Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango, kati ya Tsh.11.3 Trilioni zilizopangwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2016 -2017, mpaka sasa zimetolewa Tshs. Trilioni 3.9 tu ambazo ni sawa na asilimia 34 (34%) ya utekelezaji wa bajeti nzima. Hiyo ina maana, bajeti ya Maendeleo ya mwaka fedha uliopita, IMEFELI kwa asilimia 66.