Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara amelipa mtihani Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuahidi kufanya maamuzi ya kumtolea posa Wema Sepetu endapo ratiba ya ligi kuu haitabadilishwa hadi mwisho wa msimu.
Aidha msemaji amedai kama muigizaji huyo atakataa basi atatembea akiwa amevaa nguo ya ndani pekee (Boxer) kutoka nyumbani kwake hadi katika ofisi za TFF zilizoko Ilala Dar es Salaam.
Kupitia taarifa ambayo ameichapisha kupitia mtandao wa facebook, ameonyesha kuchukuzwa na kitendo cha TFF kubadilisha ratiba ya Lig Kuu mara kwa mara.
“Nimalizie Kwa kuwapa mtihani mwingine TFF na bodi ya Ligi, iwapo Kama ratiba yao ya Ligi kuu na Kombe la shirikisho haitabadilishwa kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu, ntamposa mlimbwende Wema Sepetu, na akikubali ntamuoa, akikataa ntatembea na boxer toka Nyumbani kwangu hadi TFF” Amesema Manara
Hatua hii ya Haji imekuja ikiwa ni saa chache baada ya Bodi ya Ligi kusogeza mbele mchezo kati ya Simba na Yanga uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 18, mwaka huu na sasa utachezwa Februari 25 mwaka huu.
Hatua hiyo ya Bodi ya Ligi imekuja kama kutimiza kile ambacho Manara alikiahidi awali mwanzoni mwa msimu, ambapo alisema kuwa angetembea akiwa mtupu endapo ratiba ya ligi isingebadilishwa.
Katika tamko lake la sasa kupitia ukurasa wake wa Facebook, Manara ameeleza kusikitishwa kwake na kile alichokiita ubabaishaji katika upangaji ratiba, na kulitaja suala hilo kuwa ni moja ya sababu ya Tanzania kukwama katika soka.
“Ninajiuliza iwapo ratiba ya Ligi yetu ni muhali kuipanga,vipi kuhusu program nyingine za maendeleo? Itakuwaje kuhusu timu yetu ya taifa juu ya ndoto zetu za mchana wa jua kali? vipi kuhusiana na zile programu hewa za soka la vijana, watoto na wanawake?”
Ameendelea kusema “Hakika kwetu hayo ni sawa na bahari ya Mediterranean au bahari kuu ya hadithi za Alfu Leila uleila, hatuwezi ratiba tutaweza kwenda Afcon 2019? hatuwezi kupanga ratiba tutaweza kuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza mchezo huu ambao yatajwa watu bilioni tatu duniani kote wanaushabikia?”