

Shafii: Daah! Ila kweli kabisa. Unajua ulivyoniambia tupige kiki kwa staili ile nilidhani watu wangeshtukia...ila daah! Wameingia wazima wazima kama mbuzi

Manara: Mimi si ndiyo mzee wa kuwachachafya. Unajua wewe haupo karibu na wanamuziki, ila Platnumz, Konde wote wanatumia njia hii, mnaichangamsha Instagram, watu wanawazungumzia kumbe nyuma ya pazia mko poa tu

Shafii: Aisee nimeamini sasa hivi. Kwa hiyo mpango unaokuja tunausuka vipi ili watu watujadili kama kawaida yetu?

Manara: Ngoja tukishacheza mechi yetu nitakwambia. Ila nitajifanya naifufua ishu ya Utopolo, halafu wewe utaingilia kama kuwatetea, mashabiki wa Uto watanijia juu, halafu wa Simba watanitetea.

Shafii: Sasa na mimi nikijiwa juu na mashabiki wa Mnyama?

Manara: Wa Utopolo watakutetea.

Shafii: Poa..ila unavyonipiga kwa suala la jezi, hizi ng'ombe zitafikiri kweli niliomba dili la kutengeneza jezi.

Manara: Sasa si ndiyo promo yenyewe, Mondi ilisemekana kanunua private jet, kwani kanunua kweli?

Shafii: Dah! Aya bhana. Ila ongea na Edo asiingilie sana hii ishu.

Manara: Yule dogo kashaona hapa kuna kiki kubwa ndiyo maana naye anaiingilia. Yaani kupitia hii, followers utawapata na madili yatakuja. Wewe vumilia madongo yangu tu

NB: Maneno ya kupachikwa kiutani.

Source: Copy & Paste.
IMG-20210514-WA0055.jpg
 
mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,644

Source: Copy & Paste. View attachment 1784931
Umejitahidi Ubunifu na kuna mataga yatakayoamini ulichokiandika hapa!! Ila ni ubunifu mbaya maana unawachonganisha watu wote dhidi ya Manara na Shafii. Hili andiko ni la kupuuza!
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
24,085
2,000
Nchi ya aina yake

Mchambuzi wa Michezo na Msemaji wa Club ni maarufu kuliko Ma Straker wenyewe wanaopambana Uwanjani!

Siasa ya Mpira imekuwa na Mashabiki kuliko Mpira wenyewe!
 
Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
16,513
2,000
Salaam

Nimeamua kuandika ujumbe huu mfupi kwenu baada ya picha yangu na Shaffih Dauda kuzagaa mitandaoni jana ikionyesha tupo Johannesburg tukila pamoja chakula !!

Wengi wa washabiki wakinilaumu kwa nn nimekubali kukaa meza moja na mtu anaenituhumu mara kwa mara na kuisema Simba vibaya na wengine kumlaumu Shaffih kwa nn kakaa na mm ilhali nimemwita takataka ?

Narudia kusema kwamba neno hilo nililitamka ktk Group ya Watsapp ambapo kulikuwa na ubishani mkali kuhusu Game ya Simba na Yanga ambapo ktk group hilo kuna wachambuzi na wadau wengine wa soka ,,,,sikumkusudia yoyote nje ya group letu na hata niliowakusudia wenyew hawawezi kulalamika,coz kuna mengi yalisemwa kwangu ktk mjadala ule,,

Bahati mbaya clip yangu ikavujishwa kusudi na baadhi ya watu wakaichukua na kuruka nayo mitandaoni ,akiwemo Shaffih ambae kiukweli alikosea kuipa tafsiri yake kwamba nimewatukana Wachambuzi na Waandishi wa michezo ,,,

Jana Eddo kumwembe na Oscar Oscar waliponita Mandela Square hapa Jozi tukisubiria muda wa kwenda mazoezini jioni,,ndipo nilipomkuta Shaffih,,,,

Kiukweli kabla ya jambo lolote nilimwambia umenikosea sana na kumwambia ukweli wake mbele ya kina Eddo na mbele ya rafiki zake wengine anaofanya nao kazi Clouds akiwemo kijana wake Privadinho,,,

Uzuri hakubisha na akasema yy hakujua kuwa nimeongelea ktk group la Watsapp,,nikamsisitiza anazo namba zangu na tunaongea mara kwa mara,,why hakuniuliza kwanza ?

Lakini baada ya kusema ya moyoni na kutoa dukuduku langu ,,kama Mwanamme kwa nn niendelee na ugomvi ukizingatia nasaha kwetu zilizotolewa na ndugu zetu tuliokuwa nao kipindi hcho ?

Nakumbuka Oscar alisema nyie ni Waislaam na mmetoka kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu why muendeleze malumbano ?

Sikutegemea busara ya rafiki yangu yule ‘mnywaji ‘ but he was right na kibinadaam nikaona niyamalize na hasa baada ya wote kuusiana kuishi kwa wema na kila mmoja aheshimu kazi ya mwingine !!

Ni kweli Simba inaihitaji sana media lakini Media pia inaihitaji sana Simba na mm ndio source ya taarifa za Simba ,,,

C vyema kuandika jambo hili ukizingatia lishaisha ,,but imebidi kwa kuwa washabiki hususan waliomini nipo sahihi kuanza kunilaumu ,,,,

Wanaonijua mm nna sifa mbili nzuri na mbaya wakati mwingine,,

Sina hofu ya kumwambia mtu yoyote kitu nnachokiona hakipo sawa iwe kwangu binafsi au cha klabu yangu,,na siku hz naweza kustahmili mashambulizi binafsi zaidi kuliko ya Simba,,

Pili sina nongwa na nasamehe na kusahau jambo haraka sana,,,nadhani hili nalifanya kwa misingi ya kidini na kiutu zaidi,,na kwa nn nafanya hv,,,ni hofu ya Mungu,,tunamkosea Mungu kila siku na kwake tutahitaji msamaha,,so lazma tusameheane na cc tunapokoseana !!

Watu wangu nieleweni siwezi kuwa snich kwenu na mmeonyesha kustand na mm kwa hoja lakini kwa maslahi ya kiutu,kidini na mpira wetu lazma maisha yaendelee na hatutarajii kuona malumbano yakiendelea !!

Hope mtanielewa na sasa tujikite na mijadala yetu adhimu ya game yetu ya leo

Na inshaallah jema laja usiku wa leo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom