Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Mapema mwaka 2015 Gwajima akiwa katika jukwaa la siasa pamoja na Dk Slaa alisema kuwa Dk Slaa ndiye Joshua atakayeivusha Tanzania kwenda nchi ya ahadi.(Kaanani)
Alipotabiri hivi, juu ya Dk Slaa na kuutangazia umma, CHADEMA walimshangilia, na waliuunga mkono ule unabii. Huku kwenye mitandao Dk Slaa akaanza kuvuma kwa lakabu mpya, si nyingine Joshua Mwana wa Nuni.
Hata waumini wake pia, bila kujali vyama vyao, walimuunga mkono askofu wao, kwasababu askofu haneni kwa tamaa yake bali hunena kwa maelekezo ya kinabii toka kwa Mungu.
Mwaka huohuo, Lowassa alipotangaza nia kwenye uwanja Amri Abeid Arusha, Gwajima pia kwenye jukwaa la siasa aliwatangazia kanisa lake na watanzania kuwa, Lowassa ndiye Joshua atakayevusha Tanzania kwenda nchi ya ahadi.
Kwa tangazo lile juu ya Lowassa, CHADEMA walimpinga na walisema kuwa Gwajima kahongwa na anatumia vibaya neno la mungu.
Hapa pia waumini wake waliendelea kumuunga mkono, bila hata kujiuliza ni Mungu yupi aliyemwambia Gwajima kuwa Dk Slaa ni Joshua na ni Mungu yupi aliyemwambia Gwajima huyohuyo kuwa Lowassa ni Joshua. Ama ni Joshua yupi ambaye ni Lowassa na ni Joshua yupi ambaye ni Dk Slaa.
Wenye akili, wanaojua utapeli wa hawa watu wanojiiita wachungaji, manabii na mitume waliigundua kuwa mwaka wa uchaguzi ni mwaka wa fursa kwa wapiga ramli, wachungaji, bodaboda, mama na baba lishe, na kwa vyovyote vile mchungaji tapeli hawezi kuiwacha fursa hiyo kuitumia.
Sivyo tu, baada ya Lowassa kuingia CHADEMA na UKAWA, kuna mambo pia yalitokea na mambo hayo yote yanathibitisha ujinga, unyumbu na ufinyu wa kufikiri wa waumini wa kanisa la Gwajima na wanachama wa CHADEMA.
Sote mashahidi, tukaona jinsi Gwajima alivyoamua kumshambulia mtu aliye mtabiria urais kwa kumuita jina la Joshua. Gwajima alimshambulia sana Dk Slaa kama vile si Gwajima yule aliyepewa maono na Mungu kuwa Dk Slaa ndiye Joshua wetu watanzania.
Hapa CHADEMA, kwa unyumbu wao wakashangilia na kumuunga mkono, huku wakisaahu kuwa, Gwajima aliposema Dk Slaa anafaa kuwa rais na atashinda urais walimshangilia, leo Dk Slaa anashambuliwa na kupondwa kisa tu Dk Slaa si CHADEMA tena! Hivi, huyu Gwajima anawaonaje hawa CHADEMA na viongozi wao kama si MANYUMBU? Kwanini hawana akili ya kujiuliza na kujitafakari?
Si CHADEMA tu, hata kanisa lake pia lilimuunga mkono Gwajima alipomshambulia Dk Slaa, walifanya hivyo bila kumuliza askofu wao, kuwa huyu Dk Slaa unayemshambulia leo si ndiye huyu uliyesema kuwa Joshua wetu?
Tuendelee...
Katika ufunguzi wa kampeni za UKAWA jangwani, kama kawaida, pamoja na kumuombea na kumtabiria ushindi Lowassa, lakini alionesha pasina kigegezi chochote kuwa yeye anamunga mkono Lowassa hasa ukizingatia ni yeye ndiye aliyekuwa mshenga wa kufanikisha biashara ya kuuza chama na nafasi ya ugombea urais kwa Lowassa.
Baada ya matokeo kutangazwa ya urais, ikawa Lowassa kashindwa na Magufuli akatangazwa kuwa rais wa awamu ya tano. Matokeo yale yalimaanisha nini na yalituma ujumbe gani kwa kanisa na CHADEMA?
MOSI.
Kwa kanisa.
1.................
Waumini watafakari ukweli, nguvu, uwezo, na uaminifu wa Mungu wao. Haiwezekani Mungu awe kigeugeu kama mwanaume au mwanamke malaya. Sababu tunajua, malaya sifa yake kubwa ni ukigeugeu, mbili haikai moja haitulii, tatu yacheza, ili muradi tafarani, hamsini rasi hamsini majinuni, huyo ndio MUNGU wa kanisa la Gwajima.
Na hapa watu watatoka povu na kuniletea mifano ya Samweli kwa Sauli na Daud, kwamba Mungu mwanzo alimchagua Sauli, kisha akaachana na Sauli akamchagua mwana Yese kupitia kinywa cha Nabii Samweli.
Kuna tafauti kubwa kati ya maudhui ya kisa cha unabii wa Gwajima kwa Dk Slaa na Lowassa, na unabii Samweli kwa Sauli na Daud. Tafauti ni hizi zifuatazo.
*Unabii wa Samweli kwa Sauli na kwa Daud ulitimia. Mungu alimwambia Samweli kuwa Sauli atakuwa mfalme, na kweli akawa mfalme.
Rejea
1Samweli 9:19,
1Samweli 10:1
1Samweli 16:12-13
*Unabii wa Gwajima kwa Dk Slaa hakuwahi kutimia, Gwajima alimwambia Dk Slaa kuwa atakuwa Joshua wa kuivusha Tanzania, akimaanisha kuwa atakuwa rais, lakini ukweli Dk Slaa hakuwa Joshua, hakuwa rais na sanasana alimwagia mikosi badala baraka kwani Dk Slaa hata ndani ya chama chake hakupewa nafasi ya kugombea na kaishia kutukanwa na wanachama na viongozi wenzake.
*Unabii wa Samweli kuwa Sauli ametengwa na Mungu na ya kwamba ufalme wake atapewa jirani yake, ulitimia kwa Daud kuwa mfalme.
*Unabii wa Gwajima kwa Lowassa kuwa, atakuwa Joshua na rais wa Tanzania haukutimia.
Huenda watu wa Gwajima na Gwajima mwenyewe walijidanganya kuwa Mungu wao alimuacha Dk Slaa sababu alitenda dhambi, lakini, ukweli ni kwamba unabii kutoka kwa Mungu lazima kwanza utimie pamoja na mapungufu ya mwanadamu.
Mfano, wana wa Israeli walitabiriwa kumiliki nchi ya Kaanani, pamoja na dhambi zao walizozifanya lakini unabii ulikamilika. Mfano mwingine, Petro alitabiriwa kuwa mwamba wa kanisa, na kweli akawa mwamba wa kanisa na juu ya juhudi zake kanisa likajengwa na kuimarika, lakini Petro huyuhuyu ndiye akiyetenda dhambi ya kumkana Yesu mara tatu kwa fuuza. Nina mifano mingi toka katika biblia ju ya hili, ila naomba mufahamu kuwa dhambi si kikwazo cha kutimia unabii wa MUNGU, sababu MUNGU akiahidi lazima atimize.
Rejea
Mathayo 16:18
Mathayo 26:34
2..........
Kanisa linatakiwa kuzinduka, huenda Mungu ambaye Gwajima anamuabudu si huyu Mungu aliyebainishwa kwa kinywa cha Yesu Kristo kupitia ujumbe wake uliomo ndani ya injili ya takatifu.
Sababu sifa kuu za Mungu aliyebainishwa na Yesu na Kristo ni kutosema urongo, uaminifu, ukweli, haki, kuwa na nguvu kuu, kutimiza ahadi, na nyingine jaza wewe huku ukizingatia mafunzo ya Yesu Kristo.
Rejea Hesabu 23:19
"Mungu si mtu, aseme uongo...."
