Haiti: Waziri Mkuu kufanyiwa Mahojiano kuhusu Mauaji ya Rais

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Mwendesha mashitaka mkuu nchini Haiti amemtaka Waziri Mkuu Ariel Henry kuelezea sababu za kuzungumza kwa simu na mmoja kati ya washukiwa wa mauaji ya Rais Jovenel Moise usiku wa tukio lenyewe tarehe 7 Julai 2021.

Barua ya mwaliko iliyoandikwa kwa maneno ya hadhari inasema Henry alizungumza mara kadhaa kwa simu na mshukiwa mkuu wa mauaji ya Rais Mose, Joseph Felix Badio, wakati mshukiwa huyo, ambaye bado anatafutwa, alipokuwa bado karibu na eneo la mauaji.

Barua hiyo iliyotumwa na mwendesha mashitaka, Bed-Ford Claude, kwa waziri mkuu huyo siku ya Ijumaa (Septemba 10) inasema "ingawa ni rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuamuru kuitwa kwenye mahojiano kwa mtu mwenye cheo chako, lakini kwa sasa Haiti haina raisi, nami nakualika kuhudhuria na kutowa ushirikiano."

Claude alimwambia waziri mkuu kwamba angependa kuonana naye kuthibitisha mazungumzo yake na Badio, ingawa aliashiria kwamba halikuwa jambo la lazima kwake kukubali mwaliko huo.

Mahojiano hayo yatafanyika Jumanne ijayo (14 Septemba) saa 4:00 asubuhi kwenye Mahakama ya Kwanza ya mji mkuu, Port-au-Prince.
 
Hata Mke wa Raisi nae ana Cha kujibu yaan wapo wote kitandani na mme wake wanakula tunda Kisha jamaa analimwa Risasi zote zile lkn yeye anatoka na kamchubuko tu kama Cynthia rothrock kwenye movie
 
Back
Top Bottom