Haina ubishi mkoa wa Tanga umekamilika kuliko mikoa yote Tanzania

aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,650
3,662
Licha ya kuwa ndio umepangika kuliko mikoa yote Tanzania,
Lakini mkoa,wa Tanga ndio mkoa uliokamilika sana kiasi kwamba wakisema kila mkoa ujitegemee nahisi utakuwa mbali sana

Kwa uchache tu

Madini
Kuna dhahabu ya kutosha handeni na amani acha madini mengne

Uchukuzi
Bandari
Reli
Uwanja,wa ndege

Viwanda
Unga wa ngano pembe
Viwanda vya cement simba ,rhino
Viwanda vya mafuta sabuni na lotion
Viwanda vya soda healtho na anjari
Kiwanda,cha majani ya chai ya amani
Kiwanda cha nondo
Ambon plastic
Maji ya kunywa

Utalii
Kuna pwani ya pangani
Mbuga ya saadani
Shamba la vipepeo lushoto
Amboni

Michezo
Uwanja,wa mkwakwani
Timu,3 ligi kuu coastal union african,sports na mgambo jkt

Kilimo
Mahindi hapa ukienda mgambo jkt wanazalisha tani elfu 12 kwa mwaka bado pengine
Chai
Katani
Mihogo
Michikichi

Matunda
Maembe kule handeni dr idrs rashid ana heka 100 za miembe na ndio muuzaj mkubwa kwa bakhresa
Machungwa
Mananasi
Ma apple
Mafenesi

habari
Magazeti
Redio km mwambao na zngne
Tanga tv

Elimu shule za kutosha na bora
Shule za vipaji maalum
Vyuo,vya ufundi
Vyuo,vikuu

Bado kuwa na
Mtandao wake wa simu
Kiwanda cha bia
Kiwanda,cha nguo
Mkoa ukamilike
wp_ss_20160421_0003.png
wp_ss_20160421_0004.png
wp_ss_20160421_0003.png
wp_ss_20160421_0004.png
wp_ss_20160421_0005.png
wp_ss_20160421_0006.png
wp_ss_20160421_0008.png
wp_ss_20160421_0007.png
wp_ss_20160421_0009.png
wp_ss_20160421_0010.png
 
Umesahau fitna majungu na uchawi inaongoza na pamoja na kua na vyote hivyo ulovitaja hauendelei kwa sababu ya fitna na majungu

Wewe wasema hivyo, lakini hayo yote hutokana na kutoelimika na umaskini.

Hivyo viwili vikiwa clear hutasikia majungu na fitna ingawa hivi vipo kila mahala.
 
Mkuu aka2030, juzijuzi nikiwa kwenye ndege nimekutana na binti mmoja wa UK akanambia baba yake ana mashamba ya kakao kule Lushoto.

Lakini akasema sasa hivi huyo baba yake ni mzee na hajiwezi kuendeleza kilimo.

Mtu anatoka nje anakuja kulima kakao halafu anasafirisha kwenda nje na anawauzia Costa Café, na Starbucks, ilhali watanzania wapo hapohapo Tanga wanaendeleza fitna na majungu.

Hii inaumiza sana sometimes.
 
Wanatanga wajiandae kurudi Tanga.
Naipenda Tanga na sijawahi kujuta. Home sweet home. Karibuni Lushoto tupambane na Baridi.
Mtumba, mimi napenda hali ya baridi Lushoto ndo nimepanga ku-settle nikiwa pensioner.
 
Tanga Revisit.

Tanga Development Agency?

Tanga Strategic and Regeneration Agency?

Tanga Municipal- Website?

Tanga Buses

Wana- Tanga mpo?
 
Umesahau fitna majungu na uchawi inaongoza na pamoja na kua na vyote hivyo ulovitaja hauendelei kwa sababu ya fitna na majungu
Acha utoto, uropokaji, ubinafsi , ujinga, maradhi.. Watanzania ndo maana wanakaribia kutumia,, mwenzetu amatangaza utalii ameilezea tanga wewe ulipaswa kuunga mkono.... Sasa wote Watanzania tatizo nini tukisifia mikoa yetu?Acha fikra mbovu
 
We ndo unaona utoto mi ni mmoja wa wawekezaji mkoa wa tanga na nilipata tabu sana kutaka kuwekeza na hadi hapa navoongea nipo tanga hakuna kinachoendelea ni fitna na majungu tu watu wa tanga mawajua mimi maana asilimia kubwa ya vijana wa tanga hawawez kazi wao ni mirungi na majungu nimetembea mikoa yote tz na nimefanya nao kazi ila mkoa wa tanga nimechemka mimi kwa fitna zao
 
Regeneration Masterplan.

Tanga City Centre - Car Parks

Tanga Library

Tanga Bus Terminal

Tanga Railway Station

Tanga Airport

Haya maeneo yakiboreshwa na kuwa ya kisasa basi Tanga City itakuwa cool sana.

Mkuu aka2030 nakuomba unitafutie contacts za RC niwasiliane nae, maana nimepata mwamko wa kuendeleza mji wa Tanga.
 
We ndo unaona utoto mi ni mmoja wa wawekezaji mkoa wa tanga na nilipata tabu sana kutaka kuwekeza na hadi hapa navoongea nipo tanga hakuna kinachoendelea ni fitna na majungu tu watu wa tanga mawajua mimi maana asilimia kubwa ya vijana wa tanga hawawez kazi wao ni mirungi na majungu nimetembea mikoa yote tz na nimefanya nao kazi ila mkoa wa tanga nimechemka mimi kwa fitna zao

Haya mwenzetu, unawekeza kwenye eneo lipi?

Si vibaya tukipeana mawazo chanya kwenye hili.
 
Ama hakika Tanga imepangika mkuu aka2030

Hapa ni namna Tanga inayoonekana toka juu,inaonekana imepangika kwa mitaa na barabara nzuri,mpango mji bora kabisa kuliko hata JIJi pendwa la Dsm....Ama hakika waja leo waondoka kesho

Niliipenda Tanga sababu JKT nilifanya Kikosi cha Maramba,kule tulilima cocoa,maparachichi,nanasi,pilipili manga,passion na matunda yote unayoyajuwa...Maji bwerere ya mito na vijito

Kweli Tanga ni Mji,wajao na waje
image.jpeg
image.jpeg

Kwa sasa nipo hapa Majani Mapana napata supu ya pweza na juice ya Tende...Nilipoona uzi huu toka kwa ndugu yangu aka2030 nikasema wacha niitazame Tanga toka kwenye Satelite yangu...Hii ndio Tanga aliyopangwa na kupangika
 
Back
Top Bottom