Ajabu sasa, Mungu wa Gwajima katabiri kuwa Lowassa tashinda, lakini hakushinda na kisingizio kikubwa cha kushindwa kwao ni wizi wa CCM uliobarikiwa na jaji Lubuva. Ni mungu gani anazidiwa ujanja, hila na mbinu na CCM? Huyo ni Mungu au ni wazimu? Waumini wa Gwajima kwanini hawajiulizi maswali haya? Kwanini hawatafakari?
Hata hivyo, sishangai sana na si ajabu, sababu kanisa la Yesu Kristo limevamiwa na matapeli na watu wanaojitajirisha kwa kutumia matatizo na ujinga wa watu. Huko Afrika Kusini BBC iliripoti kuwapo kwa mchungaji aliyewataka waumini wake watumie SUMU ya panya.
Si hivyo tulisikia kituko hukohuko Afrika Kusini waumini wakitakiwa wapige puchu ndani ya kanisa na kisha shahawa zilete upako kwao na kanisa, wako waliolishwa majani kama mbuzi, wapo wanaokanyagwa huku wakiombewa, ukijumlisha na lile sakata la Kibwetele ni mjinga pekee ndiye atakayekataa kuwa kanisa limechafuka. Kanisa limechafuka na watu kama wakina Gwajima ndio wachafuzi wa kanisa.
PILI.
Kwa CHADEMA.
Wanajua kuwa Lowassa kapelekwa CHADEMA chini ya uratibu wa Gwajima, na wanajua kuwa Gwajima alikuwa anamuunga mkono Lowassa katika uchaguzi ule.
Lakini baada ya Magufuli kushinda na kuanza kutumbua majipu mchana na usiku, Gwajima akatangaza kumuunga mkono Magufuli, si jambo baya, lakini jambo baya ni pale aliposema hakuwahi kumuunga mkono Lowassa na ya kwamba Arusha na Jangwani alikwenda kama kiongozi tu wa dini aliyeombwa kuombea MKUTANO ufanyike kwa amani.
Kwa kauli hii, kama kawa CHADEMA wakaanza tena kumponda Gwajima kwa kitendo chake cha kumuunga mkono Magufuli na kumkana Lowassa.
Baada ya Gwajima na Mbowe kuwapo katika orodha ya Makonda kama wauuza madawa ya kulevya, CHADEMA kwa nguvu zao zote wakaanza kuwatetea washukiwa hao pamoja na Gwajima. Na leo hii, walikaa kwa hamu KUBWA kumsikia Gwajima atasema nini mara baasa ya kutoka Sero. Wamesikia, na sasa mtandaoni habari ni Gwajima ni maneno yake dhidi ya Makonda.
Ila mimi nawaambia, kama Kibwetere aliweza kuchoma kanisa kwa jina la Yesu na kisha kukimbia na mali za wapendwa, kama mchungaji anaweza kuuza chumvi ya Tsh 100/= kwa milioni moja kisa tu kaimwagia upako, kama mchungaji unaweza kuumpa maelfu ya fedha na kisha asikupe chochote zaidi ya kukulisha majani kama meee; Mchungaji kama huyo anashindwa kuuza madawa ya kulevya kwa jina la Yesu ili apate kutajirika zaidi huku vijana wakihangamia, wakiteketea, na kuteseka?
"Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?"
Mathayo 7:21-22
MWISHO.
Huyo ndio Gwajima anayewaendesha CHADEMA na kanisa lake vile anavyotaka yeye, hiyo ndiyo Gwajima mfufua wafu na mponya UKIMWI na maradhi mengine, huyo ndiyo Gwajima mwenye utajiri mkubwa, huyo ndiye Gwajima aliyetazamwa jicho kali na Makonda Dodoma, huyo ndiye Gwajima aliyeshukiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya.
Na miye ndiye Dotto mwana wa Rangimoto, Njano5 ukipenda [HASHTAG]#JiniKinyonga[/HASHTAG].
0622845394
Morogoro.