Hajafunga ndoa na mumewe na mumewe anafunga, atafanyaje wasifanye mapenzi?

Neema j swai

Senior Member
Mar 27, 2017
177
103
Wazima jamani,

Naombeni ushauri,

Nina rafiki yangu anaishi na mpenzi wake Mslamu na yeye ni Mkristo ila hawajafunga ndoa wala limekuja Ramadhan hii mwanaume kafunga kamwambia mpenzi wake asimguse ukifika mda wa kulala ni kulala hairusiwi kufanya mapenzi kipindi hichi kama hawajaoana ila ftari anapika huyo mwanamke ambaye hajaolewa.

Swali linakuja je atafanyaje ili aweze kuvumilia mpaka Ramadhan ishe bila kugusana maana wanaishi chumba kimoja na mwanaume amefunga.

Msaada maana hapo kazi ipo.
 
Kiimani ninavyojua huyo mwanamke haruhusiwi kupika futari!!
Mwenzie yupo kwa toba yeye je?
BTW sku 30 siyo nyingi mbona!!alale chini
 
Avumilie tu ni kipindi cha mpito ikiwezekana arudi kwao ampe nafasi mwenzake
 
Kwanza inabid watengane chumba...yan kila mmoja aishi chumba chake(kama wanapoish wana iyo option),pia ftari hatakiwi apike uyo mwanamke napia ela yaftar haiakiwi atoe uyo mwanamke
 
Sio kwenye Ramadan tu. Uzinzi ni thambi kwanini wasifunge ndoa ya fasta waishe kwa raha. Inamaana anafunga kwajili ya Ramadhani na si kwa Mnyezi mungu.
 
I see mwambie huyo shemeji yako ale tu hakuna haja ya yeye kujishindisha njaa,anachokifanya ni kinyume na matakwa ya dini ya kiislamu na dini nyingine yeyote ;kuishi na mwanamke unayemuita mke bila ndoa!? Alafu anakupikia iftari !! Kwani wenzie hawaoni wanaooa mke uji japo hairuhusiwi ila angalau hata machoni pa wanaadamu
 
Inabd nipate mda wa kukaa na Shem nimpe somo ikishndkana kutafuta ustaarabu mwingne wa kutengana chumba kpnd hiki inabd fimbo itumike kuwatawanya maana nliwambia hairusiwi mnavyofanya nkamwambia na mshkaj ni bora tu apoteze mwaka huu acfunge na afanye utaratbu Wa ndoa ili mfungo mwingne ndoafunge ila kagoma amefunga bt namwonea Huruma sana coz najua anakosea
 
Nahisi niwewe ila dadayangu uwetyari kubadilisha dini cz wanajifanyaga wameokoka wakisha kuoa wanarudi nyumban kumenoga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom